Jumanne, 9 Januari 2018

MATUKIO KATIKA PICHA YA MATEMBEZI YA VIJANA YA KUAENZI MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA MWAKA 1964 YALIYOTIMIZA MIAKA 54.

MWENYEKITI wa UVCCM Taifa  Kheri James (kulia) akisalimiana na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar  Abdul-ghafari Idrissa Juma (kushoto) kabla ya kuanza matembezi ya Umoja huo ya kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyotimiza miaka 54.
 MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheri James(kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Kamaria Suleiman Nassor baada ya kuwasili katika kiwanja cha kuanzia matembezi hayo. VIONGOZI mbali mbali wa UVCCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri James, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Mwita, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar  Abdul-ghafari Idrissa poamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis.

 KAIMU Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar akizungumza kabla ya kuanza matembezi hayo huko katika kijiji cha Mwera Unguja.

 MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheri James akiwasalimia vijana zaidi ya 1000 kutoka Mikoa yote ya Zanzibar na baadhi ya Mikoa ya Tanzania bara walioshiriki katika matembezi hayo.

 MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheri James(kulia) akimkabidhi kiongozi wa matembezi Asya Ali Khamis picha ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume ikiwa ni ishara ya kuanza matembezi hayo.

 MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheri James(kulia) akimkabidhi kiongozi wa matembezi Asya Ali Khamis picha ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ikiwwa ni ishara ya kuanza kwa matembezi hayo.

 MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheri James(kulia) akimkabidhi kiongozi wa matembezi Asya Ali Khamis picha ya Aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni ishara ya kuanza matembezi hayo.

 MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheri James(kulia) akimkabidhi kiongozi wa matembezi Asya Ali Khamis picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  ikiwwa ni ishara ya kuanza kwa matembezi hayo.

 MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheri James(kulia) akimkabidhi kiongozi wa matembezi Asya Ali Khamis bendera ya Taifa ya Zanzibar ikiwwa ni ishara ya kuanza kwa matembezi hayo.

 VIJANA wa UVCCM wakiwa na picha za Marais wa sasa na wastaafu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.

 Vijana wa UVCCM wakiwa katika matembezi hayo

 VIJANA wa kikundi cha  Brass Band cha Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar wakiongoza matembezi hayo kwa wimbo maalum.
 BAADHI ya viongozi wa UVCCM  akiwemo na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed wakiwa katika matembezi hayo.

 MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheri James akiwafariji vijana wa UVCCM mara baada ya kufika katika kituo cha kwanza kwa ajili ya Mapumziko katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Mjini iliyopo Aman Mjini Unguja.


 MAMIA ya vijana wa UVCCM na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi walioshiriki katika matembezi hayo.
 VIONGOZI mbali mbali wa CCM wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Saadalla Mabodi, Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib(wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Mkoa Kusini Ramadhan Abdalla Ali.


 BAADHI ya maafisa wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar walioshiriki matembezi hayo.Maoni 4 :

 1. Imependeza Sana. Hongereni Sana vijana mliotuwakilisha. Muungano udumu milele.

  JibuFuta
 2. Kazi nzuri na ya mfano kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Hatuna budi kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar ili kurithisha vizazi na vizazi historia hii njema

  JibuFuta
 3. Ni jitihada nzuri,vijana na jamii kwa ujumla,tuendelee kujitolea katika majukumu mbalimbali ya ujenzi Wa taiga.

  JibuFuta
 4. Ni jitihada nzuri,vijana na jamii kwa ujumla,tuendelee kujitolea katika majukumu mbalimbali ya ujenzi Wa taiga.

  JibuFuta