MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia mabalozi wa CCM Wilaya ya Dimani. |
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Magharibi Mohamed Rajab Sudi akizungumza na mabalozi wa CCM Wilaya ya Dimani. |
MABALOZI wa CCM wilaya ya Dimani wakifuatilia kwa kina hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein. |
BAADHI ya viongozi na mabalozi wa CCM Wilaya ya Dimani wakiimba wimbo wa mashujaa wa Zanzibar katika ziara ya Dk.Shein ya kuzungumza na mabalozi wa Wilaya ya Dimani. |
MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Dimani Hussein Ali Mgema 'Kimti' akizungumza na mabalozi wa wilaya hiyo katika ziara ya Dk.Shein. |
MSOMA risala ya mabalozi wa Wilaya ya Dimani Mwanakheir Iddi akisoma risala hiyo kwa mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein. |
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein amesema
serikali ya awamu ya saba chini uongozi wake ametekeleza Ilani ya uchaguzi ya
CCM ya mwaka 2015/2020 kwa kiwango kikubwa kwa lengo la kumaliza changamoto
zinazowakabili wananchi.
Pia amesema mafanikio yaliyotokana na utekelezaji huo wa sera imara za Chama Cha
Mapinduzi ni makubwa kuliko changamoto zilizobaki kabla ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2020.
Hayo
ameyasema wakati akizungumza na mabalozi wa CCM Wilaya Dimani katika ukumbi wa
CCM Mkoa wa Mjini uliopo Amani Unguja, alisema serikali imeimarisha sekta za
afya, elimu, maji safi na salama,umeme
pamoja na ukarabati na ujenzi wa barabara za kisasa.
Amesema serikali inaendelea na mikakati ya kumaliza tatizo la kujaa maji katika eneo la
Mwanakwerekwe sokoni kwa kuanza ujenzi wa kuinua barabara kutokea makutano ya
barabara ya Mwanakwerekwe hadi makaburini
sambamba na ujenzi wa mitaro mikubwa
itakayopitisha maji kuelekea baarini kupitia shehia za Magogoni, Amani
mboriborini hadi Pwani ya kinazini.
Amefafanua kuwa katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kabla ya mvua za masika mwaka
2019 kiasi cha Dola za kimarekani milioni 33 zimetengwa ambazo ni mkopo kutoka
Benki kuu ya Dunia.
Dk.
Shein amesema Serikali pia imedhamiria kutenga bajeti itakayomaliza tatizo la
kujaa maji katika maeneo ya kibondemzungu ili kuwaondoshea wananchi usumbufu wanaopata
katika mvua za masika.
Katika
ziara hiyo aliwataka Mabalozi hao washirikiane na wanachama katika kusimamia
utekelezaji wa ilani ya Chama na kuwa karibu na wananchi wa makundi yote.
Nae
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi amesema Chama Cha Mapinduzi
wilaya ya Dimani imepiga hatua katika kuimarisha Chama cha mapinduzi ikiwemo kuvunjwa
kwa makundi ya kuharisha uhai wa Chama ndani Wilaya hiyo.
Mapema
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Mohamed Rajab Sudi, ameeleza hali ya kisiasa katika
mkoa wake imeimarika kutokana na umoja na mashirikiano yaliyopo kati ya
Viongozi wa wanachama na serikali.
Akisoma
Risala ya Mabalozi, Mwanakheir Iddi waliipongeza Serikali kwa kutekeleza miradi ya kimaendeleo jambo
ambalo limejenga imani kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar.
Ziara
hiyo ya Makamo mwenyekiti CCM Zanzibar iliyoanza
May 2, mwaka 2018 Kisiwani Pemba iliyokuwa na lengo la kuimarisha Chama na
kuzungumza na Mabalozi wa Mikoa yote ya Unguja na Pemba imefika tamati May 8, mwaka huu katika
Mkoa wa Magharibi kwa kuzungumza na Mabalozi wa Wilaya za Mfenesini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni