Baadhi ya Wananchi waliovutiwa na hotuba ya Katibu Mkuu Ndg.Kinana,ilibidi wasogee zaidi na kuendelea kusikiliza.
TAARIFA NA IS-HAKA OMAR..
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa, Abdulrahman
Omar Kinana amewataka wanachama wa Chama
hicho kutofanya makosa ya kuchagua kiongozi asiyekuwa na msimamo wala uzalendo
wa kweli kwa jamii anayoitumikia.
Maelekezo hayo ameyatoa jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM kabla hawajapiga kura ya maoni za kumchagua mwana CCM atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo utakaofanyika hivi karibuni kumtafuta Mbunge wa jimbo la Singida
Kaskazini.
Katibu Kinana, amewambia wanachama hao kwamba CCM kwa sasa
haina muda wa marumbano wala kujadili wanasiasa na vyama vilivyopoteza muelekeo
kisiasa, bali chama kina muda wa kutatua kero za wananchi.
Amesema kwa sasa wananchi wanatakiwa kuendelea kumuunga
mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kupambana na vitendo vya
rushwa na ufisadi.
“Sote ni mashahidi jinsi serikali ya awamu ya tano
inavyopigania haki na maisha ya wananchi wote bila ubaguzi wa dini, kabila na
rangi wote mnapata haki sawa.
Pia ni wakati wenu wa kuwakataa wanasiasa uchwala na madalali
wa kisiasa wenye nia ya kujineemesha wao huku wananchi mkibaki na dhiki, chama
pekee chenye sera zinazojali na kuthamini maisha ya watu ni CCM wala hakuna
kingine”.amewambia wanachama hao Kinana.
Uchaguzi huo utafanyika kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo,
Lazaro Nyarandu kwa tiketi ya CCM Kujivua uachama wa Chama cha Mapinduzi na
kujiuzulu nyadhifa zake zote.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni