Jumanne, 29 Mei 2018

KINANA ATANGAZA RASMI KUSTAAFU UKATIBU MKUU WA CCM.


KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM (NEC) KINACHOENDELEA KUFANYIKA CHINI YA UENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM,DKT JOHN POMBE MAGUFULI KIMEPITISHA MAJINA MAWILI YA WAJUMBE WAPYA WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NEC AMBAO NI WAZIRI MKUU MSTAAFU WA AWAMU YA NNE NDUGU MIZENGO PETER PINDA NA NDUGU MAKONGORO NYERERE.

KIKAO HICHO PIA KIMEPIGA KURA YA KUWAPATA WAJUMBE SITA  KWA KUZINGATIA JINSIA WATATU KUTOKA TANZANIA BARA NA WATATU KUTOKA TANZANIA ZANZIBAR AMBAO WATKUWA WAJUMBE WA KAMATI KUU

MAJINA 14, TISA KUTOKA KILA UPANDE YALIPENDEKEZWA KUWANIA NAFASI HIZO.



MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. MAGUFULI AONGONZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM


 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli  akiwa meza kuu katika Ukumbi wa mikutano wa Kikwete kwa ajili ya kuongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) leo Jumatatu Mei 28, 2018. Kushoto ni Makamu Mwenyeti wa CCM Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na kulia ni Mamaku Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.

 Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.

Jumamosi, 12 Mei 2018

MAKATIBU NA WENYEVITI WA CCM NA JUMUIYA ZAKE JIMBO LA MAHONDA WAPEWA MAFUNZO

MBUNGE wa CCM Jimbo la Mahonda Zanzibar Mhe. Bahati Ali Abeid akifungua mafunzo ya siku moja kwa makatibu na wenyeviti wa CCM na jumuiya zake ngazi za matawi hadi jimbo hilo, yaliyofanyika katika ofisi ya CCM jimbo la mahonda iliyopo Kinduni.

 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya organazesheni CCM Zanzibar  ndugu Bakari Hamad Khamis akitoa mada ya Historia ya kuzaliwa kwa CCM katika mafunzo hayo.

 WENYEVITI na makatibu wa CCM na jumuiya zake ngazi za matawi hadi jimbo la mahonda  walioshiriki mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo.

 KATIBU msaidizi wa CCM, Idara ya organazesheni Hamid Saleh Mhina akizungumza katika mafunzo.

 


MBUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Mahonda, Bahati Ali Abeid amewataka watendaji na viongozi wa ngazi mbali mbali za Chama na jumuiya katika jimbo hilo kufanya kazi kwa bidii ili kuimarisha taasisi hiyo kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo makatibu na wenyeviti wa  CCM na Jumuiya zake ngazi za matawi hadi jimbo huko katika ofisi ya Jimbo la mahonda iliyopo Kinduni Wilaya ya Kaskazini 'B' Unguja.

Amesema viongozi hao wanatakiwa kufanya kazi za CCM na kutekeleza maagizo mbali mbali ya viongozi wa ngazi za juu kwa lengo la kuongeza kasi ya kuwatumikia wananchi waliokipa ridhaa  Chama kuongoza dola.

Mh. Bahati amewakumbusha viongozi hao kwamba wanakiwa kulinda na kutetea maslahi ya CCM kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili Chama kishinde katika uchaguzi mkuu ujao.

Amesema viongozi hao wanatakiwa kufuatilia kwa makini mafunzo hayo ambayo ni miongoni mwa nyenzo za kurahisisha majukumu yao ya kiutendaji ndani Chama Cha Mapinduzi.

Ameeleza kuwa baada ya mafunzo hayo Chama kinatarajia kuona mabadiliko ya haraka ya kiutendaji kutoka kwa viongozi na watendaji hao.

"Baada ya mafunzo haya mnatakiwa kusimama imara na kujiamini ili wanachama waliokuchagueni muwe viongozi waone umuhimu wenu katika kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.

Pia mnatakiwa kufanya maamuzi na kujadili matatizo na kero za wanachama kupitia vikao halali vya kikatiba ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima katika ngazi zenu za kiutendaji na kiuongozi", alisema Mbunge huyo ambaye ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya Jimbo hilo.

Akitoa mada ya kuliwa kwa CCM, Katibu wa Kamati maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar  Bakari Hamad Khamis, alisema CCM ina historia ndefu ambayo msingi wake unatokana na juhudi za waasisi wa ASP na TANU ambao ni marehemu Mzee Abeid Amani Karume  na Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika kuleta umoja na mshikamano kwa wananchi.

Amesema mwaka 1964 Chama cha ASP kiliamua kufanya Mapinduzi kwa lengo la kuwakomboa wananchi wa visiwa vya Zanzibar, waliotawaliwa kwa mabavu na utawala wa kisultani.

Alieleza kwamba baada ya Mapinduzi hayo waasisi hao walifanya maamuzi ya kuziunganisha nchi mbili ya Zanzibar na Tanganyika ili kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Pamoja na hayo Katibu huyo amefafanua kuwa mwaka 1977 vyama vya ASP na TANU baada ya kushauriana kwa muda mrefu vikaamua kuungana na kuunda Chama kimoja chenye nguvu ambacho ni Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa lengo la kusimamia siasa na demokrasia za kweli kwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania bara.

Katibu huyo Bakari amewasisitiza vijana nchini kusoma historia halisi ya Zanzibar ili wajifunze na kutambua mambo ya maendeleo yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake kwa awamu mbali mbali za uongozi wa dola.



Jumanne, 8 Mei 2018

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA MABALOZI WILAYA YA DIMANI, ASEMA MAFANIKIO NI MENGI KULIKO CHANGAMOTO

 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia mabalozi wa CCM Wilaya ya Dimani.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara yake ya kuzungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya Dimani.

 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Magharibi Mohamed Rajab Sudi akizungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya Dimani.

 MABALOZI wa CCM wilaya ya Dimani wakifuatilia kwa kina hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.

BAADHI ya viongozi na mabalozi wa CCM Wilaya ya Dimani wakiimba wimbo wa mashujaa wa Zanzibar katika ziara ya Dk.Shein ya kuzungumza na mabalozi wa Wilaya ya Dimani.

 MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Dimani Hussein Ali Mgema 'Kimti' akizungumza na mabalozi wa wilaya hiyo katika ziara ya Dk.Shein.

 MSOMA risala ya mabalozi wa Wilaya ya Dimani Mwanakheir Iddi akisoma risala hiyo kwa mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.





MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein amesema serikali ya awamu ya saba chini uongozi wake ametekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa kiwango kikubwa kwa lengo la kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi.

Pia amesema  mafanikio yaliyotokana na utekelezaji huo wa sera imara za Chama Cha Mapinduzi ni makubwa kuliko changamoto zilizobaki kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na mabalozi wa CCM Wilaya Dimani katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini uliopo Amani Unguja, alisema serikali imeimarisha sekta za afya, elimu, maji safi na salama,umeme  pamoja na ukarabati na ujenzi wa barabara za kisasa.

Amesema serikali inaendelea na mikakati ya kumaliza tatizo la kujaa maji katika eneo la Mwanakwerekwe sokoni kwa kuanza ujenzi wa kuinua barabara kutokea makutano ya barabara  ya Mwanakwerekwe hadi makaburini sambamba na ujenzi wa  mitaro mikubwa itakayopitisha maji kuelekea baarini kupitia shehia za Magogoni, Amani mboriborini hadi Pwani ya kinazini.

Amefafanua kuwa katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kabla ya mvua za masika mwaka 2019 kiasi cha Dola za kimarekani milioni 33 zimetengwa ambazo ni mkopo kutoka Benki kuu ya Dunia.

