Jumatatu, 25 Februari 2019

WANANCHI WA NGOMENI PEMBA WAMPONGEZA DK.SHEIN, WAMUOMBA ATATUE CHANGAMOTO YA MAWASILIANO.

BAADHI ya Wananchi wa Kijiji cha Ngomeni wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Afya Ngomeni Wilaya ya Chake Chake Pemba, kilichozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 

WANANCHI wa Kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Chake Chake  Pemba wamempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa juhudi zake za kuimarisha huduma za msingi zilizofungua fursa za kiuchumi katika Kijiji hicho na vijiji jirani.

Wakizungumza kwa wakati tofauti mara baada ya kumaliza hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Afya cha Ngomeni wameeleza kuwa wamefurahishwa na kasi ya Dk.Shein katika kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati mwafaka.

Wameeleza kuwa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na SMZ katika Kijiji hicho wataituza na kuithamini ili iwahudumie wananchi mbali mbali wa Kijiji hicho.

Akizungumza mkaazi wa Kijiji hicho Bi.Mariam Juma Fakih, ameeleza kuwa Akina Mama wajawazito walikuwa wakijifungulia njiani na wengine kupoteza Maisha kutokana na ukosefu wa huduma za Afya katika maeneo ya karibu ambapo kwa sasa ameeleza kuwa changamoto hiyo tayari imetatuliwa na SMZ kwa kujenga klituo cha Afya cha Kisasa.

Naye Suleiman Haji Bakari Mkaazi wa Kijiji hicho, amesema wananchi wa maeneo hayo wanaishukuru serikali kwa kuimarisha huduma ya barabara kwani inawasaidia wakulima wa mazao mbali mbali hasa zao la Karafuu.

Pamoja na hayo Suleiman amemuomba Dk.Shein kuwasaidia wananchi hao kupata mnara wa mtandao wa simu kutokana na wananchi kukosa mawasiliano ya simu kwa sababu eneo hilo lipo bondeni jambo linalokwamisha baadhi ya harakati za kiuchumi.

DK.SHEIN ATOA AGIZO KWA WIZARA YA AFYA, AZINDUA BARABARA YA KUYUNI -NGOMENI (3.2KM) NA KITUO CHA AFYA NGOMENI PEMBA.


RAIS wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiweka Jiwe la Msingi na kukizindua  Kituo cha Afya cha Ngomeni katika Wilaya ya Chake Chake Pemba.

BAADHI ya Wananchi wakiwa katika uzinduzi wa kituo cha Afya Ngomeni huko Wilaya ya Chake Chake Pemba.

BAADHI ya Viongozi mbali mbali wa Serikali na CCM wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Barabara na KItuo cha Afya cha Ngomeni Wilaya ya Chake Chake Pemba.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ngomeni mara baada ya kuzindua Barabara na Kkituo cha Afya katika Kijiji hicho.

WAZIRI wa Nchi(OR) Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheir akizungumza katika hafla hiyo juu ya dhana ya Ugatuzi ambapo Serikali Kuu imeshusha baadhi ya madara kwa Serikali za Mitaa ili wananchi waamue wenyewe vipaumbele vyao katika masuala ya Huduma za Kijamii.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi(kushoto) akifuatilia matukio mbali mbali katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kituo cha afya.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dk Sira Ubwa Mamboya akitoa maelezo juu ya mikakati ya SMZ itakavyoendelea  kujenga barabara za Kisasa katika maeneo mbali mbali ya Pemba.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ameiagiza Wizara ya Afya Zanzibar kutoa huduma bora za Afya sambamba na kuwashauri wananchi juu ya masuala mbali mbali ya Afya huko katika Kituo cha Afya kilichopo  Kijiji cha Ngomeni, Wilaya ya Chake Chake Pemba.


Dk.Shein ametoa agizo hilo mara baada ya kuweka jiwe la msingi na kukizindua rasmi Kituo cha Afya katika Kijiji hicho, amesema kuwa kituo hicho lazima kitoe huduma bora na kuwaondoshea wananchi changamoto za ukosefu wa huduma bora za afya ambazo awali wananchi wa Kijiji hicho walizifuata maeneo ya mbali.


Amesema lazima Wizara husika ihakikishe inapeleka Watendaji na Vifaa tiba vya kutosha ili kumaliza changamoto za ukosefu wa huduma hizo muhimu za Afya kwa wananchi hao.


Amesema kuwa baada ya miezi miwili ataenda kukagua Kituo hicho kwa lengo la kujiridhisha juu ya maagizo yake yamefanyiwa kazi kwa kiasi gani.


Ameeleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitomvumilia Watendaji na Viongozi wanaokwamisha maendeleo ya nchi kwa makusudi kwani serikali inatumia gharama kubwa kuwasogezea wananchi huduma za msingi lakini wapo baadhi ya watendaji wanaokwamisha juhudi hizo kwa makusudi.


Katika maelezo yake Dk. Shein, ameeleza kuwa uamuzi wa Serikali kujenga  Barabara ya Kuyuni hadi Ngomeni pamoja na Ujenzi wa Kituo cha Afya   Ngomeni,  umekuja kufuatia eneo hilo kuzalisha kiwango kikubwa cha zao la karafuu.


Dk. Shein amesema ufunguzi wa  barabara ya Kuyuni hadi Ngomeni yenye urefu wa kilomoita 3.2, iliojengwa kwa kiwango cha Lami  pamoja na kituo cha Afya , ujenzi uliofanikishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni miongoni mwa fursa za maendeleo katika Kijiji hicho na vijiji jirani.


Amesema juhudi za ujenzi wa barabara na kituo hicho cha Afya, utaendana na ujenzi wa barabara ya Mgelema hadi Wambaa, kazi itakayotekelezwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.


Amewaeleza wananchi hao, kuwa maendeleeo makubwa yaliopatikana katika eneo hilo yanatokana na uzalishaji mkubwa wa karafuu, hivyo akawapongeza wananchi wa maeneo hayo kwa kuuza karafuu zao ZSTC.
Dk. Shein amewataka  wananchi kukaa pamoja na Wawakilishi wao ili waweze kusaidia upatikanaji wa gari la wagonjwa (ambulance) ili kusaidia usafirishaji wa wagonjwa wanaohitaji huduma za ziada  katia Hospitali kuu.


Katika hatua nyengine, Dk. Shein amemuagiza  Katibu Mkuu Wizara Afya kujipanga na watendaji wake na kuainisha gharama za ujenzi wa kituo cha Afya Ngomeni, baada ya kushindwa kubainisha katika taarifa yake.


Dk.Shein ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amesema mafanikio yanayopatikana katika Nyanja mbali mbali Visiwani Pemba yatatokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.


Amesema kabla ya kupelekwa huduma za msingi katika Kijiji cha Ngomeni wananchi wa maeneo hayo waliishi kwa changamoto mbali mbali kutokana na kukosa Barabara, Umeme, Maji Safi na Salama, Kituo cha Afya mambo ambayo kwa sasa tayari yametekelezwa kwa ufanisi mkubwa.


Katika hatua nyingine Dk.Shein mara baada ya uzinduzi huo amepokea Taarifa za Serikali na Chama Cha Mapinduzi kupitia Majumuisho ya ziara yake katika Wilaya hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa ZSTC Makonyo Pemba, ikiwa ni hitimisho la ziara hiyo kwa Unguja na Pemba.


Jumapili, 24 Februari 2019

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA DK.SHEIN WILAYA YA MICHEWENI AKIKAGUA MACHIMBO YA MCHANGA HUKO SHUMBA VIAMBONI PEMBA.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua eneo jipya la Shumba Viamboni  linalochimbwa Mchanga katika Wilaya ya Micheweni Pemba katika mwendelezo ya ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020  katika Wilaya Mbali Mbali za Unguja na Pemba.

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe.Mariam  Juma Mabodi(aliyevaa mtandio wa rangi nyekundu),akitoa maelezo juu ya uchimbaji wa mchanga katika eneo hilo la Shumba viamboni  katika Wilaya ya Micheweni Pemba.

ENEO Mmaalum la Shumba viamboni linalochimbwa mchanga kwa ajili ya matumizi mbali mbali ya ujenzi na n.k huko Wilaya ya Micheweni Pemba.

VIONGOZI mbali mbali wa SMZ na CCM wakiwa katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara yake ya kukagua machimbo ya Mchanga huko Shumba Viamboni.

VIONGOZI mbali mbali wa CCM wakiwa katika ziara ya Dk.Shein huko katika machimbo ya mchanga ya Shumba Viamboni Wilaya ya Micheweni Pemba.

VIONGOZI mbali mbali wa CCM wakiwa katika ziara ya Dk.Shein huko katika machimbo ya mchanga ya Shumba Viamboni Wilaya ya Micheweni Pemba.Jumamosi, 23 Februari 2019

MATUKIO KATIKA PICHA MAJUMUISHO YA ZIARA YA DK.SHEIN WILAYA YA WETE PEMBA-23/02/2019.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wana CCM pamoja na Viongozi katika Majumuisho ya Wilaya ya Wete Pembe.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akitoa salamu za CCM katika Majumuisho ya ziara ya Rais Dk.Shein katika Wilaya ya Wete Pemba.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Ndugu Haji Omar Kheir akizungumza katika majumuisho hayo.

VIONGOZI na Wanachama wa CCM wakiwa katika majumuisho ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein yaliyofanyika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba.

MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Wete Pemba ndugu Kombo Hamad Yussuf akimkabidhi zawadi kwa niaba ya Wazee wa Wilaya hiyo Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika majumuisho ya ziara yake Wilaya ya Wete Pemba.

BAADHI  ya Viongozi  wa CCM wakiwemo Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makatibu wa Kamati Maalum a NEC Taifa wakiwa katika hafla ya Majumuisho ya ziara ya Rais wa Zanzibar Dk.Shein katika Wilaya ya Wete.

MKUU wa Wilaya ya Wete  Abeid Juma Ali akimkabidhi zawadi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika majumuisho ya ziara ndani ya Wilaya ya Wete Pemba.

MKUU wa Wilaya ya Wete Mhe.Abeid Juma Ali akiwasilisha taarifa ya Wilaya ya Wete mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

BAADHI ya Wana CCM wakifuatilia kwa makini matukio mbali mbali yanayofanyika katika majumuisho ya Wilaya ya Wete.

KATIBU wa CCM Wilaya ya Wete ndugu Salum Khamis Haji akiwasilisha taarifa ya Chama Cha Mapinduzi katika Wilaya hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.

WAZEE wa CCM Pemba wakiwa katika majumuisho hayo ya Wilaya ya Wete.

BAADHI ya Watumishi wa Wilaya ya Wete na wanachama wa CCM wakiwa katika Majumuisho ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein huko Wilaya ya Wete Pemba.

PICHA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO AFISI KUU YA CCM ZANZIBAR.

MATUKIO KATIKA PICHA UZINDUZI WA SKULI YA MSINGI YA BOPWE WILAYA YA WETE-23/03/2019.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua Jengo la madarasa ya Shule ya Msingi ya Bopwe huko Wilaya ya Wete Pemba.

KATIBU Mkuu Wizara ya Nchi (OR), Serikali za Mitaa, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Radhia Haroub Juma akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa Jengo hilo la Shule ya Bopwe kupitia mfumo wa Ugatuzi Zanzibar.
WAZIRI wa NChi Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheir akizungumza katika hafla hiyo,

VIONGOZI mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika uzinduzi wa shule ya msingi bopwe.

VIONGOZI wa Meza Kuu wakiimba wimbo wa Sisi sote tumegomboka katika hafla ya uzinduzi wa Shule ya Msingi ya Bopwe Wilaya ya Wete Pemba.

BAADHI ya Mawaziri na Viongozi mbali mbali wa SMZ wakiimba wimbo maalum wa Mashujaa wa SISI SOTE TUMEKOMBOKA.

VIJANA wa Kikundi cha Hamasa wa Wilaya ya Wete wakiimba nyimbo mbali mbali za kuhamasisha katika hafla hiyo.

BAADHI ya Wanafunzi wa Wananchi Wilaya ya Wete wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya Bopwe Pemba.DK.SHEIN: AZINDUA JENGO LENYE MADARASA MANNE YA KISASA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA MCHANGA MDOGO WETE PEMBA-23/03/2029.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baaza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizindua Jengo la Madarasa Manne ya Shule ya Sekondari Mchanga Mdgo iliyopo katika Wilaya ya Wete Pemba.

JENGO la Madarasa Manne ya Shule ya Sekondari ya Mchanga mdogo iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibr Dk.Abdulla Juma Mabodi pamoja na wananchi na Wana CCM wakicheza Dufu katika hafla wa uzinduzi wa jingo la madarasa manne katika Shule ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba.

KATIBU wa Kamati  Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar  Bi.Catherine Peter Nao akizungumza na wanafunzi wa shule ys sekondari mchanga mdogo.

KATIBU wa Taalum Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Ndugu Madina Mjaka akitoa taarifa ya kitaalamu katika hafla hiyo.

BAADHI ya Viongozi na makada wa Chama Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika hafla hiyO.

VINGOZI na Wananchi wa SMZ wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa shule ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete.

BAADHI ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mchanga Mdogo wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la shule hiyo lete madarasa manane.

Ijumaa, 22 Februari 2019

WANANCHI WASEMA DK.SHEIN NI SHUJAA WA MAENDELEO


BARABARA ya Mkanyageni-Kangani  Wilaya ya Mkoani Pemba.

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

BAADHI ya Wananchi wa Wilaya ya Mkoani Pemba wamepongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha miundo mbinu ya Barabara ndani ya Wilaya hiyo.

Wameeleza kuwa Serikali ya awamu ya saba chini ya uongozi wa Dk.Shein, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutatua matatizo sugu yaliyowathiri wananchi wa wilaya hiyo kwa miaka mingi kabla na baada ya  Mapinduzi ya mwaka 1964.

Wakizungumza kwa wakati tofauti baadhi ya wananchi hao, mara baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuweka Jiwe la Msingi katika Barabara ya Mkanyageni -Kangani (KM5), wamesema barabara hiyo itakuwa ni mkombozi kwa wananchi wa wilaya hiyo na maeneo jirani.

Mkaazi wa Kijiji cha Mkanyageni Juma Faki Hamad(45), amesema barabara ni moja ya kichocheo cha maendeleo kwa wananchi waoishi vijijini kwani wanapata kusafirisha mazao na bidhaa mbali mbali kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Naye Mkaazi wa Kijiji cha Mkanyageni Fatma Masoud Kombo( 50) amempongeza Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kwa juhudi zake za kutengeneza barabara hiyo itakayokuwa mkombozi kwa Akina mama wajawazito kufika kwa wakati katika Vituo vya Afya.

Katika maelezo yake Bi.Fatma amemtaja Dk.Shein kuwa ni shujaa wa maendeleo anayeasisi maendeleo ya kuvinufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Ameeleza kwamba Dk.Shein amekuwa ni kiongozi muadilifu anayejali maisha ya wananchi wa kipato cha chini kwa sasa amewafanya wamekuwa na hadhi kutokana na kuimarika kwa huduma mbali mbali za kijamii na kiuchumi.

Naye Zuwena Hiji Kombo(65), amesema mtu yeyote anashindwa kushukru na kuthamini huduma za kimaendeleo zinazotekelezwa na Serikali, mtu huyo atakuwa hana uzalendo na hastahiki kuishi katika jamii ya watu wanaopenda maendeleo ya Zanzibar.

Said Nassor Mjaja(39), amewataka wananchi wa Wilaya ya Mkoani kuendeleza utamaduni wa ustarabu na kuachana na siasa zilizopitwa na wakati za kuharibu miundombinu mbali mbali inayotekelezwa na Serikali kwani wanaonufaika ni wananchi wote.

VISIWA VIDOGO VIDOGO PEMBA NA UNGUJA KUPATA VIVUKO VYA KISASA.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Mkoani na Chama Cha Mapinduzi katika Majumuisho ya ziara yake huko Skuli ya Sekondari ya Mohamed Juma Pindua.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akitoa salamu za CCM katika majumuisho hayo.


KATIBU wa CCM Wilaya ya Mkoani Mohamed Ali Abdalla akisoma taarifa ya CCM katika majumuisho hayo.

BAADHI ya Viongozi mbali mbali wa CCM wakiwa katika majumuisho hayo.

BAADHI ya Maziri wa SMZ wakiwa katika majumuisho ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Wilaya ya Mkoani Pemba.

WAZEE wa Chama Cha Mapinduzi Pemba wakiwa katika majumuisho.


 NA IS-HAKA OMAR, PEMBA.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzbar Dk.Ali Mohamed Shein,a mesema serikali inaendelea na juhudi za kutafuta vivuko vya kisasa vyenye uwezo wa kuwavusha kwa usalama wananchi wanaoishi katika visiwa vidogo vidogo Pemba na Unguja.

Amesema mipango hiyo inaendelea kwa umakini Zaidi wa kupata vivuko hivyo vilivyokuwa katika viwango vya kimataifa ili wananchi wa visiwa vyote wawe na uhakika wa usafiri wa baharini.

Ameeleza kuwa mkakati huo unaenda sambamba na uimarishaji wa ulinzi wa maeneo yote ya Bahari, kikosi  cha KMKM kwa lengo la kudhibiti uhalifu na magendo katika maeneo ya bahari.

Dk.Shein ameeleza kwamba fursa hizo zinatokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, inayoangazia kumaliza changamoto zote zinazowakabili wananchi ili kujenga taifa imara lililoendelea kiuchumi na kijamii.

Amefafanua kwamba CCM imekuwa ni taasisi yenye viongozi waadilifu wanaoahidi na wakatekeleza kwa vitendo masuala mbali mbali yayosaidia jamii bila ya kuwabagua watu kidini na kikabila.

Ameeleza kwamba kabla ya mwaka 2020 Zanzibar itakuwa ni miongoni mwa Nchi ya Visiwa yenye maendeleo ya kupigiwa mfano katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo.

Amewambia baadhi ya Viongozi na watendaji wa Serikali kuwa asiyeweza kutekeleza Ilani ya CCM huyo atakuwa hatoshi kuwa kiongozi hivyo ni bora akajiondoa mapema katika nafasi anayoitumikia.

Ameeleza kwamba kwa sasa Chama kinahitaji viongozi wabunifu na wachapakazi ili kwenda sambamba na Sera imara za kukuza uchumi wa Nchi.
Alisoma taarifa ya utekelezaji wa majukumu mbali mbali ya CCM katika Wilaya hiyo Katibu wa CCM Wilaya ya Mkoani Mohamed Ali Abdallah, amesema kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM, umekuwa ni kivutio kikubwa cha wanachama wengi wa upinzani kisiwani Pemba wakiwemo vigogo kujiunga na CCM.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe,Issa Juma Ali,akisoma taarifa ya Wilaya hiyo ameeleza kuwa Serikali imetekeleza kwa ufanisi masuala mbali mbali yakiwemo kuimarisha Sekta za Afya, Elimu, Kilimo,Uvuvi, Mazingira na miundombinu ya Majini na Nchi Kavu.

Akitoa salamu za CCM Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dk.Abdulla Juma Mabodi ameeleza Chama kinaridhishwa na kasi ya kiutendaji kwa upande wa Serikali na Chama kwa ujumla.

Amesema kazi iliyobaki kwa sasa ni kila mwanachama kujipanga vizuri katika kuhakikisha CCM inashinda katika majimbo yote yaliyomo katika Wilaya hiyo.