Jumanne, 30 Aprili 2019
Ijumaa, 26 Aprili 2019
RC AYOUB- ATAKA MUUNGANO ULINDWE NA KUTHAMINIWA.
NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa
akitoa maelezo juu ya Bonanza hilo. |
MATEMBEZI ya UVCCM kupitia Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu
wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe.Ayoub Mohamed. |
WASHIRIKI wa matembezi hayo ambao ni Vijana wa UVCCM
kupitia Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu wakifanya mazoezi ya kunyoosha viungo mara
baada ya Matembezi katika Viwanja vya Maisara. |
WASHIRIKI wa matembezi hayo ambao ni Vijana wa UVCCM
kupitia Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu wakicheza Mpira wa Nage. |
VIJANA nchini wametakiwa kujitathimini na kujipima kifikra juu ya mwenendo wao wa uzalendo kama unaenda sambamba na dhamira ya Waasisi wa Muungano wa Serikali mbili ya Zanzibar na Tanganyika.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mjini na Magharib Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud wakati akiwahutubia Vijana zaidi ya 700 katika Bonanza la UVCCM kupitia Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika maadhimisho ya Kilele cha miaka 55 ya Muungano wa Tanzania, huko katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Amesema ni muda wa Vijana wa sasa kujipanga vizuri kwa kuendeleza mema yaliyoasisi na Waasisiwa wa Muungano huo ambao ndio chimbuko la maendeleo endelevu ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Ameongeza kuwa lengo la Muungano huo ni kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa Nchi zote mbili unaimarika sambamba na kukua kwa Uchumi.
Ameeleza kwamba dhamira ya Wazee walioasisi Muungano huo waliamini kwamba maendeleo ya Nchi yoyote Duniani yanapatikana baada ya kuwepo kwa Amani na Utulivu ya kudumu.
Katika maelezo yake Mhe.Ayoub,amesema ni wajibu wa kila kijana kulinda Muungano huo, uliobeba mafanikio na matumaini ya Mamilioni ya Watanzania.
Amesema wapo baadhi ya Watu wanaopotosha juu ya Muungano kwa kudai hauna maslahi hali ya kuwa wao wananufaika na fursa mbali mbali zinazopatika katika Muungano huo.
"Vijana nakuombeni tuendelee kuwa Wamoja katika kulinda Muungano huu ili Nchi zetu ziendelee kustawi Kiuchumi,Kisiasa na Kijamii", amesema RC Ayoub.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa amesema lengo la Matembezi hayo ni kuunga mkono juhudi za Waasisi waliobuni jambo la kimaendeleo la kuanzisha Muungano, kama Chombo rasmi cha kulinda maslahi ya Wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini 'B' Mhe.Rajab Ali Rajab, amewataka Vijana Wasomi kuwa Mabalozi wazuri wa kuelimisha Jamii juu ya faida zilizopatikana katika kipindi cha miaka 55 ya Muungano huo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu ya UVCCM Zanzibar Ndugu Masoud Shibli Makame amesema katika Sekta ya Elimu Vijana wa Zanzibar wananufaika na fursa ya Mikopo miwili ya Elimu ya Juu hatua inayochochea upatikanaji wa Wasomi wengi Nchini.
Bonanza hilo limetanguliwa na Matembezi ya Vijana zaidi ya 700 kutoka Taasisi za Elimu ya Juu pamoja na UVCCM wa Mikoa mbali mbali ya Zanzibar sambamba kuchezwa Michezo mbali mbali ikiwemo Mpira wa Nage,Mpira wa Miguu na kuvuta kamba.
DK.MABODI ATANGAZA NEEMA KIJIJI CHA KIKOBWENI, MHE.NADIR AELEZA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM 2016-2017.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizungumza katika Mkutano wa Jimbo wa Jimbo la Chaani wa kuelezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM. |
MWAKILISHI wa Jimbo la Chaani Unguja Mhe.Nadir Abdul-Tif Yussuf akizungumza na Wananchi katika Mkutano wa Jimbo hilo katika uwanja wa Mpira wa Kijiji cha Kikobweni Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja. |
BAADHI ya Wananchi wa Jimbo la Chaani wakisikiliza kwa makini taarifa mbali mbali za Utekelezaji wa Ilani katika Jimbo hilo. |
NAIBU
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abudlla Juma Saadalla
Mabodi amesema CCM itachimba Kisima cha Maji Safi na Salama kwa muda wa wiki
mbili ili kuondosha changamoto ya ukosefu wa nishaji hiyo kwa Wananchi wa
Kijiji cha Kikobweni Jimbo la Chaani Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja.
Ahadi
hiyo ameitoa katika Mkutano wa Jimbo la Chaani wa kueleza utekelezaji wa Ilani
ya CCM kwa Chama na Serikali,ambapo baadhi ya Wananchi wa kijiji hicho wamedai
kuwa na upungufu wa huduma za maji ambapo kwa sasa wanatumia maji kisima cha
zamani ambacho hakikidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa wananchi hao.
Dk.Mabodi
amesema kwa hatua ya awali anatoa kiasi cha shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya
maandalizi ya uchimbaji wa kisima hicho ili wananchi wa kijiji hicho na vijiji
jirani wapate huduma hiyo kwa wakati hasa katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa
kuanzi hivi karibuni.
Amesema
wananchi wana haki ya kueleza changamoto
zinazowakabili kwa viongozi wao waliowapa ridhaa ya kuwaongoza katika ngazi
mbali mbali za kiuongozi katika Chama na Serikali.
Amesema
CCM ni Taasisi ya Kisiasa inayoahidi na
ikatekeleza kwa vitendo na kwa wakati mwafaka na haitoi ahadi za kuwalaghai Wananchi kama vinavyofanya baadhi ya vyama vya upinzani kuwa wataijenga
Zanzibar kwa Siku 100 iwe kama Nchi ya Singapore.
Amesema
Maendeleo hayana itikadi wala misimamo
ya kisiasa kwani inapotekelezwa Ilani ya CCM kwa kuwafikishia wananchi huduma
za maji,Umeme,Bababara na Vituo vya Afya fursa hizo hazitumiwi na Wanachama wa
CCM pekee yao bali wananufaika wananchi wote.
Ameeleza
kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwa sasa inatekeleza Ilani ya CCM kwa kujenga Barabara yenye kiwango cha Lami
katika Mkoa wa Kaskazini Unguja ili kurahisisha huduma za Usafiri kwa Wananchi
wa Mkoa huo.
Katika
maelezo yake Dk.Mabodi amewambia Wananchi wa Jimbo la Chaani kwamba Serikali
ipo katika hatua za kutekeleza Mradi mkubwa wa Maji Safi na Salama ambapo
ukikamilika utamaliza changamoto ya upungufu wa huduma za maji Mkoani humo.
Kupitia
Mkutano huo Dk.Mabodi ameeleza kuridhishwa kwake na Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo hilo, licha ya
kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo zinazotafutiwa ufumbuzi wa kudumu na viongozi
wa jimbo hilo.
Amewataka
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo watatue changamoto zilizopo katika maeneo
mbali mbali ya jimbo hilo ili Chama kishinde bila vikwazo katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Amesema
CCM inapozungumzia ushindi wake wa
Kihistoria katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020, ni kutokana na utekelezaji
mzuri wa ahadi zilizotolewa kupitia Uchaguzi Mkuu uliopita.
Pamoja
na hayo amewasihi wananchi wa Jimbo hilo kuthamini miradi ya maendeleo
inayotekelezwa kwani kuna baadhi yao wamekuwa wakihujumu miradi hiyo kwa
makusudi hali inayokwamisha baadhi ya fursa za kimaendeleo.
"
Nimeshuhudia katika Mkoa huu inahujumiwa miondombinu ya Maji Safi na Salama kwa
kuiba vifaa vya umeme,kuharibiwa kwa Gari ya wagonjwa na matukio mengine ya
kukatisha tamaa na yote hayo yanatekelezwa na watu wachache wapinga maendeleo.",ameeleza Dk.Mabodi.
Amewaonya
baadhi ya Watendaji na Viongozi wa Ngazi
za Majimbo katika Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja, wanaojihusisha na mipango ya
kuwaandaa Wagombea wa ngazi mbali mbali
za Uongozi kabla ya muda wa kufanya hivyo kufika kwani kufanya hivyo ni kukiuka
Katiba ya CCM ya mwaka 1977 na miongozo yake.
Pamoja
na hayo amesema CCM itaendelea kulinda
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa gharama yeyote na atakayejaribu kubeza
atakuwa ni msaliti na adui wa Taifa.
Akitoa
Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe.Nadir
Abdul-Tif Yussuf amesema kwa kipindi cha mwaka 2016-2017 alitekeleza masuala
mbali mbali yakiwemo kuvipatia fedha za mitaji vikundi vya
ujasiriamali,alinunua Gari maalum la Wagonjwa,kuweka Taa za umeme za kuwasha
usiku Viwanja Vitatu,kujenga visima vya Maji Safi na Salama pamoja na kununua
mashine za Kilimo za Power Tiller kwa ajili ya shughuli za Kilimo.
Miradi
mingine iliyotekelezwa ni pamoja na matengenezo ya Ofisi mbali mbali za
CCM,ununuzi wa Dawa za Binadamu katika Vituo vya Afya mbali mbali mbali pamoja
na ununuzi wa Vyarahani 10 kwa ajili ya vikundi vya Jimbo.
Mhe.Nadir ametoa tahadhari kwa baadhi ya Watu wanaotengeneza
makundi ya kuwagawa na kuwafitinisha viongozi wa Jimbo hilo uku wakipanga
wagombea kinyume na utaratibu na kuongeza kwamba watu hao hawakitakii mema
Chama Cha Mapinduzi.
Wakizungumza
kwa wakati tofauti Wananchi wa Jimbo hilo mara baada ya Mkutano huo,wameeleza kwamba
wamenufaika sana na miradi inayotekelezwa na fedha za Mfuko wa Jimbo wa
Mwakilishi.
Jumatano, 24 Aprili 2019
CCM MKOA WA MAGHARIB YAENDELEA NA ZIARA YAKE JIMBO LA KIEMBE SAMAKI UNGUJA.
DIWANI wa Wadi ya Mbweni Unguja Ndugu Maabadi Ali Maulid akitoa maelezo juu ya usambazaji wa mipira ya maji Safi na Salama katika maeneo mbali mbali ya Wadi hiyo. |
KAMATI ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharib wakikagua Mradi wa Maji Safi na Salama uliotekelezwa chini Mfuko wa Jimbo la Kiembe Samaki katika ziara yao ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM. |
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Magharibi Unguja kimewataka Viongozi wa Jimbo la Kiembe Samaki kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ili kutatua kwa wakati mwafaka changamoto zinazowakabili Wananchi.
Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Ndugu Mohamed Rajab Soud katika mwendelezo wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo la Kiembe Samaki.
Amesema pamoja na kutekelezwa kwa miradi mbali mbali ya maendeleo kupitia fedha za mifuko ya maendeleo ya Jimbo hilo bado kupanahitajika juhudi za ziara za kutatua kero za wananchi katika sekta za Afya,Maji Safi na Salama pamoja na miondombinu ya barabara za ndani.
Amesema lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi inayotekelezwa na viongozi hao kama thamani ya fedha zinazotumika zinaendana na miradi inayotekelezwa.
Amewambia viongozi hao kuwa wahakikishe miradi wanayoitekeleza inasaidie jamii husika badala ya watu wachache.
Aidha amewasihi Wananchi wa Jimbo hilo kuithamini na kuitunza miradi mbali inayotekelezwa kupitia Ilani ya CCM ili iwanufaishe vizazi vya sasa na vijavyo.
"Utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya Jimbo la Kiembe Samaki unafanuyika lakini bado sijaridhika kwa baadhi ya maeneo hivyo wahusika wanatakiwa kuongeza kasi kubwa katika kutatua kero za wananchi.",amesema Mwenyekiti huyo Mohamed.
Naye Diwani wa Wadi ya Mbweni Ndugu Maabadi Ali Maulid amesema katika kutatua kero za wananchi wamejipanga kutekeleza miradi mitatu ikiwemo kujenga minara mitatu mirefu katika visima vya maji safi na salama,kumalizia kuezeka bweni Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki pamoja na matengenezo ya Barabara za ndani kwa kushirikiana na Serikali Kuu.
Naye Afisa Mipango Manispaa ya Magharib 'B' Ndugu Saumu Daniel Yussuf akizungumza katika Kituo cha Afya cha Kiembe Samaki amesema wanaendelea kuimarisha huduma za Afya katika Vituo mbali mbali licha ya kukabiliwa na changamoto za uchakavu wa majengo waliokabidhiwa katika mfumo wa ugatuzi.
Jumatatu, 22 Aprili 2019
DK.MABODI-ASEMA CCM IMEJIZATITI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI NA KUSIMAMIA DEMOKRASIA.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Abdulla
Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema Chama hicho kimejizatiti kutatua changamoto za Wananchi pamoja na kusimamia Demokrasia kwa kukemea vitendo viovu vinavyohatarisha
Amani na Utulivu wa Nchi.
Kauli hiyo ameitoa katika ziara yake ya kukagua Uhai wa
Chama na Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo la Makunduchi Wilaya ya
Kusini Unguja, amesema vipaumbele vya CCM ni kutekeleza kwa kasi ahadi
zilizotolewa na Taasisi hiyo kwa wananchi kupitia Uchaguzi Mkuu uliopita.
Amesema Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kuaminiwa,kupendwa na
kuthaminiwa na Mamilioni ya Watanzania kutokana na usimamizi mzuri wa
utekelezaji wa Sera zake, kwa kutatua changamoto za kijamii kwa wakati mwafaka.
Aidha amesema katika kusimamia dhana ya Demokrasia CCM
haitosita kukemea vitendo viovu vinavyoashiria kuvunja Sheria za Nchi, hasa
vinavyotekelezwa na baadhi ya Vyama vya upinzani.
“Tumekubali kuingia katika mfumo wa Vyama vingi ili
tushindane kwa Sera na sio kushindana kwa vituko na vurugu ni muhimu kila
mwanasiasa kujitathimini juu ya mwenendo wake kwa jamii anayoiongoza.”, ameeleza Dk.Mabodi.
Amesema katika zama za CCM mpya imekuwa imekuwa ni kimbilio
la wananchi wanaoamini katika siasa za maendeleo ambao wametelekezwa na Vyama
vyao na kupokelewa vizuri ndani ya CCM ili
wanufaike na Demokrasia iliyotukuka.
Amewataka Viongozi na Watendaji wa CCM kutowawekea vikwazo
Wananchi wanaotaka kujiunga na Chama na
badala yake wapewe fursa hiyo bila masharti magumu sambamba na kuwasomesha miongozo
na itikadi za kitaasisi.
Amewaagiza Wabunge,Wawakilishi na Madiwani kufanya mikutano
katika maeneo yao ya kuwaeleza Wananchi mafanikio yaliyofikiwa katika
utekelezaji wa Ilani ili wananchi hao wawe Mabalozi wa kufikisha taarifa hizo
kwa jamii.
Amewambia wananchi kuwa CCM imesimamia kwa ufanisi miradi
ya maendeleo ukiwemo wa TASAF ambao upo katika Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020,
ambao umewaondosha wananchi katika wimbi la umasikini na kuwa na kipato cha
kati.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa mbali mbali vikiwemo
Runinga (Television) pamoja na Fedha kwa vikundi 11 vya Saccos ya Shehia ya
Mzuri katika Maskani ya CCM ya Kisonge Makunduchi Dk.Mabodi amesisitiza kuwa
uhai wa Taasisi hiyo ya kisiasa unaanza kuimarishwa kuanzia ngazi ya mashina.
Naye Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe.Haroun Ali
Suleiman amesema tayari Ilani ya CCM ndani ya Jimbo hilo imetekelezwa kwa
asilimia 90, na kwa sasa wanaendelea kutatua baadhi ya changamoto ili
kuzimaliza kabla ya 2020.
Mhe.Haroun amesema kwa kushirikiana na Kamati ya Siasa ya
Jimbo hilo wamefanya ziara katika Shehia 13 za Jimbo kwa kuratibu
changamoto zinazowakabili wananchi na nyingi zimetatuliwa sambamba na kueleza
fursa na miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ameir Haji Timbe ameeleza kuwa maendeleo yaliyopatikana katika Jimbo hilo yametokana na ushirikiano mkubwa
uliopo baina ya viongozi na wananchi.
Akizungumza Mwenyekiti wa Maskani ya CCM ya Kisonge iliyopo
Makunduchi Abdallah Hassan Haji amesema wanaendelea kuvuna wanachama wapya
kutoka vyama vya upinzani huku wakijipanga kufuta masalia ya upinzania ndani ya
Jimbo hilo.
Naye Mwenyekiti wa Maskani ya CCM ya Hapa Kazi Tu Yussuf
Abeid Haji, akizungumza katika uzinduzi wa Maskani hiyo amefafanua kuwa eneo la maskani
yao litatumika kuwa chachu ya kujenga umoja,mshikamano pamoja na kuwa kituo
mbadala cha kubuni miradi mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya Wana CCM.
MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZNZ DK.ABDULLA JUMA MABODI KATIKA JIMBO LA MAKUNDUCHI UNGUJA.
MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Abdulaziz Haji akizungumza katika ziara hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi katika Jimbo la Makunduchi. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akikabidhiwa zawadi ya Madafu na Wananchi wa Kijiji cha Kibuteni Makunduchi. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla
Mabodi akikagua ukarabati wa ujenzi katika Ofisi ya CCM Jimbo la Makunduchi. |
WAJUMBE wa Kamati ya Siasa ya Jimbo la Makunduchi wakizungumzia mafanikio mbali mbali yaliyofikiwa katika masuala mbali mbali ya utekelezaji wa Ilani ya CCM Jimboni humo. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla
Mabodi akimkabidhi fedha kiongozi wa Kikundi cha Saccos ya Shehia ya Mzuri iliyopo Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla
Mabodi akikabidhi Runinga(Television) kwa Uongozi wa Maskani ya CCM ya Kisonge iliyopo katika Jimbo la Makunduchi. |
MWAKILISHI wa Jimbo la Makunduchi Mhe.Haroun Ali Suleiman akielezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya Jimbo hilo. |
MBUNGE wa Jimbo la Makunduchi Mhe. Ameir Haji Timbe akizungumza na Wananchi wa Jiimbo la Makunduchi katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Mabodi. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla
Mabodi akiwa amebeba ndoo yenye udongo katika ujenzi wa Tawi la CCM Miwaleni
Jimbo la Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja. |
MKUU wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrisa Mustafa Kitwana (aliyebeba kifaa cha kubebea udongo wa kifusi wa pili kushoto) akishiriki ujenzi wa Taifa katika Tawi la CCM Miwaleni Makunduchi. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla
Mabodi akizindua Maskani ya CCM ya Hapa Kazi Tu iliyopo Mtende Mndo Makunduchi. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akikagua ujenzi wa Tawi la CCM Mtende Mndo Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla
Mabodi akikabidhi Runinga kwa Uongozi wa Maskani ya CCM ya Mtende Mndo Makunduchi. |
Jumamosi, 20 Aprili 2019
MATUKIO KATIKA PICHA HAFLA YA JUMUIYA YA MAENDELEO YA VIJANA YA CCM KUTOA VIFAA VYA UJENZI NA SARE ZA WANAFUNZI SKULI YA KIDAGONI KASKAZINI 'A'
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akipokelewa na Wanafunzi wa Shule ya maandalizi,msingi na Kati ya Kidagoni Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akikagua Kituo hicho. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizungumza na Uongozi wa Kamati ya Maendeleo ya Skuli ya Kidagoni. |
VIJANA mbali mbali wa UVCCM wakishusha mabembea mbali mbali yaliyotelewa na Jumuiya ya Vijana wapenda maendeleo kwa ajili ya wanafunzi wa maandalizi wa Skuli hiyo. |
WAJUMBE mbali mbali wa Jumuiya ya Vijana wapenda maendeleo wakiimba wimbo wa mashujaa mara baada ya kuwasili skulini hapo. |
WANAFUNZI wa Skuli ya Kidagoni wakisoma utenzi |
VIJANA wa kundi Maalum la Hamasa kutoka CCM Afisi Kuu wakiwa katika hafla hiyo. |
Mwalimu wa Skuli ya Kidagoni Neema Othman Khamis akisoma risala ya Skuli hiyo. |
VIJANA wa kikundi cha sarakasi cha UVCCM Wilaya ya Kaskazini 'A' wakionyesha uwezo wao katika hafla hiyo. |
|
MJUMBE wa Jumuiya ya Vijana wapenda Maendeleo akisoma risala ya Jumuiya hiyo. |
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana wapenda Maendeleo Mwinyi Ahmed Mwinyi akizungumzia lengo la kutoa vifaa vya ujenzi pamoja na sale,viatu,mikoba na mabembea kwa wanafunzi wa Jumuiya hiyo. |
MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Kaskazini 'A' akitoa salamu za CCM katika Wilaya hiyo. |
KATIBU wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mulla Othman Zubeir akitoa salamu za CCM kwa niaba ya Mkoa. |
MWAKILISHI wa Jimbo la Nungwi Mhe. Ame Haji Ali akizungumzia utekelezaji wa Ilani katika Jimbo hilo mbele ya mgeni rasmi katika hafla hiyo. |
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana wapenda Maendeleo Mwinyi Ahmed Mwinyi akikabidhi Sale za wanafunzi ambavyo ni moja vitu mbali mbali vilivyotolewa na Jumuiya yake kwa Skuli ya Kidagoni. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwahutubia wananchi wa Kidagoni katika hafla hiyo. |
PICHA ya pamoja ya viongozi wa Jumuiya, Viongozi wa Skuli ya Kidagoni pamoja na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwa na Ujumbe wa Viongozi mbali mbali wa CCM na Jumuiya zake kutoka Kibiti na Rufiji.(PICHA NA IS-HAKA OMAR-AFISI KUU YA CCM ZNZ). |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)