Jumatano, 31 Julai 2019

MHE.AMINA IDDI: AING'ARISHA UWT ZNZ KWA NYENZO ZA KISASA,ASEMA MASLAHI YA CCM YAWEKWE MBELE.

 MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi  Mhe.Amina Idd Mabrouk(wa pili kushoto) akikabidhi Komputa Moja kwa Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo(wa pili kulia) komputa hiyo kwa ajili ya Matumizi ya Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu huyo.

 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo(wa pili kulia) akimkabidhi Komputa Moja Katibu wa UWT Mkoa wa Magharibi Ndugu Zuwena Suleiman Mohamed (wa kwanza kushoto) kwa ajili ya Matumizi ya Ofisi ya Mkoa huo,iliyotolewa na  Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk(wa pili kushoto).

  NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo(wa pili kulia) akimkabidhi Komputa Moja Katibu wa UWT  Wilaya ya Mfenesini (wa kwanza kushoto Pili Issa Juma) kwa ajili ya Matumizi ya Ofisi ya Wilaya hiyo,iliyotolewa na  Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk (wa pili kushoto).

 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo(kulia),akimkabidhi Komputa Moja Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani Ndugu Sunna Said Mzee(wa kwanza kushoto),Komputa hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk(wa pili kushoto).

 MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk, akizungumza katika Hafla hiyo ya utoaji wa Komputa hizo, katika Hafla iliyofanyika Ofisi za CCM Kiembe Samaki Unguja.

 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo akizungumza katika Hafla ya utoaji wa komputa hiyo iliyofanyika katika Ofisi za CCM Kiembe Samaki Unguja.
 MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Magharibi Unguja akizungumza katika Hafla ya utoaji wa Komputa zilizotolewa na Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd iliyofanyika katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Kiembe samaki Znz.

 VIONGOZI na Wanachama wa UWT wa Mkoa wa Magharibi wakiwa katika hafla ya kukabidhi komputa nne ya Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk, iliyofanyika katika Ofisi za CCM Kiembe Samaki Unguja.


MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk,amewasihi Viongozi na Wanachama wa CCM kufanya Kazi za Chama Cha Mapinduzi kwa bidii ili kuandaa Mazingira rafiki ya Ushindi wa Mwaka 2020.  

Rai hiyo aliitoa wakati akikabidhi Komputa Nne zenye Thamani ya Shilingi Milioni Nane kwa Ofisi za UWT Zanzibar ambazo ni Afisi Kuu ya UWT Zanzibar, UWT Mkoa wa Magharib,UWT Wilaya ya Dimani na UWT Wilaya ya Mfenesini ambapo kila Ofisi imekabidhiwa komputa Moja,Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za CCM huko Kiembembe Samaki Unguja.

Mhe.Amina amesema ili Chama kishinde katika Uchaguzi Mkuu ujao kila mwanachama anatakiwa kuweka mbele maslahi ya CCM badala ya maslahi binafsi.

Katika maelezo yake Mhe.Amina, ameeleza kuwa Vifaa hivyo ni mwendelezo wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020,ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo ahadi alizozitoa kwa Wananchi.

Pamoja na hayo amewaahidi Akina Mama wa Mkoa wa Magharibi kuwa ataanzisha Vikundi vya Ujasiriamali ili kuwakwamua kiuchumi na waweze kujiajiri wenyewe na kuondokana katika wimbi la umaskini. 

Amewasihi  Viongozi na Wanachama wa UWT kuthamini juhudi za kimaendeleo zinazofanywa na Viongozi hao ili wazidi kupata nguvu na Uthubutu wa kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi.

Akizungumza katika Hafla hiyo Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo,amempongeza  Mbunge huyo Mhe. Amina na Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo ambao wamekuwa karibu na Wananchi kwa kutekeleza kwa Vitendo Ilani ya CCM.

 Ndugu Tunu, amewataka Viongozi na Watendaji waliokabidhiwa Komputa hizo kuzitunza vizuri ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuhakikisha shughuli za kiutendaji za UWT zinatekelezwa kwa ufanisi zaidi.

Amesema Viongozi wa Chama na Serikali wanatakiwa kufuata nyayo za Viongozi Wakuu ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa katika kuwatumikia Wananchi kwa uadilifu.

Awali Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi Ndugu Zainab Ali Maulid,amesema Umoja na Mshikamano ndio siri ya mafanikio ya kuimarika kwa Umoja huo.
  


Jumapili, 14 Julai 2019

MHE.FAHARIA AKABIDHI VIFAA VYA TSH.MILIONI 15 KWA UWT MAJIMBO 9 YA MKOA WA MJINI.MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja Bi.Ghanima Sheha akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Mkoa huo,huko katika Ukumbi wa Mkoa wa Mjini ulioopo Amani Unguja.

MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis  Shomari akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini kabla ya kukabidhi Vifaa.


BAADHI ya Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT  Mkoa wa Mjini wakisikiliza nasaha za mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini, kilichofanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja.


MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis Shomari (kulia),akimkabidhi Viti 50 Katibu wa UWT Jimbo la Magomeni Ndugu Khadija Rajab Pazi (kushoto).

MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis  Shomari(kulia) akimkabidhi Viti 50 Katibu wa UWT Jimbo la Kikwajuni Ndugu Amina Hassan Suleiman.


MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis  Shomari(kulia) akimkabidhi Viti 50 Katibu wa UWT Jimbo la Malindi Ndugu Salma Said Muumin.

MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis  Shomari akimkabidhi Katibu wa UWT Wilaya ya Amani Ndugu Asha Mzee Kiti Kimoja na Meza Moja vya Ofisi.

 MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini ambaye pia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakiklishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma,akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi Vifaa kwa Akina Mama wa UWT wa Majimbo 9 ya Mkoa wa Mjini.

 KATIBU wa UWT Mkoa wa Mjini Ndugu Stamili akitoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali ya Kiutendaji katika Kikao cha Baraza Kuu la UWT  Mkoa huo kilichofanyika sambamba na kukabidhi Vifaa kwa Akina Mama.

 MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Mhe.Saada Ramadhan,akizungumza katika hafla hiyo.MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis Shomari,amekabidhi Vifaa mbali mbali vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 15 kwa Majimbo yote ya UWT ndani ya Mkoa huo.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti 451,Meza Moja ya Ofisi na  Mashine  Moja ya kutengenezea Chaki ikiwa ni sehemu ya kuunga Mkoa juhudi za Ujasiliamali za Akina Mama wa Mkoa huo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi Vifaa hivyo Mbunge huyo Mhe.Faharia amesema lengo la kutoa Vifaa hivyo ni kutekeleza Ilani ya CCM ya Mwaka 2015/2020.

Mhe.Faharia ameeleza kuwa Akina Mama wa UWT ndani ya Mkoa huo pamoja na majukumu ya kisiasa waliyokuwa nayo bado wanatakiwa kujiajiri wenyewe kupitia ujasiriamali hivyo vifaa vilivyotolewa vitawasaidia katika harakati hizo za kujiajiri wenyewe.

Pamoja na hayo alitoa Wito kwa Wanawake wa rika mbali mbali ndani ya Mkoa wa Mjini kushiriki kaiunga Mkoa CCM ili ishinde katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

Katika hafla hiyo Wawakilishi wa Viti Maalum wa Mkoa huo ambao ni Mhe.Mgeni Hassan Juma ameahidi kutoa Mashine mbili za Photocopy kwa UWT Wilaya ya Amani na Mjini huku Mhe.Saada Ramadhan amekabidhi Mifuko Mitano ya Jipusamu kwa ajili ya kutengenezea chaki na kuahidi shilingi Milioni Moja kwa kila Wilaya zilizomo katika Mkoa huo.

Wakizungumza kwa wakati tofauti Makatibu wa UWT wa Majimbo yote yaliyomo katika Mkoa huo, wameahidi Vifaa hivyo kuvitunza na kuhakikisha wanavitumia katika matumizi yaliyokusudiwa.

Awali akifungua Kikao cha Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini Mwenyekiti wa Mkoa huo Ndugu Ghanima Sheha,amesema Kikao hicho kitajadili masuala mbali mbali ya kiutendaji na kutoa maelekezo ya kiutendaji juu ya ufanikishaji wa majukumu mbali mbali ya UWT na CCM kwa ujumla.

Jumamosi, 6 Julai 2019

U.W.T MKOA WA MAGHARIB WAFANYA MKUTANO WA BARAZA.

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Magharib Ndugu Mohamed Rajab Soud,akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Mkoa huo Mwera Unguja

MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Magharibi,Ndugu Zainab Ali Maulid (kushoto),akifungua Mkutano wa Baraza hilo la UWT Mkoa wa Magharibi.

BAADHI ya Wabunge na Wawakilishi wa UWT walioudhuria katika Mkutano wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi.

  KAIMU Katibu wa UWT Mkoa wa Magharibi, Ndugu Zuwena Suleiman Mohamed(wa kwanza kulia) akiwatambulisha viongozi mbali mbali walioudhuria katika Mkutano huo.

 BAADHI ya Viongozi wa UWT walioudhuria Mkutano huo wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi.

MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Magharibi,Ndugu Zainab Ali Maulid (kushoto),akiongoza kikao hicho cha Baraza la Mkoa huo akiwa na Kaimu Katibu wa UWT Mkoa wa Magharib,Zuwena Suleiman Mohamed(kulia).JUMUIYA za Chama Cha Mapinduzi Nchini zimetakiwa kuzidisha juhudi katika kufanya kazi za kuimarisha CCM ili Taasisi hiyo iendelee kuwa bora kisiasa Nchini.  

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharibi Ndugu Mohamed Rajab Soud,wakati akiwahutubia Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi Unguja. 

Amesema Jumuiya za CCM licha ya kufanya vyema katika majukumu yake ya kila siku bado zinatakiwa kuongeza kasi ya kiutendaji na kiubunifu hili kuhakikisha Chama ndani ya Mkoa huo kinaimarika Kisiasa,Kiitikadi na Kiuongozi.

Kupitia Mkutano huo Mwenyekiti huyo Ndugu Rajab, amewambia Akina Mama hao kuwa  Wanategemewa na Chama Cha Mapinduzi katika harakati mbali mbali za Kisiasa hivyo wanatakiwa kutumia uwezo wao wa Kisisa na Kitaaluma ili kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi wa mwaka 2020.

Amesema Akina Mama hao kwa juhudi zao za kutekeleza kwa wakati mwafaka hasa katika kufanya vikao mbali mbali vilivyoelekezwa na Katiba ya Jumuiya hiyo.

Amesema Viongozi na Wanachama kila mmoja kwa nafasi yake wanatakiwa wanatakiwa kuwaeleza Wananchi katika maeneo yao Utekelezaji wa Ilani ya CCM unaotekelezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wabunge,Wawakilishi na Madiwani.

Aidha amesema Mkoa huo upo katika maandalizi ya kutekeleza kwa Vitendo kampeni ya Magharibi ya Kijani kwa kuhakikisha Mkoa huo unakuwa ni Ngome imara ya CCM Kisiasa.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo,Ndugu Zainab Ali Maulid amesema Jumuiya hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza kazi mbali mbali za kuleta maendeleo endelevu ndani ya CCM.

Ameeleza kuwa  kwa sasa jumuiya hiyo inaendelea na mipango ya kuongeza Wanachama wapya hasa Wanawake ili kuhakikicha CCM inaingia katika Uchaguzi Mkuu Ujao ikiwa na Takwimu sahihi za Wanachama wenye sifa za kupiga kura.

Akitoa Shukrani kwa niaba ya Jumuiya hiyo,Mbunge wa Jimbo la Welezo Dkt.Saada Mkuya amesema nasaha zilizotolewa na Mgeni rasmi watazifanyia kazi kwa vitendo sambamba na kuwahamasisha Wanawake wengine waendelee kulinda,kuthamini na kutetea maslahi ya CCM.

 

Alhamisi, 4 Julai 2019

WAZEE WA CCM ZANZIBAR WASOMA HITMA YA DK.BADRIYA.


 BAADHI ya Viongozi na Wazee wa CCM Zanzibar wakiwa katika Kisomo cha Hitma ya Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Badriya Abubakar Gurnah, kilichoandaliwa na Baraza la Wazee wa CCM Zanzibar na kimefanyika Nyumbani kwake Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Rahaleo Unguja.


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, akitoa shukrani kwa Wananchi na Wazee wa CCM walioudhuria Kisomo hicho cha Hitma ya Marehemu Dk.Badriya.
BAADHI ya Viongozi na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi kwa upande wa Wanawake walioshiriki katika Kisomo cha Hitma hiyo ya Marehemu Dk.Badriya.


 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,akipewa mkono wa pole na Wazee mbali mbali wa Chama mara baada ya Kisomo hicho.


WAZEE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar pamoja na Viongozi na Wananchi mbali mbali wameungana kusoma Hitma ya Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Badriya Abubakar Gurnah.  

Kisomo hicho kilichoandaliwa na Wazee wa Chama kimeudhuriwa na Viongozi na Watendaji wa Serikali,Chama na Jumuiya zake pamoja  Wananchi kwa ujumla.

Akitoa Shukurani zake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,amewashukuru Wazee hao na Wananchi mbali mbali kwa mchango walioutoa kabla na baada ya Msiba huo.

Kwa upande wa Wazee hao wametoa pole kwa Familia ya Dk.Mabodi na kuwasihi waendelee kuwa na subri huku wakiungana na Wananchi wengine kumuombea Dua Marehemu.

Kisomo hicho cha Hitma kimesomwa Nyumbani kwake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Mabnodi  Mtaa wa Rahaleo Unguja.