Jumamosi, 16 Desemba 2017

MATUKIO KATIKA PICHA MAPOKEZI YA VIONGOZI WAPYA WA UWT NGAZI YA TAIFA MKOANI DODOMA.

 MWENYEKITI wa UWT Taifa, Gaudencia Kabaka akihutubia katika hafla ya Mapokezi ya viongozi wapya wa Umoja huo ngazi ya Taifa iliyoandaliwa na UWT Mkoa wa Dodoma, na kufanyika katika viwanja vya White House Makao Makuu ya CCM Dodoma.

 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa, Thwaiba Kisasi  akitoa salamu zake kwa Akina Mama wa Mkoa wa Dodoma katika hafla ya Mapokezi ya viongozi wapya wa Umoja huo ngazi ya Taifa iliyoandaliwa na UWT Mkoa huo, hafla iliyofanyika katika viwanja vya White House Makao Makuu ya CCM Dodoma.

 KATIBU wa UWT Mkoa wa Dodoma, Kaundime Kassase akisoma taarifa ya utekelezaji ya Mkoa huo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

 KATIBU Mkuu wa UWT Taifa, Amina Makilagi, akizungumza na Akina Mama wa UWT walioudhuria hafla hiyo.

 MWENYEKITI wa UWT, Gaudencia Kabaka (kushoto) akisalimiana na mwanachama mpya wa CCM Dinna John (kulia) katika hafla hiyo.

 VIONGOZI mbali mbali wa UWT Taifa wakiungana na wanachama wapya katika kula kiapo cha utii kwa wanachama wapya.

 WANACHAMA wapya 1700 waliojiunga na CCM wakila kiapo cha utii katika hafla hiyo.

 NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akizunguma katika hafla ya kuwakaribisha viongozi wapya wa UWT Taifa Mjini Dodoma. 
 KIKUNDI cha Ngoma ya Asili cha Mkoa wa Dodoma kikitoa burudani katika hafla hiyo.


 BAADHI ya wanachama wapya waliojiunga na CCM na kukabidhiwa kadi za uanachama kupitia hafla hiyo.

 AKINA Mama wa UWT walioudhuria hafla hiyo wakiwa katika ubora wao wa kutabasamu huku wakifuatilia matukio mbali mbali yanayofanyika katika mkutano Mkuu huo.

 BAADHI ya viongozi wa UWT wakiwa katika hafla hiyo.

 MEZA Kuu ya viongozi wa ngazi ya Taifa wa UWT wakifuatilia burudani mbali mbali zinazotolewa kwa ratiba maalum katika hafla hiyo.
 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Thwaiba Kisasi akivishwa shuka nyeupe na akina Mama wa Mkoa wa Dodoma ambalo ni miongoni mwa vazi rasmi la utamaduni wa Mkoa huo.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni