Alhamisi, 29 Novemba 2018

DK.MABODI: ASEMA MIRADI INAYOTEKELEZWA CHINI YA KIWANGO HAIKUBALIKI.



NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akivuna Tungule katika Shamba la wakulima waliopewa mafunzo ya kilimo cha kisasa huko shehia ya Kisauni.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akikagua kiti maalum cha kung'olea meno katika kituo cha Afya cha Kombeni.

 VITANDA Vya Kisasa kwa ajili ya huduma za kujifungua kwa Akina Mama Wajawazito katika Kituo cha Afya Kombeni.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akibadilishana mawazo na madaktari wa kujitolea kutoka nchi za nje waliopo katika kituo cha Afya cha Kombeni.



 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akipewa maelezo juu ya ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Jeshi la Polisi katika eneo la Chukwani kinachojengwa na serikali ya Mkoa Mjini Magharib na Manispaa ya Magharib 'B' kwa lengo la kuthibiti uhalifu katika mitaa hiyo na shehia jirani.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akizungumza na Watendaji na Viongozi wa Baraza la Manispaa ya Magharib 'B' kabla ya kutembelea miradi.

 MKURRUGENZI wa Manispaa ya Magharib 'B' Ali Abdalla Natepe akisoma ripoti ya utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja utekelezaji wa mfumo wa ugatuzi.

 MKUU wa Mkoa Mjini Magharib Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud akitoa ufafanuzi wa hoja mbali mbali katika kikao hicho.   

 BAADHI ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar NEC walioshiriki katika ziara hiyo

 BAADHI ya Watendaji wa Baraza la Manispaa Magharib 'B ' wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akipewa maelezo ya bidhaa mbali mbali zinazotengenezwa kupitia mazao ya baharini yakiwemo mwani.

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

NAIBU katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi amesema CCM itawachukulia hatua za kali za kisheria Watendaji watakaoruhusu kutekelezwa chini ya kiwango miradi mbali mbali katika  Mabaraza ya Manispaa na Halmashauri za Wilaya Zanzibar.

Kauli hiyo ameitoa katika mwendelezo wa ziara yake katika Manispaa ya Magharib 'B' ,amesema lazima miradi yote hasa inayotekelezwa na mamlaka hizo chini ya mpango wa ugatuzi iwe ni miradi imara iliyopo katika viwango bora.

Amewambia Watendaji hao kuwa lazima wahakikishe miradi yote inayotekelezwa kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za kijamii ziwe na viwango vinavyoridhisha na sio vya kuitia hasara Serikali za Mitaa pamoja na wananchi kwa ujumla.

Dk. Mabodi amesema yeye akiwa ni msimamizi Mkuu wa  Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa upande wa Zanzibar, ataendelea kufuatilia kwa karibu miradi yote inayotekelezwa na ugatuzi kwa lengo la kujiridhisha kama ina viwango vinavyostahiki.

Dk. Mabodi ameeleza kuwa miradi ya kijamii inayotekelezwa katika kiwango bora,inasaidia kupunguza gharama zisizokuwa za lazima na kuwawezesha wananchi kupata kwa wakati mahitaji muhimu ya kijamii.

"Wananchi wanahitaji huduma bora na sio bora huduma ni lazima watendaji mliopewa dhamana kupitia mfuko wa ugatuzi muwe waadilifu wa kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa inafuata taratibu zote za kisheria na inakuwa na viwango vinavyositahiki. "ameeleza Dk. Mabodi.

Pia amesisitiza manispaa hiyo kuendelea kutumia mfumo wa kisasa wa ukusanyaji wa mapato  ili kudhibiti ukwepaji wa kodi.

Akizungumza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud amesema dhana ya ugatuzi imetekelezwa kwa ufanisi katika Manispaa ya Magharib 'B' kwa kuwanufaisha wananchi wa Shehia mbali mbali zilizomo katika Manispaa hiyo.

RC Ayoub ameleza kwamba pamoja na mafanikio yaliyofikiwa bado Manispaa hiyo inakabiliwa na changamoto ya vitendo vya udhalilishaji, jambo ambalo Mkoa wa Mjini Magharib wanaendelea kuchukua juhudi mbali mbali za kuthibiti uhalifu huo.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Magharib 'B' ndugu Ali Abdalla Natepe amesema katika kipindi cha nusu muhula wa awamu ya saba Manispaa hiyo ilijipangia kukusanya mapato kiasi cha shilingi bilioni 4,097,703,098 na kufanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 3,964,119,200 sawa na asilimia 90 ya makadirio.

Amesema jumla ya wakulima 72 wa kikundi cha mboga Mwanakwerekwe (ULEZI KAZI)  wamepatiwa mafunzo ya mboga mboga ikiwemo njia bora ya umwagiliaji wa taka.

Mkurugenzi huyo amesema jumla ya mikarafuu 7,000 imetolewa kwa wakulima wa sheria za Maungani, Kisauni, Kombeni pamoja  na Kibondeni.

Amebainisha kwamba jumla ya lita za maziwa 692,664,Mayai ya kuku trea 826,152 ,kuku wa nyama 714,120 na Mtindi glasi 48,712 zimezalishwa na kukusanywa.

Amebainisha kwamba katika sekta ya uvuvi jumla ya wavuvi 1,000 wamepatiwa mafunzo ya uvuvi endelevu, umuhimu wa mikoko kwa mazao ya baharini pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza Suleiman Amour Hassan Mkulima wa shehia ya Kisauni ambaye amenufaika na mfumo wa ugatuzi amesema ni miongoni mwa wakulima waliopatiwa mafunzo ya kilimo cha kisasa ambacho kimeinua hali za kiuchumi kwa zaidi ya wakulima 200 wa eneo hilo.

kwa upande wake Muhudumu wa Afya ya Jamii katika Kituo cha Afya ya Mama na Mtoto huko Maungani, ameeleza kuwa kabla ya kujengewa jengo la kisasa Manispaa ya Magharib 'B' walikuwa wakitoa huduma ya elimu ya afya chini ya muembe lakini kwa sasa wamepata Ofisi ya kudumu.

Dk.Mabodi ametembelea miradi mbali mbali iliyotekelezwa na ugatuzi na kutoa miongozi, ushauri na maelekezo ya kuimarisha utendaji wenye ufanisi katika miradi hiyo.

Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na Kituo cha Afya cha Kombeni, Kituo cha Afya ya Mama na Mtoto Maungani, Machinjio ya Kisakasaka, Kikundi cha wajasiriamali cha Ukweli njia Safi kilichopo Bweleo, Shamba darasa la Mboga mboga za aina mbali mbali Kisauni, Bweni la Wanafunzi wa skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki pamoja na Jengo la Kituo cha Kisasa cha Jeshi la Polisi katika maeneo ya Chukwani.

Kupitia ziara hiyo Dk. Mabodi akiwa ameambatana na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharib, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar Uongozi wa Mkoa wa Mjini na Magharibi Pamoja na Watendaji na viongozi wa Baraza la Manispaa ya Magharib 'B'.


Jumatano, 28 Novemba 2018

DK.MABODI AENDELEA NA ZIARA YAKE MANISPAA YA MAGHARIB 'A', AWAONYA WANAOBEZA JUHUDI ZA SMZ.


 NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.


 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akikagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Manispaa ya Magharibi 'A'   katika Skuli ya Msingi ya Kihinani.

 
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi (wa kwanza kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud na viongozi na watendaji wa Manispaa ya Magharib 'A'  wakikagua mashine ya kukausha dagaa inayomilikiwa na Kikundi cha ujasiriamali cha 'TUSIYUMBISHANE' kinachonufaika na fursa za ugatuzi.
 
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi  akikagua Kituo cha Afya cha Bumbwisudi kilichojengwa na wadau wa maendeleo wa Milele Foundation ambayo kipo katika Mfumo wa Ugatuzi.


 Daktari Dhamana wa Kituo cha Afya cha Bumbwisudi Said Fadhil Abbass, akieleza maendeleo yaliyofikiwa katika kituo hicho cha Afya Bumbwi sudi.
  
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi  akizungumza na watendaji na viongozi wa Baraza la Manispaa Magharib 'A'  kabla ya kutembelea miradi ya maendeleo. 

Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa hiyo, Ndugu Amour Ali Mussa akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Baraza la Manispaa hiyo. 

 BAADHI ya watendani, viongozi wa Manispaa pamoja ,Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharib pamoja na Mkoa wa Mjini Magharib wakifuatilia maelekezo ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Dk.Abdulla Juma Mabodi.

 MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar  Ndugu Amini Salmin Amour akichangia masuala mbali mbali ya uimarishaji wa Kiutendaji katika Manispaa ya Magharib 'A'


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi', amesema CCM inasimamia Sera zake ipasavyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii na kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa leo katika mwendelezo wa ziara yake kwa siku ya tatu ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Katika Baraza la Manispaa ya Magharibi 'A' Zanzibar.

Amesema CCM inaamini kwamba suala la maendeleo kwa jamii halina itikadi za kisiasa bali linatakiwa kutekelezwa kwa wananchi wote bila ya ubaguzi, hatua ambayo imefikiwa kwa kiasi kikubwa na mfumo wa ugatuzi wa madaraka katika Serikali za Mitaa.

Ameeleza kwamba fikra na dhana ya zanzibar kuwa 'Singapore' ya Bara la Afrika inaendelea kutekelezwa kwa vitendo na Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar inayoongozwa na CCM kupitia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Amesema sifa kuu ya viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi ni uadilifu, hekima, busara, ukweli, utu na uongozi bora katika kutatua kero za wananchi.

Kupitia ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo, Dk. Mabodi amewaonya baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani nchini kuacha tabia ya kupotosha umma kwa makusudi juu ya hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa na Serikali katika Sekta ya Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia na kueleza kuwa Sera hiyo ipo katika Ilani ya CCM na inaendelea kutekelezwa kwa kufuata matakwa ya kisheria.

" Kuna baadhi ya watu wanaojiita wanasiasa hapa Zanzibar wao kazi yao kubwa ni kuisubiri Serikali itekeleze jambo lolote la maendeleo, na wao waibuke na kukosoa na kubeza bila ya hoja za msingi ili waweze kupata siku za kuishi kisiasa.

Kwa hali hiyo nawambia kwamba hakuna wa kuzuia kasi ya CCM katika kuwaletea wananchi maendeleo tutaendelea kufanya mambo mbali mbali tunayoyaona yana tija kwa maslahi mapana kwa wananchi kwani CCM ndio Chama tawala tulioaminiwa na wananchi wakatupa ridhaa ya kuongoza dola.", amesema Dk.Mabodi.

Dk. Mabodi amesema CCM haina mzaha wala haiwezi kuyumbishwa na wanasiasa waliochoka na kufilisika kifikra na kisiasa, bali itaendelea kuwa imara na kutekeleza kwa kasi maendeleo ya wananchi.

Naibu Katibu Mkuu huyo, amesema kwa sasa wananchi wa maeneo mbali mbali hasa waliopo pembe zoni 'Vijijini' wananufaika sana na miradi mbali mbali ya kujikwamua kiuchumi kupitia mfumo wa ugatuzi hasa katika sekta za ufugaji,kilimo,uvuvi,afya,elimu na ujasiliamali.

Pamoja na hayo Dk. Mabodi ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM uliofanywa na Manispaa hiyo kupitia mfumo wa ugatuzi kwani umesaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi.

Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud ameeleza kwamba kupitia mfumo huo wa ugatuzi wataimarisha huduma bora za kijamii na kupunguza hatua kwa hatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi.

RC Ayoub ameweka bayana kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea kutoa ushirikiano wa kudumu katika kulinda na kutumia vizuri miradi mbali mbali inayotekelezwa na ugatuzi ili iwe endelevu katika kuwasaidia wananchi wengi kwa mujibu wa mahitaji yao ya msingi.

Naye Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa hiyo, Ndugu Amour Ali Mussa amesema Baraza hilo lililenga kukusanya shilingi bilioni 1,322,381,262 hadi kufikia Septemba 2018 na limefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 1,510,357,388 sawa na asilimia 114 ambapo wamevuka malengo 
yaliyokusudiwa.

Amesema wameendelea kupiga hatua kubwa katika Sekta zilizogatuliwa zikiwemo elimu, Afya na kilimo ambapo wananchi wa shehia mbali mbali zilizomo katika Baraza hilo wamenufaika na fursa zilizomo katika mfumo wa ugatuzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya watendaji  wanaohudumu katika mfumo wa ugatuzi ndani ya manispaa hiyo, pamoja na wananchi wanaonufaika na fursa zinazotokana na ugatuzi wamekiri kuwa utaratibu huo umeharakisha upatikanaji wa huduma bora za kijamii.

Alizungumza Daktari Dhamana wa Kituo cha Afya cha Bumbwisudi Said Fadhil Abbass, amesema toka kuanzishwa kwa mfumo huo huduma za Afya zimeimarika sambamba na upatikanaji wa dawa ni kwa asilimia 99 na asilimia moja inayobaki dawa zinanunuliwa na Manispaa ya Magharibi 'A'.

Ameitaja changamoto wanayokabiliana nayo ni upungufu wa wafanyakazi kwani wananchi wanaohitaji huduma wanakuwa wengi huku wafanyakazi wakiwa ni kidogo.

Naye Afisa Mifugo wa Wilaya Magharibi 'A', Ahmada Ramadhan Nassor amesema wametoa mafunzo ya ufugaji wa kisasa kwa wafugaji mbali mbali pamoja na kujenga kituo cha kisasa kitakachotumika katika matibabu mbali mbali ya mifugo.

Kwa upande wake Afisa Uvuvi Wilaya ya Magharib 'A' Khamis Bai amesema katika hatua za kuwawezesha wananchi ambao ni wajasiriamali wa biashara za kukausha na kuuza dagaa katika eneo la Bububu Kihinani wanaendelea kuwekewa mazingira rafiki ya kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Amesema kwa sasa wanatumia mashine ya kisasa ya kukaushia dagaa yenye thamani ya shilingi milioni 40 inayokausha ndoo tatu zenye kilo sitini kwa masaa matatu, ambapo bado wana mahitaji ya mashine nyingine kubwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Akizungumza Kaimu Mwalimu Mkuu wa skuli ya maandalizi ya Kihinani, Mwajuma Makame Issa amesema mfumo wa ugatuzi umesaidia kuimarisha miundombinu ya utoaji wa elimu, kwani kwa sasa wanapata kwa haraka vifaa mbali mbali vya kufundishia tofauti na utaratibu uliokuwepo zamani.

Ameitaja changamoto iliyopo katika Skuli hiyo kuwa ni wingi wa wanafunzi unaosababisha vyumba vya madarasa kuwa kidogo, ambapo darasa moja linachukuwa wastani wa wanafunzi 100 kiwango ambacho ni kikubwa.





Jumanne, 27 Novemba 2018

DK.MABODI AENDELEA NA ZIARA YAKE HALMASHAURI YA WILAYA YA KATI UNGUJA.

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.


 NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR DK.ABDULLA JUMA  SAADALLA AKIKAGUA MASHINE YA KUTENGENEA MAZIWA KATIKA KIKUNDI CHA WAJASRIAMALI CHA MPAPA WILAYA YA KATI UNGUJA KATIKA ZIARA YAKE.

 CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kitaendelea kufuatilia na kusimamia kwa  karibu utendaji wa Serikali za Mitaa ili zilete maendeleo endelevu kwa jamii. 
Ufafanuzi huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi ameutoa leo katika mwendelezo wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja, ameeleza kwamba Sera za CCM zimejielekeza katika kutatua kwa vitendo changamoto zinazowakabili wananchi wa Mijini na Vijiji. 
Amesema lengo la Serikali Kuu kupeleka madaraka ngazi za Serikali za mitaa kupitia mfumo wa ugatuzi imelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kijamii na zenye viwango.
Dk. Mabodi amewambia Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali kuwa wanatakiwa kutumia muda mwingi katika maeneo mbali mbali ya Kijamii kwa dhamira ya kuratibu na kutafuta njia bora za kutatua kero za wananchi.
Katika maelezo yake, Dk.Mabodi ameeleza kwamba CCM inafuata falsafa ya Uongozi Shirikishi na Jumuishi kwa lengo la kuzisimamia Serikali zitekeleze kwa ufanisi Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.
Naibu Katibu Mkuu huyo,  Dk. Mabodi amesema CCM haina muda wa kufanya siasa za marumbano,mihemuko na machafuko bali viongozi wake wanakesha usiku kucha wakibuni njia bora za kuzisimamia Serikali zake zifanye Mapinduzi ya kihistoria katika Nyanja za Kiuchumi, Kijamii ,Kisiasa na Kimaendeleo. 
Pia ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati kwa hatua kubwa waliyopiga katika kutekeleza miradi katika Sekta za Elimu, Kilimo Afya pamoja na ukusanyaji wa mapato kupitia mpango wa ugatuzi. 
Aidha amewataka wananchi maendeleo kuendelea kuamini na kuthamini, juhudi zinazofanywa na viongozi wakuu wa Serikali ambao ni Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM taifa Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwa maarifa na uadilifu wa kuweka mazingira salama ya ulinzi wa rasilimali za nchi huku wakidhibiti rushwa,ufisadi na matumizi mabaya ya mali za umma. 
Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM DK. Mabodi ametoa ahadi ya kuchangia shilingi milioni Moja kwa maskani ya CCM ya Kijibwe Mtu pamoja na kuchangia fedha za matengenezo ya Choo cha Skuli ya Maandalizi ya Kijiji hicho cha Kijibwe Mtu sambamba  kuchangia masuala mbali mbali ya miundombinu ya kijamii katika Wilaya hiyo ya Kati Unguja. 
Pamoja na hayo DK. Mabodi amempongeza Diwani wa Wadi ya Chwaka,Mlenge Hatib Mlenge kwa juhudi zake za kusimamia vizuri miradi  ya ujenzi wa miundombinu ya Skuli ya Msingi Chwaka pamoja na Skuli ya maandalizi ya 'Kiu' itakayohudumia wanafunzi wa Vijiji vya Kijundu na Uchuchuma.
Akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Said Mtaji Askari amesema Halmashauri imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ambayo ni  vipaumbele muhimu kwa jamii.
Alitoa Taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja ya utekelezaji wa Ilani ya CCM,Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mohamed Salum Mohamed  amesema makisio ya makusanyo ya fedha kwa mwaka 2018/2019 ni shilingi 800,000,000 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba mwaka 2018 wamekusanya shilingi 236,215,050 kutoka katika vyanzo tofauti vya mapato sawa na asilimia 29.
Amesema wamehamasisha wananchi kuunda vikundi vya ushirika vya uzalishaji mali na kuweka na kukopa sambamba na kukuvisajili vikundi 60.
Kwa upande wa fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo zinazoingia katika Halmashauri hiyo   wametoa vifaa vya ujenzi katika skuli Tisa za maandalizi na kutoa vifaa vya kusambazia maji katika shehia nane. 
Aidha amesema wameongeza idadi ya mabibi shamba na mabwana shamba pamoja na kutoa mafunzo ya kilimo bora kwa wakulima, pamoja na kuongeza idadi ya uzalishaji wa mpunga kutoka  0.7 hadi 1.6.
Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo, amezitaja changamoto zinazowakabili Halmashauri hiyo kuwa ni ukosefu wa maabara za Sayansi katika skuli mbali za Sekondari hali inayochangia wanafunzi wengi kutofaulu masomo ya Sayansi. 
Aidha ameitaja changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa madawati kwa skuli za maandalizi, msingi na Sekondari. 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Mashavu Sikwa akijibu hoja za baadhi ya washiriki katika ziara hiyo juu ya uwepo wa vitendo vya wizi wa mazao na Mifugo kwa baadhi ya maeneo,amesema njia pekee ya kudhibiti vitendo hivyo ni wananchi kushirikiana katika kufanya ulinzi shirikishi wa Polisi jamii. 
Akizungumzia  changamoto zinazowakabili wananchi wa Shehia ya Kijibwe Mtu, Diwani wa Wadi ya Bambi Rashid Abass Othman amesema wana ukosefu wa huduma ya umeme, maji safi na salama pamoja na huduma za Afya kuzifuata masafa ya mbali na Kijiji hicho. 
Mwenyekiti wa Wilaya ya Kati Unguja,Hassan Mrisho Vuai amewataka watendaji wa Halmashauri kuwa wabunifu zaidi katika kuitumikia jamii. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Mabodi amekagua miradi mbali mbali ikiwemo Vyuo Dunga Kiembeni, Skuli ya Maandalizi Chwaka, Ujenzi wa Skuli ya Kijundu, Utiaji wa umeme Skuli ya Jumbi,Ujenzi wa Choo Skuli ya Kikungwi pamoja na kutembelea Skuli ya maandalizi Kikungwi.
Miradi nyingine ni Skuli ya maandalizi Umbuji, Utiaji wa umeme kisima cha jamii Mitakawani, mradi wa kusanifu maziwa ya Ng'ombe na Mbuzi Mpapa pamoja na mradi wa umeme wa Nguvu za Jua kisima cha Maji cha Kijibwe Mtu. 

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU CCM Z'BAR DK.MABODI HALMASHAURI YA WILAYA YA KATI UNGUJA

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kati Unguja ndugu Hassan Mrisho Vuai (kulia) mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya ziara.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' (kushoto) akisalimiana na MNEC Amini Salmin Amour   mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya ziara.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' (kushoto) akisalimiana na MNEC Ramadhan Abdalla Shaaban.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' (kushoto) akisalimiana na  Mkurugenzi