Dk. Shein amesema Serikali pia imedhamiria kutenga bajeti itakayomaliza tatizo la kujaa maji katika maeneo ya kibondemzungu ili kuwaondoshea wananchi usumbufu wanaopata katika mvua za masika.

Katika ziara hiyo aliwataka Mabalozi hao washirikiane na wanachama katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama na kuwa karibu na wananchi wa makundi yote.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi amesema Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Dimani imepiga hatua katika kuimarisha Chama cha mapinduzi ikiwemo kuvunjwa kwa makundi ya kuharisha uhai wa Chama ndani Wilaya hiyo.

Mapema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Mohamed  Rajab Sudi, ameeleza hali ya kisiasa katika mkoa wake imeimarika kutokana na umoja na mashirikiano yaliyopo kati ya Viongozi wa wanachama na serikali.

Akisoma Risala ya Mabalozi, Mwanakheir Iddi waliipongeza  Serikali kwa kutekeleza miradi ya kimaendeleo jambo ambalo limejenga imani kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar.

Ziara hiyo ya Makamo mwenyekiti CCM Zanzibar  iliyoanza May 2, mwaka 2018 Kisiwani Pemba iliyokuwa na lengo la kuimarisha Chama na kuzungumza na Mabalozi wa Mikoa yote ya Unguja na Pemba imefika tamati May 8, mwaka huu katika Mkoa wa Magharibi kwa kuzungumza na Mabalozi wa Wilaya za  Mfenesini.




Jumatatu, 7 Mei 2018

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA MABALOZI WILAYA YA AMANI, APOKEA WANACHAMA WAPYA.

 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia mabalozi wa CCM Wilaya ya Amani, katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini uliopo Amani Zanzibar.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kadi ya CCM mwanachama mpya aliyejiunga na Chama katika mwendelezo wa ziara zake katika Wilaya CCM Amani.
 ALIYEKUWA Kada wa CUF aliyejiunga na CCM Salim Mussa Omar(kushoto), akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.


WANACHAMA wapya wa CCM wakila kiapo  cha  Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ziara ya Dk.Shein Wilaya ya Aman.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akionyesha kadi za CUF zilizorejeshwa na aliyekuwa kada wa Chama hicho aliyejiunga na CCM Salim Mussa Omar, katika ziara ya Dk.Shein.


MABALOZI na viongozi mbali mbali wa CCM Wilaya ya Amani walioshiriki mkutano wa kuimarisha Chama katika ziara ya Dk.Shein.

 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib akizungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya Amani katika ziara ya Dk.Shein.

 MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Amani Abdi Mzee 'Mrope' akizungumza na mabalozi wa CCM Wilaya hiyo.


JUMLA ya wanachama wapya 1457 akiwemo kigogo mmoja wa Chama Cha CUF wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Amani.

Wanachama hao wamepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa (CCM) Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika mwendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya Amani Unguja.

Mapokezi hayo ya wanachama wapya yamejumuisha na aliyewahi kuwa mjumbe wa Baraza la vijana CUF Taifa,  Salim Mussa Omar ambaye amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi.

Katika ziara hiyo Dk.Shein aliwambia mabalozi hao kwamba wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa ili kukiletea ushindi Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema ushindi wa CCM unatokana na juhudi za mabalozi ambao wanatakiwa kueleza vizuri sera za CCM kwa wananchi waliopo katika ngazi ya mashina.

Aliitaja dhamira ya serikali ni kutekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020, ili Zanzibar iwe na miji bora nay a kisasa.

Alisema katika kutekeleza mipango hiyo tayari serikali imefungua milango ya uwekezaji kwa wageni na wazawa ili wawekeze katika sekta ya ujenzi wa miji ya kisasa ikiwemo maeneo ya Fumba, Nyamanzi na Matemwe na inaendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi wa nyumba za kisasa katika maeneo ya Chumbuni na Kwahani.

“Mipango hii ya kuifanya Zanzibar kuwa nchi yenye makaazi ya kisasa inawezekana, lakini lazima tufanye kazi ya ziada ya kuhakikisha serikali ya CCM inaendelea kubaki madarakani.”, aliwambia Mabalozi hao Dk.Shein.

Kupitia hotuba hiyo Dk.Shein alisema hatowavumilia baadhi ya watu wanaotaka kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.

Alieleza na kuongeza kuwa maendeleo yaliyopatikana visiwani Zanzibar yametokana na  uwepo wa amani na utulivu.

Dk.Shein ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alisema kuna watu waliowahi kuanzisha vikundi vya kuchafua hali ya amani lakini wamedhibitiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

“ Nchi mbali mbali walichezea amani na utulivu wa nchi na sasa wameshindwa kurejesha hali hiyo na badala yake mamia ya wananchi wasiokuwa na hatia wanakufa kila siku”, alieleza Dk.Shein.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk.Abdalla Juma Mabodi alisema ziara hiyo ya Dk. Shein inatokana na matakwa ya sera za CCM zinazomtaka kila kiongozi kushuka ngazi za chini kuangalia utekelezaji wa ilani na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi.

Alieleza kuwa Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuaminiwa na wananchi kutoka na utarabu wake wa uongozi shirikishi kwa wanachama wote.

Akizungumza Mwenyekiti wa Mkoa huo, Talib Ali Talib alimpongeza Dk.Shein kwa juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa mijini na vijijini.

Mapema akisoma risala ya mabalozi hao, Fatma Kassim alisema viongozi hao wanaridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 iliyotekelezwa ndani ya Wilaya hiyo.

 Mabalozi hao wamesema serikali imejenga mitaro mikubwa ya kusafirisha maji machafu katika majimbo ya Magomeni, Mpendae ,Shaurimoyo na Chumbuni pamoja na ujenzi wa skuli ya ghorofa iliyopo Mabanda ya ng’ombe Chumbuni.

Nyingine ni Ukarabati wa barabara ya Saaten hadi Shirika la Umeme Gulioni pamoja na uwekaji wa taa za barabarani katika Wilaya hiyo.

Aidha wamezitaja Changamoto zinazowakabili kuwa ni upungufu wa ajira kwa vijana, tatizo la udhalilishaji wa kijinsia na baadhi ya watendaji wa serikali kuwadharau viongozi na watendaji wa Chama.

Pamoja na hayo mabalozi hao wameahidi kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda na kuendelea kuongoza Dola.

Jumapili, 6 Mei 2018

DK.SHEIN-ASEMA WANAOKWEPA KUTEKELEZA ILANI WASIPE FOMU ZA KUGOMBEA UONGOZI


 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia na mabalozi wa CCM Wilaya ya kaskazini ''A'' Unguja.

 MAKAMU Mwenyuekiti wa UWT Taifa Thuwayba Kisasi akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika Afisi ya CCM Mkoa wa kaskazini mahonda katika mwendelezo wa ziara zake za kuzungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya kaskazini ''A''.
 BAADHI ya mabalozi wa CCM Wilaya ya kaskazini'' A'' wakifuatilia kwa makini hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Mabodi akizungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya kaskazini 'A' Unguja.

 MAKATIBU wa Idara Maalum ya NEC CCM Zanzibar wakijitambulisha kwa mabalozi wa CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja.

 MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa UWT  Taifa Thuwayba Kisasi (kulia) wakiwasalimia mabalozi wa Wilaya ya kaskazini ''A''.

 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akionyesha Ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015/2020.

 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisisitiza umuhimu wa mabalozi kusoma Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2017.


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM), Dk. Ali Mohamed Shein ameitaka Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, kutowapatia fomu za kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao  Wabunge, Wawakilishi na madiwani wanaoshindwa kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Pia Dk. Shein amesema suala la viongozi hao kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kiongozi yeyote aliyepewa ridhaa ya kuwatumikia wananchi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Agizo hilo amelitoa katika mwendelezo wa ziara zake wakati akizungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja, huko katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja-Mahonda.

Dk.Shein alisema kiongozi yeyote ndani ya CCM anayeshindwa kutekeleza kwa wakati ahadi alizotoa kwa wananchi asipewe nafasi nyingine ya kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Aliwambia mabalozi hao kwamba CCM haitowaonea huruma Wabunge, Wawakilishi na Madiwani waokwepa kutekeleza majukumu yao na badala yake kukiletea Chama mzigo mkubwa wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

"Wakumbusheni Wabunge, Wawakilishi na madiwani kutekeleza ahadi zao kwa wakati na wakikataa basi katika uchaguzi mkuu ujao msiwape fomu za kugombea tena.", alisisitiza Dk. Shein.

Agizo hilo Dk.Shein alilitoa kufuatia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Idd Ali Ame kusema kuwa  Kamati ya siasa ya Mkoa wake tayari imefanya ziara ya kuimarisha Chama katika majimbo tisa(9) ya mkoa huo na kupokea malalamiko ya baadhi ya viongozi hao wa majimbo kushindwa kutekeleza ahadi walizoahidi kwa wananchi.

Akizungumza katika Mkutano huo Dk.Shein alisema Chama Cha Mapinduzi kinawategemea na kuwaamini mabalozi katika kulinda, kutetea na kukiletea ushindi Chama kwa kila uchaguzi kwani wao ndio waliokuwa karibu zaidi na wananchi wa makundi yote.

Amewataka mabalozi hao kulinda maadili, miongozo na miiko ya Chama Cha Mapinduzi ili taasisi hiyo ya kisiasa iendelee kubaki katika misingi yake ya kiuongozi na ustawi wa demokrasia.

 Pamoja na hayo hayo Dk. Shein alisema hafurahishwi na kuripotiwa kwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto, hivyo mamlaka husika zinatakiwa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaofanya matukio hayo.

Aliwakumbusha mabalozi hao kuwa mstari wa mbele kutangaza mambo mema yanayotekelezwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili wananchi waliopo katika maeneo yao waweze kuyafahamu.

Dk.Shein alisema serikali inaendelea na jitihada za kutekeleza miradi ya kimaendeleo kwa wananchi, ikiwemo ujenzi wa barabara za kisasa ndani ya Mkoa huo za maeneo ya Mkwajuni-Kijini km 7.6.

Zingine ni barabara za Mkwajuni-Mbuyu maji km 22, Pale-Kiongele km 4.6 pamoja na Bububu-Kinyasini zote zikiwa ni miongoni mwa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Aidha Dk.Shein alisema serikali ina dhamira ya kujenga mji wa kisasa katika eneo la Mkokotoni ili kwenda sambamba na dhana ya kuifanya Zanzibar kuwa na miji ya kisasa.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi ameeleza kuwa viongozi wa chama na serikali wamekuwa wakishirikiana vizuri katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Dk.Mabodi amesifu juhudi za kuimarisha Chama Cha Mapinduzi zinazofanywa na uongozi mpya wa Mkoa huo kuwa zinajenga matumaini na uaminifu kwa Wana-CCM.

Akisoma risala ya mabalozi, Jafar Ali Haji alisema wanampongeza Dk.Shein kwa kuendelea kuongoza serikali kwa ufanisi mkubwa, sambamba na kusimamia vizuri utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa vitendo.

"Tunakupongeza Dk.Shein kwa mambo mengi mazuri uliyoyafanya kwa maslahi ya wananchi wa Wilaya ya Kaskazini 'A' na maeneo mengi hasa kuanzisha mfuko ya pencheni ya wazee tunayopata shilingi 20,000 kwa kila mwezi.

Kupitia risala hiyo walieleza kuwa tayari maagizo ya Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, aliyotoa katika ziara zake za kiserikali mwaka jana yametekelezwa kwa kiwango kikubwa katika vijiji vya Mbuyu tende na Mlilile na kwa sasa wananchi wa  wanapata huduma za maji safi na salama, skuli na barabara.

Mabalozi hao walisema licha ya mafanikio hayo bado Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi kwa ngazi ya sekondari na msingi pamoja na upungufu wa wauguzi katikka vituo vya Afya ya Wilaya hiyo hasa kituo cha Kivunge. 

                                


DK.SHEIN-ATOA ONYO KALI KWA WASAKA URAIS WA Z'BAR.


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

 MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwahutubia Mabalozi wa CCM Wilaya ya Kati Unguja, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar (SUZA) kilichopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

  MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akipokea risala ya mabalozi wa CCM Wilaya ya Kati Unguj.

 BAADHI ya wajumbe wa NEC waliofuatana na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika ziara yake ya kuzungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja.
 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhani Abdallah Ali 'Kichupa' akizungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya kati , kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Dk.Mabodi katika ziara ya Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Shein kuzungumza na mabalozi.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Jumsa Mabodi pamoja na viongozi mbali mbali wa CCM na junmuiya zake waliofutana na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakiimba wimbo wa mashujaa wa Zanzibar katika ziara ya kuzungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya Kati.




      MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein amewaonya baadhi ya watu wanaofanya kampeni za kusaka Urais wa Zanzibar kabla ya muda wa kufanya hivyo kufika na kusisitiza  kuwa yeye bado ni Rais wa Zanzibar.

Amesema kuna baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali tayari wameanza kupanga timu za Urais badala ya kushughulika na mambo ya msingi ya kufanya shughuli za Chama zitakazofanikisha kuiweka serikali madarakani katika uchaguzi mkuu ujao.

Onyo hilo amelitoa katika mwendelezo wa ziara zake za kuimarisha Chama Cha Mapinduzi kwa kuzungumza na mabalozi wa mashina katika Wilaya ya kati Unguja,iliyofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA) ulipo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema nafasi ya Urais ndani ya CCM haipatikani kwa kampeni na makundi yasiyokuwa halali bali inapatikana kwa utaratibu maalum kupitia vikao vya kikatiba ambavyo vipo kwa mujibu wa Katiba na miongozo na kanuni  mbali mbali za CCM.

Alibainisha kuwa kwa wakati tofauti amewatahadharisha baadhi ya viongozi na wanachama hao kuacha tabia hizo kwani zinaweza kuleta migogoro na mgawanyiko isiyokuwa ya lazima ndani ya CCM kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Amebainisha kuwa watu hao wanaosaka Urais kwa sasa wasipoacha tabia hiyo na kuvumilia mpaka 2020, atawachukulia hatua kali za kinidhamu zikiwemo kufikishwa katika vikao vya usalama na maadili vya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ili wahojiwe na kuchunguzwa dhidi ya mwenendo wao  juu ya mwenendo wao usiokuwa na manufaa kwa CCM.

Alisema viongozi, watendaji na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wanatakiwa kuelekeza nguvu zao katika kutekeleza mipango mbali mbali ya kukisaidia Chama kushinda na sio kuangaika na urithi wa kiti cha Urais.

“Naheshimu Katiba ya nchi muda wangu ukifika naondoka madarakani kwani huo ndio utaratibu wa Chama chetu na kwa mujibu wa sheria za nchi, lakini sifurahishwi hata kidogo kuona baadhi yenu mnaanza kuangaika na Urais badala ya kufanya kazi za kuitafutia ushindi CCM mwaka 2020", alisisitiza Dk.Shein na kuwataka Mabalozi na viongozi wengine wa ngazi za mashina kukataa kuingizwa katika mitandao hiyo ya kampeni.

Akizungumzia umuhimu wa viongozi hao, Dk.Shein alisema CCM inathamini mchango mkubwa wa kuimarisha Chama unaofanywa na viongozi wa mashina ambao ndio jeshi la kisiasa la Chama Cha Mapinduzi.
Alisema Chama kitaendelea kuisimamia vizuri serikali ili itekeleze Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kama ilivyowaahidi wananchi katika kampeni za uchaguzi zilizopita.

Kupitia mkutano huo Dk.Shein aliwataka viongozi hao kujenga utamaduni wa kusoma Katiba ya CCM  ya mwaka 1977 toleo la 2017, ili wajue majukumu waliokuwa nayo kwa mujibu wa Katiba na kuyatekeleza ipasavyo.

Alisema katika hatua za kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wananchi, serikali inaendelea na mikakati ya matengenezo ya barabara ya maeneo ya Mwanakwerekwe na kutengeneza daraja la kisasa katika eneo la Kibonde mzungu ili kuwaondoshea usumbufu wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja.

Aidha alisema kwa upande wa changamoto ya maji yanayotwaama katika eneo la Kibonde mzungu tayari serikali inaendelea na mikakati ya kuanza ujenzi wa daraja kubwa litakaloweza kumaliza tatizo hilo la maji katika maeneo hayo.

Pia aliwambia mabalozi hao kuwa hakuna wa kuzuia ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao kwani Chama hicho kimejiandaa kushinda kwa nguvu za demokrasia, kwani kina wananchi wengi wanaokiamini na kukiunga mkono kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020.

Alisema Serikali inaendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira ya ASP ya kuwapatia wananchi huduma bure za kijamii hasa elimu na Afya.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi, amesema mabalozi wa Chama Chama Mapinduzi wamekuwa mstari wa mbele kurejesha Chama kwa wananchi.

 Alisema Chama Cha Mapinduzi kwa sasa kinaendelea na mfumo wa uongozi shirikishi unaowashirikisha viongozi wa ngazi tofauti jambo ambalo Dk.Shein anaendeleza mfumo huo kwa kuzungumza na mabalozi hao kila mwaka.

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Ramadhan Abdalla Ali 'Kichupa', alipongeza Dk.Shein kwa juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa huo katika nyanja za kijamii,kiuchumi na kisiasa.

Mapema akisoma risala ya mabalozi, ndugu Mkombe Vuai Khamis alisema serikali ya awamu ya saba inayoongozwa na Dk.Shein wananchi wameshuhudia kuimarika kwa sekta mbali mbali nchini hasa suala zima la kuanzisha penchini ya kuwalipa  wazee ya shilingi 20,000 kwa kila mwezi.

Kupitia risala hiyo walimpongeza Dk.Shein kwa kuasisi na kuendeleza kwa vitendo hatua yake ya kutoa pencheni kwa wazee hatua ambayo ni ya kishujaa kwani imesaidia mamia ya wazee wengi kupata fedha za kujikimu kila mwezi.

Walisema wataendelea kulinda na kutetea maslahi na miongozo ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo ili kishinde kwa ngazi zote katika uchaguzi mkuu ujao.




Jumamosi, 5 Mei 2018

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA DK.SHEIN YA KUZUNGUMZA NA MABALOZI WILAYA YA KUSINI UNGUJA


 MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na mabalozi na viongozi mbali mbali wa CCM ngazi za mashina katika Wilaya ya Kusini Unguja.
 MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika mawendelezo wa ziara zake za kuzungumza na mabalozi katika Wilaya ya Kusini Unguja.



 BAADHI ya mabalozi na viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali walioshiriki katika ziara ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi ya Dk. Shein kuzungumza na viongozi hao wa ngazi za mashina.
MSOMA risala ya mabalozi Bi. Mwajuma Ramadhani Abdalla(kulia) akimkabidhi  risala hiyo Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), mara baada ya kusomwa katika mwendelezo wa ziara hiyo Wilaya ya Kusini Unguja.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akisoma Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa mabalozi na viongozi wa ngazi za mashina Wilaya ya kusini Unguja.


 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Ndugu Ramadhani Abdallah Ali akizungumza na mabalozi hao kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu Dk. Mabodi ili amkaribishe mgeni rasmi.