Ijumaa, 31 Agosti 2018
Alhamisi, 30 Agosti 2018
DK.SHEIN AMEFANYA ZIARA KATIKA TAASISI ZA UTAFITI ZANZIBAR.
BAADHI ya viongozi na wanachama wa CCM walioudhuria katika ziara hiyo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. |
WANANCHI walioudhuria katika ziara hiyo ya Dk.Ali Mohamed Shein.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amesema serikali itaimarisha taasisi zote za utafiti nchini ziweze kufanya utafti wenye hadhi ya kimataifa. Kauli hiyo ameitoa leo wakati akifanya ziara katika taasisi mbali za utafiti ambazo ni taasisi ya Utafti wa Mifugo Langoni Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A" pamoja na Taasisi ya Utafti wa masuala ya Afya iliyopo Wilaya ya Kati Zanzibar. Amesema Taasisi hizo ni nyenzo za kuharakisha maendeleo ya Zanzibar kwani katika ulimwengu wa sasa kila jambo lenye kuleta maendeleo ama madhara katika jamii lazima lifanyiwe Utafti wa kitaalamu. Dk.Shein Akizungumza mara baada ya kukagua eneo litakalojengwa Hospitali kuu ya kisasa Zanzibar, ambayo itakuwa na taasisi ya utafti ya Afya itakayotoa mafunzo kwa wataalamu wa afya ili waweze kuwa na ujuzi mkubwa wa kutoa huduma za afya kitaalamu. Amesema ujenzi wa hospitali hiyo utakapokamilika itawasaidia wananchi wa maeneo mbali mbali ya Zanzibar na kupunguza msongamano wa wananchi kwenda kufuata huduma za Afya katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja. Dk.Shein ameongoza kuwa hatua hizo ni miongoni mwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa lengo la kutatua changamoto za wananchi na kuwaletea maendeleo. Ameeleza kwamba CCM inaendeleza utamaduni wake wa asili wa kutekeleza kwa vitendo miradi mbali mbali ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wote. "Hospitali hii itakapokamilika itakuwa na uwezo mkubwa wa vifaa tiba, wataalamu na miundombinu ya kisasa ya masuala ya Afya hivyo wananchi mnaoishi karibu na eneo hili muunge mkono juhudi za serikali. Pia vijana wetu wenye utaalamu wa masuala ya Afya watakuja hapa kupata mafunzo na kufanya utafti wa tiba za maradhi mbali mbali na kuwatibu wananchi.",amesema Dk.Shein. Akikagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Taasisi ya utafti wa Mifugo huko Langoni Unguja, Dk.Shein amesema taasisi hiyo itasaidia kufanya utafti wa Mifugo hapa nchini na kupunguza gharama za kwenda Tanzania bara na maeneo mengine kufanya utafti huo. Mapema Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafti wa Mifugo Zanzibar,Dk.Kassim Gharib Juma amesema taasisi hiyo tayari imefanya utafti mbali mbali wa mifugo ikiwemo Ng'ombe,Mbuzi na kuku ulioweza kuleta tija kwa kubaini maradhi na njia za kitaalamu za kukabiliana na changamoto hizo pamoja na ufugaji bora wa Mifugo hiyo. Pia alieleza kwamba wamefanya utafti wa kutengeneza chakula cha wanayama kupitia zao la mwani, ambao utasaidia kuzalisha chakula bora cha mifugo hapa nchini. Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Halma Maulid Salum amesema ujenzi wa majengo mbali mbali ya Taasisi ya utafti wa afya pamoja na Hospitali katika eneo la Binguni Wilaya ya Kati Unguja hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi cha shilingi bilioni nne. Ameeleza kuwa Wizara ya Afya itasimamia kikamilifu ujenzi wa majengo hayo ili taasisi hiyo itowe huduma bora za Afya kwa jamii. Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla (Mabodi), amempongeza Dk.Shein kwa mfumo mzuri wa uongozi shirikishi baina ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amesema mambo mema yanayotekelezwa na serikali ya awamu ya Saba Zanzibar chini ya uongozi wa Dk.Shein inafuata nyayo za utawala wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar hayati Abeid Aman Karume kwa kutekeleza miradi ya maendeleo inayodumu kwa muda mrefu kwa maslahi ya jamii. Amesema kazi kubwa inayofanywa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuimarisha huduma muhimu za kijamii ni miongoni mwa kibali halali cha kisiasa cha kuiletea ushindi CCM katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. |
Jumamosi, 25 Agosti 2018
KHEIR JAMES: ATAKA ELIMU ZA VIJANA ZISAIDIE JAMII ILIYOWAZUNGUKA.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar ambaye pia ni mlezi wa UVCCM Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizungumza katika hafla hiyo ya kuwapongeza wanafunzi wa kidatu cha sita mwaka 2018 Zanzibar. |
Jumanne, 21 Agosti 2018
Jumatatu, 20 Agosti 2018
DK.BASHIRU AITAJA MIKAKATI YA KUKUZA UCHUMI WA CCM
VINGOZI mbalimbali wa CCM na UVCCM wakiwa katika uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili ya kumuaga Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally ambaye amehitimisha ziara yake kisiwani Pemba. |
NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Shaka Hamdu Shaka(kulia) akiagana na Katibu mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru aliyekuwa kisiwani Pemba kwa ajili ya ziara. |
Katibu mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita katika uwanja wa ndege wa Pemba. |
Jumapili, 19 Agosti 2018
DK.BASHIRU ASEMA CCM INAZIDI KUIMARIKA
NA IS-HAKA, ZANZIBAR.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Dk.Bashiru
Ally amesema CCM inaendelea kuimarika na hakuna Chama chochote cha kisiasa
nchini kinachoweza kushindana na taasisi hiyo katika uringo wa siasa za ushindani wa sera
za maendeleo kwa wananchi.
Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba
katika mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha ambapo amezungumza na
wanachama mbalimbali katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Fidel Castro Wilaya
ya Chake Chake Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Amesema kutokana na uimara huo hakuna chama kingine mbadala
wa Chama Cha Mapinduzi kinachoweza kushuka kwa wananchi nyumba kwa nyumba na kutatua changamoto za wananchi.
Dk.Bashiru amewahakikishia wanachama na viuongozi hao kuwa
CCM bado ipo imara na itapata ushindi wa kihistoria mwaka 2020 kwa nchini nzima
kuliko ushindi unaopatikana kwa sasa katika uchaguzi mdogo unaoendelea katika
maeneo mbalimbali nchini.
Ameongeza kwamba sababu za Chama Cha Mapinduzi kushinda kwa kishindo kwa kila uchaguzi huku vyama vya upinzani vikisambaratika na kukosa muelekeo wa uhalali wa kuitumikia jamii.
Kupitia mkutano huo aliwambia wanachama wa vyama vya
upinzania kisiwani Pemba kwamba huu ndio wakati wao wa kujitawala kifikra kwa
kujiunga na CCM kwani Chama Cha CUF hakina tena mvuto kwa jamii kutokana na
tabia ya unafiki na uongo unaofanywa na viongozi wakuu wa CUF.
Dk.Bashiru kupitia mkutano huo alitangaza rasmi kuwa Chama
Cha Mapinduzi kitaendelea kuvunja ngome zote za upinzani kabla ya mwaka 2020, ambapo mamlaka hayo yanatokana na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka
2015/2020.
Kupitia mkutano huo pia Dk.Bashiru aliwapokea wanachama wapya
62 waliotoka chama cha CUF na kujiunga na CCM kisiwani Pemba.
Aliwapongeza wanachama wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa kwa kumuamini kasha kupendekeza ateuliwe kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa
CCM Tanzania, na akaahidi kuwa atatumia nafasi yake kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma
Saadalla (Mabodi), amesema kazi kubwa ya Chama cha mapinduzi kwa zama za sasa ni
kutekeleza kwa vitendo dhana ya CCM mpya na Tanzania mpya kwa maendeleo ya jamii.
Amefafanua kuwa miradi mbali mbali ya maendeleo iliyotekelezwa kwa
ufanisi kisiwani Pemba ikiwemo mfuko wa maendeleo wa TASAF na kuongeza bei ya
zao la karafuu ni kutokana na utekelezaji mzuri wa sera za CCM.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Ndugu Yussuf Ali
Juma amesema ndani ya Mkoa huo wanaendelea na mikakati ya kuhakikisha CCM
inashinda kwa ngazi zote katika uchaguzi Mkuu ujao.
Katika ziara hiyo Dk. Bashiru alifuatana na viongozi mbali wa
Chama na Jumuiya wakiwemo wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, wajumbe wa
halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Makamu Wenyeviti wa Jumuiya pamoja na viongozi
mbali mbali wa Chama na Serikali Zanzibar.
MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA DK.BASHIRU PEMBA.
KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akivishwa sikafu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Pemba akitoka Unguja. |
KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mwl.Kombo Hassan Juma mara baada ya kuwasili Pemba kwa ajili ya kuendelea na ziara yake kisiwani humo. |
KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake Suleiman Sarahan mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili ya ziara ya kujitambulisha. |
KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Tabia Maulid Mwita mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Pemba. |
KATIBU Mkuu wa CCM Dk,Bashiru akiangalia ngoma ya kirumbizi kutoka Mkoa wa kusini Pemba ambayo ni miongoni mwa mapokezi ya kiongozi huyo. |
KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru akipokelewa na vijana wa UVCCM kwa wimbo wa mashujaa katika Uwanja wa Ndege wa Pemba. |
KATIBU Mkuu
wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally na msafara wake wakitembea kwa maandamano ya mapokezi kuelekea ofisi ndogo ya CCM Chake
chake mjini Pemba. |
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Pemba Ali Hamad Khatib akimpokea na kumpa nasaha Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru baada ya kufika katika Ofisi Ndogo ya CCM Pemba. |
KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru akizungumza na Watumishi wa CCM wa Ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar. |
MWANACHAMA mpya kutoka CUF Amina Juma Kassim ambaye ni miongoni mwa wanachama waliohama katika chama hicho na kujiunga na CCM, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally. |
BAADHI ya Wana-CCM wakifuatilia kwa karibu matukio yanayoendelea katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru uliofanyika leo katika Ukumbi wa skuli ya Fidel Castro. |
KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akiwahutubia wanachama na viongozi wa CCM katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro Mkoa wa Kusini Pemba. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro. |
MWENYEKITI
wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndugu Mbwerwa Hamadi Mberwa akimkabidhi
zawadi ya ndizi ya mkono wa Tembo Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally katika ziara ya kujitambulisha kwa
wanachama wa CCM Pemba. |
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndugu Mbwerwa Hamad Mberwa ya ngao ya
mwenge wa uhuru Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru kutoka Mikoa miwili ya
Pemba. |
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Ali Juma akiwakaribisha viongozi mbalimbali katika Mkoa wa Kusini Kichama. |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)