BAADHI ya Viongozi na wanachama wa ngazi za juu kutoka vyama vya upinzani waliojiunga na CCM baada ya kuvutiwa na Sera za Chama cha Mapinduzi. |
NA IS-HAKA OMAR, DODOMA.
WANACHAMA
200 wakiwemo viongozi waandamizi wa kitaifa wa vyama vya upinzani wengi wakiwa
ni kutoka ACT Wazalendo, CHADEMA na CUF wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Viongozi
hao wamepokewa na Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa Kheir James kwenye hafla fupi
ya makaribisho iliyoandaliwa na umoja huo mkoa wa Dodoma na kufanyika Makao
Makuu ya CCM (White House) mjini hapa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti kwenye hafla hiyo baada ya kukabidhiwa kadi mpya aliyekuwa
Ofisa wa Sheria Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Mwantumu Mgonja, amesema ameamua
kujiondoa katika chama hicho kwa kukosekana uwazi, demokarsia na mipango
thabiti kama chama cha siasa.
Mwantumu alisema ndani ya
chama hicho licha ya kukosekana uwazi, uwajibikaji na ukosefu wa majadiliano
kwa msingi wa kujenga na kuendelea mbele, hakina malengo ya kuleta mabadiliko
aliyoyatarajia.
"Nimeona ni heri
nijiondoe kwenye chama ambacho hakina dira, mipango na sera lakini pia nimevutiwa
na utendaji wa serikali ya awamu ya tano katika kukuza dhana ya uzalendo na
kupigania matumizi ya rasimali za nchi kwa maslahi ya wananchi,"alieleza
Mwantumu.
Naye Julius Kamabrage
aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalebdo jimbo la Butima mkoani Mara na kuwa
mgombea wa ubunge katioka jimbo hilo, alisema upinzani umepoteza maana na
matarajio na sasa hauna ajaenda.
Kambarage
alisema ana idadi kubwa ya wenyeviti na wajumbe wa serikali za vijiji na
vitongoji kwenye wilaya na mkoa wa mara ambao wote watarejea CCM na kujiondoa
kwenye vyama vya upinzani.
"Upinzani
umekabidhiwa majimbo mawili mkoa wa Mara pamoja na kuongoza halmashauri mbili
za wilaya, lakini hakuna lolote wanalolifanya huku wananchi wakikosa uwakilishi
sahihi na kuweza kutatua shida na matatizo yao,"Alieleza Kambarage.
Kwa upande wake mwenyekiti
mpya wa UVCCM Taifa, Kheir James, aliwakaribisha vijana hao katika kikosi cha
ushindi na kuwataka kuongeza nguvu ya ushindi na kujenga Chama imara
kinachotumainiwa na wananchi wote.
Kheir
alisema vijana wote hawana mahali pa kwenda na sehemu sahihi kwao ni CCM, hivyo
kurudi kwao ndani CCM kutafungua milango zaidi ya kuitumikia nchi, kuwa watii,
wazalendo na wenye wajibu wa kujituma na kuzalisha mali.
Kati ya wanachama 200
waliojiunga na CCM 15 kati yao ndiyo waliokabidhiwa kadi mpya za Chama akiwemo
Mwantumu, Mwenyekiyti wa Vijana Mkoa wa Mwanza kupitia ACT Wazalendo, Ramadhani
Itenya, Katibu wa chama hicho Mkoa wa singida, Loth Thomas, Aliyekuwa
Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Mabibo, Dar es Salaam, Jackob Mosha na
aliyekuwa Ofisa Utawala ACT Wazalendo, Emmanuel Kitundu.
Wengine ni Mwenyekiti wa
Vijana ACT Wazalendo Wilaya ya Ilala, Rose Peter, Mwenyekiti wa chama hicho
Jimbo la Singida Mjini, Nkamia John, Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Mwwanza,
Robert Gwanchele, aliyekuwa msanii wa CHADEMA, Andrew Mgalama, Pascal Waruba
kutoka ACT Wazalendo Wilayaya Tarime, Katibu Mipango na Uchaguzi ACT Wazalendo
Tarime, Anthon Mrigini Katibu wa Vijana Wilaya ya Tarime, Yaassin Daud na
Julius Sinda Katibu wa CUF Wilaya ya Tarime.
Hafla
hiyo alihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo, Naibu
Katibu Mkuu wa CCM (Zanbzibar) Dk. Abdalla Juma Mabodi, Katibu wa Halmashauri Kuu
ya (NEC) ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi, Hamprey Polepole na Katibu wa NEC,
Oganaizesheni na Siasa, Pereira Ame Silima.
Wengine ni Makamu Mwenyekliti wa UVCCM Taifa, Tabia Mwita, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCC, Shaka Hamadu Shaka na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Asia Halamga na Mwenyekiti wa umoja huo mkoani humo, Bill Chidabwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni