Vijana
waliojitokeza kwenye shughuli ya usafi wakimsikiliza Mwenyekiti wa mkoa baada
ya kumaliza kazi. |
Wana
CCM wakiendelea kusafisha maeneo ya jengo la CCM huko Amani mjini Zanzibar
jana.
Picha
na Martin Kabemba.
|
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mjini Zanzibar kimewataka wanachama wake kujitokeza kwa wingi katika shamrashamra za kuzaliwa kwa CCM ili kuunga mkono mafanikio yaliyopatikana katika nyanja za kisiasa,kiuchumi na kimaendeleo.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Ndugu Talib Ali Talib katika ufunguzi wa shamrashamra za wiki ya sherehe za kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM ndani ya Mkoa huo.
Talib amesema miaka 42 inathihirisha kuwa Taasisi hiyo ya kisiasa imeimarika kisera,kiungozi na kisiasa hatua inayotakiwa kuthaminiwa na jamii.
Amewambia wanachama wa CCM hasa vijana kuwa bado wana nafasi ya kujivunia uwepo wao ndani ya CCM kwani ni taasisi inayokwenda na wakati katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Katika kuadhimisha sherehe hizo Mwenyekiti huyo Talib amekabidhi tanki la maji la lita 5000 kwa kikundi cha ujasiriamali cha 'umasikini si kilema' kilichopo katika Wilaya ya Amani kichama ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi aliyoitoa miezi kadhaa iliyopita katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani katika Manispaa ya Wilaya ya Mjini.
Mara baada ya kukabidhi tenki hilo amewasihi akina mama wa kikundi hicho kuwahamasisha akina mama wenzako kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili wajiajiri na kuondokana na utegemezi.
Nao baadhi ya wajasiriamali wa kikundi hicho wameishukuru CCM kwa ungwana wake wa kutekeleza ahadi kwa wakati na wakaongeza kuwa kifaa hicho watakutumia kwa malengo yaliyokusudia.
Wameeleza kwamba kwa muda mrefu walikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa sehemu maalum ya kuhifadhi maji ya kumwagilia mboga mboga naazao mengine wanayolima katika kikundi hicho.
Akitoa shukrani Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ndugu Sufiani khamis amewapongeza wanachama wa CCM waliojitokeza katika zoezi hilo la usafi na kueleza kuwa suala la umoja na mshikamano ndani ya taasisi hiyo ni wajibu wa msingi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni