Ijumaa, 17 Agosti 2018

MATUKIO KATIKA PICHA MAPOKEZI MAKUBWA YA KATIBU MKUU WA CCM TANZANIA DK.BASHIRU.


 MSAFARA wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally wakitembea kwa miguu kuelekea Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar .

 WANACHAMA wa CCM waliosimama pembe zoni mwa barabara pamoja na wenye mapikipiki wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Ally.

 KIJANA wa Chipukizi akimvisha kwa ukakamavu  shada la maua maalum aina ya Koja Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza visiwani Zanzibar.

 Katibu Mkuu na viongozi mbali mbali wa CCM na SMZ wakisubiri kupokea maandamano ya wanachama wa CCM.

 Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally, akiwa na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wakipokea maandamano ya vijana na Wana-CCM walioshiriki katika mapokezi hayo.

Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Haji Haidar  viongozi mbali mbali walioshiriki katika mapokezi hayo. 

 KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru akiangalia ngoma ya kibati ambayo ni ngoma ya asili ya Zanzibar.

 Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally  pamoja na viongozi wengine wakiomba dua baada ya kuzuru kaburi la muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hayati Mzee Abeid Aman Karume.

 Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally , akisaini kitabu cha wageni katika Afisi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi.

 Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally , akizungumza na Watumishi wa CCM Zanzibar mara baada ya kupokelewa Kisiwandui (hawapo pichani).

 BAADHI ya Watumishi wa CCM Zanzibar wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally alipokuwa akizungumza katika ukumbi wa Kamati Maalum ya NEC ya CCM Zanzibar.

 Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na wazee wa CCM Zanzibar.
 WASANII wa kizazi kipya Zanzibar wakitoa burudani katika mkutano huo wa mapokezi ya Dk.Bashiru.,



  BAADHI ya waliokuwa wanachama wa CUF na  wamejiunga na CCM wakionyesha kadi za CUF walizokuwa wakizitumia wakati wapo katika chama hicho na wamezikabidhi kwa CCM. 



DK.bashiru akikabidhiwa kadi za Chama Cha CUF zilizotolewa na Wafuasi wa CUF waliojiunga na CCM.

Aliyekuwa  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo , Ramadhani Suleiman akizungumza katika mkutano wa mapokezi ya Dk.Bashiru mara baada ya kujiunga na CCM leo. 

 Aliyekuwa Katibu Mkuu wake Khamis Ali Lila amabye aliyewai kugombe nafasi ya urais mwaka 2016 akizungumza katika mkutano wa mapokezi ya Dk.Bashiru mara baada ya kujiunga rasmi na CCM.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza katika mkutano huo wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru.

 WANACCM walioudhuria katika Mkutano wa Mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru uliofanyika Kisiwandui Zanzibar.

 KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akiwahutubia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi walioshiriki katika mapokezi yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni