Jumamosi, 21 Desemba 2019

MATUKIO KATIKA PICHA KONGAMANO LA WIKI YA KACHORORA Z'BAR.


 NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la wiki ya Kachorora huko ukumbi wa Kituo cha kulelea Wazee Sebleni Zanzibar.

 BAADHI ya Wajumbe wa Maskani ya Kachorora pamoja na Maskani jirani za CCM walioudhuria katika hafla ya Wiki ya Kachorora,wakisikiliza mada mbali mbali zinazotolewa katika kongamano hilo zikiwemo mada za udhalilishaji wa kijinsia,Dhana ya kuanzishwa Maskani za CCM na Mafanikio ya Serikali ya awamu ya Saba.


 Ndugu Said Shaaban akiwasilisha mada ya Dhana ya kuanzishwa kwa maskani za CCM , kwa Wana Maskani hao.

 Ndugu Khamis Rashid Mbarouk akiwasilisha mada ya Unyanyasaji wa Kijinsia, katika kongamano hilo la wiki ya Kachorora.


 Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo, akifunga kongamano hilo la wiki ya kachorora.

MHE.ASHA AKING'ARISHA KITUO CHA UJASIRIAMALI CHA UWT


MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Mhe.Asha Abdulla Juma akikabidhi Vifaa vikiwemo vitambaa pamoja na Vyerehani kwa Mwenyekiti  wa Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Mjini Habiba Nassib Suleiman kwa ajili ya Kituo cha Elimu Amali UWT Wilaya ya Mjini.

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Mhe.Asha Abdulla Juma akizungumza na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya mjini wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali kwa ajili ya kituo cha elimu amali UWT wilaya ya mjini iliyofanyika katika kituo hicho Mwembe Matumbaku Wilaya ya Mjini unguja.

MWENYEKITI wa UWT Wilaya ya Mjini Ndugu Habiba Nassib Suleiman akimkabidhi zawadi maalum Mbunge wa Viti Maalum  Mkoa wa Mjini Mhe.Asha Abdulla Juma katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa kituo cha elimu amali UWT wilaya ya mjini iliyofanyika katika ukumbi wa chuo hicho mwembe matumbaku wilaya ya mjini unguja.

katibu wa UWT wilaya ya Mjini akizungumza na baadhi ya viongozi na wa jumuiya hiyo wakati wa makabidhiano ya vifaa mbalimbali kwa ajili ya kituo cha elimu amali UWT wilaya ya mjini uliotolewa na mbunge wa viti maalum ccm mkoa wa mjini Asha Abdulla Juma.





MBUNGE wa viti maalum wa Mkoa wa Mjini,Mhe Asha Abdulla Juma amefurahishwa na hatua ya Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi ya wilaya ya Mjini kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi kwa kuhakikisha vijana wanajikwamua kiuchumi.

Amesema kitendo cha UWT kuwakusanya vijana tofauti ndani ya mkoa huo kwa lengo la kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali ili waweze kuondokana na hali ya utegemezi ambapo baadaye wakipata ujuzi wanajishughulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kujiingizia kipato ni moja ya sehemu ya maagizo ya ilani pamoja na viongozi wa chama.

Kauli hiyo ameitoa wakati akikabidhi vifaa vya ushonaji ikiwemo chereheani mbili,meza pamoja na vitambaa vya kutengeneza mapambo katika kituo cha mafunzo ya amali cha UWT wilaya ya mjini ambapo alisema hiyo ni ahadi za CCM katika kuwakusanya vijana na kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kuondokana na utegemezi.

Amesema baada ya kuona Jumuiya hiyo imeanzisha kituo hicho cha mafunzo kwa ajili ya vijana akaiona aunge mkono juhudi hizo za kuhakikisha vijana hao wanaokombolewa dhidi ya ukosefu wa ajira ili kuongeza uzalishaji nchini kama maagizo ya viongozi wa CCM wanavyoelekeza.

"Nina amini chuo hichi kitasaidia sana juhudi hizi kwa vijana wetu na ndio maana nikaona nilete nguvu kwenye kituo hichi cha UWT hasa kwa wakina mama katika kujifunza ujasiriamali wa ushonaji,upishi na mambo mengine,"ameeleza

Naye Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mjini,Habiba Nassir Suleiman amesema lengo la uongozi wa wilaya hiyo ni kuendelea  kubuni miradi itakayosaidia kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira na ongezeko la uzalishaji kwa lengo la kukuza uchumi kama inavyoelekeza CCM.

Amesema uongozi wa UWT wilaya imeamua kufanya ubunifu wa aina hiyo wa kuwakusanya vijana na kuwapatia mafunzo ya ujuzi wa shughuli za ujasiriamali ambapo kwa namna moja ama nyingine itawasaidia sana wanawake katika kuondokana na hali ya utegemezi na kuweza kujikwamua kiuchumi.








Ijumaa, 20 Desemba 2019

BI.CATHERINE- AWAWEKA KIKAANGONI ACT-WAZALENDO.

 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM Zanzibar Bi.Catherine Peter Nao,akizungumza na Vyombo vya Habari leo Tarehe 20/12/2019.



CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimekitaka Chama cha ACT-Wazalendo kuacha siasa za maji taka na kishamba zilizopitwa na wakati zinazolenga kuhatarisha amani ya nchi.  

Kimesema Viongozi wa ACT-Wazalendo wameendelea na mikakati michafu ya kutafuta umaarufu na huruma ya kisiasa kupitia matamshi yenye uchochezi,kashifa,dharau na upotoshaji dhidi ya Viongozi wa Serikali na CCM.

Akizungumza Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar,Catherine Peter Nao, amesema CCM haitovumilia mwenendo wa siasa za maji taka za kuwatukana na kuwadhalilisha Viongozi wa Serikali na Chama hicho zinazofanywa na ACT-Wazalendo.

Catherine, ameendelea kuvitaka Vyombo vya Dola nchini kuchukua hatua za haraka dhidi ya wanasiasa hao wachochezi wanaotumia vibaya uhuru wa kisiasa kwa kuwadhalilisha viongozi wa umma.

"Siku za hivi karibuni tumeona namna viongozi ACT-Wazalendo walivyomtukana Naibu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Mhandisi Hamad Yussuf Masauni mitandaoni na Jeshi la Polisi lipo na halijachukua hatua stahiki.

Wenzetu hao baada ya kushindana kwa hoja na kufanya kazi za Wananchi wao wanakuja na mtindo wa matusi sasa tunawaonya na wasipoacha tabia hiyo wajue ushahidi wa maovu yao tunao na tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria.", amesema Catherine Peter nao.

Kupitia mkutano huo Catherine alilaani hatua ya upotoshwaji unaofanywa na chama cha ACT-Wazalendo kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura ambalo linatarajia kuanza uandikishwaji visiwani hapa Januari 18  hadi Machi 4 mwaka 2020.

Amesema mchakato wa uandikishaji wa daftari hilo upo kikatiba na kidemokrasia hivyo usichafuliwe kwa hoja dhaifu na wanasiasa  wanaoweka mbele maslahi yao  badala ya maslahi ya nchi.

Ameongeza kuwa mshakato huo ndio chimbuko la uwepo wa uchaguzi mkuu ujao hivyo panahitajika ustaarabu kwa vyama vyote vya kisiasa nchini.

Katibu huyo Catherine amesema kinachofanywa na ACT-Wazalendo ni kuwajengea hofu wananchi kwa lengo la kukwamisha ukamilishaji wa uandikishwaji wa daftari la wapiga kura ambapo jambo hilo lipo kwa mujibu wa sheria.

"Tunahitaji siasa za kistarabu pamoja na mchakato huu ambao unaanza wa uandikishwaji wa daftari hilo la wapiga kura hivi karibuni ufanyike kistaarabu na hakuna sababu ya kuwepo kwa hali ya uvunjifu waamani,"amesema.

Catherine amesema CCM haifanyi kazi ya uandaaji wa vitambulisho bali inafanya kazi za siasa na kwamba katika Ofisi ya Chama hakuna kitu kama hicho ambacho ACT-Wazalendo wanadai shutuma hizo.

Katika maelezo yake Katibu huyo, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kuchukua vitambulisho vyao vya Mzanzibar Mkaazi pamoja na kujiandisha katika daftari la wapiga pindi wakati utakapofika.  

Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi,Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Salim Abdallah Bimani alishutumu kuwa CCM imeandaa njama za kuwaandikisha vijana ambao hawajatimia umri wa kupiga kura lengo likiwa kuongeza idadi ya kura kwa Chama, madi ambayo ni uongo na yanatakiwa kupuuzwa na Wananchi wote.




Jumapili, 1 Desemba 2019

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM DR.BASHIRU MKOA WA MAGHARIB KICHAMA.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,akizungumza na Wana CCM katika ziara ya Katibu Mkuu Dkt.Bashiru Ally,akivishwa Skafu na Vijana Maalum wa UVCCM Wilaya ya Dimani baada ya kuwasili katika Ofisini hiyo kwa ajili ya kuanza ziara yake katika Mkoa wa Magharibi.

VIONGOZI mbali mbali wa CCM Mkoa wa Magharibi na Wilaya zake wakisikiliza maelekezo ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally, wakati akizungumza katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoani humo.

 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Magharib kichama ndugu Mohamed Rajab Soud, akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally, kwa ajili ya ziara yake Mkoani humo.

 BAADHI ya Viongozi walioshiriki ziara hiyo wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,wakati akizungumza na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Magharibi.

 BAADHI ya Viongozi walioshiriki ziara hiyo wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,wakati akizungumza na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Magharibi.

KATIBU  Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally, akiangalia mkoba wa asili wa ukili uliotengenezwa na Wajasiriamali wa Mkoa wa Magharibi huko katika Soko la Mboga mboga la Mombasa wakati wa ziara yake.


 KATIBU  Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally akiwa na Viongozi wengine na Wajasiriamali katika Picha ya Pamoja.

 KATIBU  Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally, akikagua Jengo la Ofisi ya Tawi la CCM Fuoni Kiembeni mara baada ya kuweka Jiwe la msingi.

 WANA CCM na Viongozi mbali mbali walioudhuria katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Tawi la CCM Fuoni Kiembeni.

 WANA CCM wa Tawi la Fuoni Kiembeni akimkabidhi zawadi ya madafu Katibu  Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,akizungumza na Wana CCM wa Tawi la Fuoni Kiembeni mara baada ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Tawi hilo.

KATIBU  Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,akiweka jiwe la msingi Tawi la CCM Pangawe.
KATIBU Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chipukizi Jimbo la Pangawe.



KATIBU  Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,akizungumza na Wana CCM wa Tawi la Pangawe. 
 MWENYEKITI wa Tawi la CCM Kitundu akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,katika Tawi hilo hili 



 KATIBU Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,akizungumza na Wana CCM wa Tawi la Kitundu.

 VIONGOZI mbali mbali wa CCM wakiwa katika Ukumbi wa Wakorea Dole ambapo Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally amezungumza na Kamati za Siasa na Mikakati za ngazi za Matawi,Wadi,Jimbo na Wilaya ya Mfenesini.

 MAELFU ya Wana CCM waliojitokeza katika Mkutano huo wa Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally.

 KATIBU wa CCM Wilaya ya Mfenesini ndugu Jumanne Kimtende, akizungumza na kuwatambulisha Viongozi mbali mbali kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,alipokutana na kamati hizo.
 MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Mfenesini ndugu Kesi Mashaka Ngusa akizungumza katika Kikao hicho.



 KATIBU Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,akizihutubia Kamati hizo huko katika ukumbi wa Wakorea  uliopo Dole Unguja.

 KATIBU Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,akikabidhiwa zawadi mbali mbali na Viongozi wa CCM Wilaya ya Mfenesini.

Alhamisi, 28 Novemba 2019

MATUKIO KATIKA PICHA UZINDUZI WA MAGHARIBI YA KIJANI LEO TAREHE 28/11/2019


 KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Bashiru Ali Kakurwa ,akivishwa Skafu mara baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Mkoa wa Magharibi huko Mwera.
 


KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Bashiru Ali Kakurwa,akielekea katika Ofisi za CCM Mkoa wa Magharibi kichama Mwera Zanzibar. 

 BAADHI ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharibi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Bashiru Ali Kakurwa akizungumza na wajumbe hao. 

 KATIBU wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndugu Mgeni Mussa Haji akikabidhi Taarifa ya CCM ya Mkoa huo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Bashiru Ali Kakurwa.

 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Magharibi ndugu Mohamed Rajab Soud akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.

 KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Bashiru Ali Kakurwa,akizungumza na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Magharibi Unguja.

 KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Bashiru Ali Kakurwa ,akikagua vikundi vya Ujasiriamali vilivyoshiriki katika uzinduzi wa kampeni ya Magharibi ya Kijani iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Zanzibar.

 BAADHI ya Wanachama wa CCM walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa Magharib ya Kijani iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Mwalimu Nyerere Zanzibar.

 

 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Magharib ndugu Mohamed Rajab Soud akimkabidhi zawadi Katibu  Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Bashiru Ali Kakurwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Magharib ya kijani .


















Jumapili, 27 Oktoba 2019

NDG.CASSIAN -AZINDUA KITUO CHA UJASIRIAMALI JANG'OMBE.


 KATIBU wa Kamati Maalumu ya NEC,idara ya Organazesheni CCM Zanzibar ndugu Cassian Galos Nyimbo(wa pili kutoka kulia),akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha mafunzo ya ujasiriamali cha Jimbo la Jang'ombe,Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe.Ramadhan Hamza Chande (wa kwanza kushoto) na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Jimbo hilo (wa kwanza kutoka kulia).
KATIBU wa Kamati Maalumu ya NEC,idara ya Organazesheni CCM Zanzibar ndugu Cassian Galos Nyimbo akihutubia wananchi katika uzinduzi wa Kituo cha ujasiriamali Jang'ombe.
MWAKILISHI wa Jimbo la Jang'ombe Mhe.Ramadhani Hamza Chande,akizungumza katika hafla hiyo.




BAADHI ya Waalikwa na wanafunzi wa kituo hicho wakisikiliza nasahas mbali mbali kutoka kwa viongozi wa JImbo la Jang'ombe.

MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Mjini ndugu Kamaria Suleiman Nassor,akitoa shukrani katika hafla hiyo.

KATIBU wa Siasa na Uenezi CCM Jimbo la Jang'ombe akizungumza katika hafla hiyo.


KATIBU wa Kamati Maalumu ya NEC,idara ya Organazesheni CCM Zanzibar ndugu Cassian Galos Nyimbo,amewataka Wanawake na Vijana wa jimbo la jang'ombe kutumia vizuri fursa ya ujasiriamali kwa kujiajiri wenyewe.

Wito huo ameutoa wakati akizindua Kituo cha Mafunzo ya Ujasiriamali cha Jimbo la Jang'ombe kilichoanzishwa na Mwakilishi wa Jimbo hilo uko Kilimani Mnara wa mbao Unguja.

Amesema ujasiriamali ni kazi kama zilivyo kazi zingine katika jamii hivyo ujuzi unaotokana na sekta hiyo unatakiwa kuthaminiwa na kupewa kipaumbele.

Galos ameeleza kuwa mafunzo hayo ya ujasiriamali watakayopewa wananchi wa jimbo hilo kupitia Kituo hicho yawe na tija ya kujikwamua kichumi na kujiongezea kipato.

Katika maelezo ya Katibu huyo, amempongeza Mwakilishi huyo kwa ubunifu wake wa kuanzisha Kituo kitakachozalisha wataalumu wengi wa masuala ya ujasiriamali wenye uwezo wa kutengeneza bidhaa mbali mbali zenye viwango.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Jang'ombe Mhe.Ramadhani Hamza Chande,alisema lengo la kuanzisha kituo hicho ni kuwapatia ujuzi wa masuala ya ujasiriamali wananchi wa jimbo hilo hasa vijana na wanawake.

Amesema wakati alipokuwa akiomba wananchi wampatie ridhaa ya uongozi aliahidi kuanzisha kituo hicho cha kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kwa sasa tayari ametekeleza ahadi hiyo.

Amesema katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020 imeelekeza uanzishwaji wa vituo vya mafunzo  ya ujasiriamali nchini, hivyo jimbo hilo wametekeleza maelekezo ya Ilani.

Amesema kituo kimesajiliwa na kupitia taratibu zote za kisheria pia wana wakufunzi waliobobe katika kufundisha utengenezaji wa bidhaa bora zinakubalika katika soko la ndani na kimataifa.

Aidha ameeleza kuwa kituo hicho kwa awamu ya kwanza kinatarajia kutoa Wanafunzi zaidi ya 300 na kitakuwa ni endelevu.

Akitoa shukrani katika hafla hiyo Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini ndugu Kamaria Suleiman Nassor, amewapongeza viongozi wa jimbo la Jang'ombe kwa ushirikiano wao uliozaa matunda ya kuanzisha kituo hicho kitakachowanufaisha Vijana wengi.

Amewasihi vijana wa jimbo hilo kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiunga kituo hicho ili wapate ujuzi utakaowawezesha kutengeneza bidhaa zitakazowapatia kipato.