Mhe. Waride B. Jabu, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi -CCM. ZANZIBAR akitoa Tamko la Chama Cha Mapinduzi, hapo katika Afisi Kuu za CCM Kisiwandui Zanzibar |
Chama Cha Mapinduzi Zanzibar: Kinaipongeza kwa dhati hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John P. Magufuli aliyoitowa jana Bungeni (Nov. 20, 2015), katika Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Moja(11). Kwani ni Hotuba ilyosheheni kila aina ya hekima na Busara za Hali ya juu. Aidha ni dira tosha ya maendeleo kwa maslahi ya jamii ya watu wa Watanzania.
Vile Chama Cha Mapinduzi kinatambua kuwa wananchi wa Zanzibar hasa wale wanaopenda Amani na Utulivu kwa mara nyengine wamepatwa na machungu makubwa juu kutokana na kitendo cha jana cha kuvunjiwa heshima kiongozi wao. Hata hivyo kwa niaba ya CCM, nchukua fursa hii kuwaomba kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu. Kwani Dawa ya Wapinzani iko njiani. kwa mara nyengine tena tunaiomba Tume ya Uchaguzi Zanzibar itangaze siku ya uchaguzi ili tufanye uchaguzi utakaokuwa wa huru na haki. Ni dhahiri, baada ya uchaguzi huo, CCM Zanzibar na Wananchi wa Zanzibar watalazimika kufanya maamuzi mengine ingawa yatakuwa magumu.
Aidha, CCM inawaambia Viongozi na wafuasi wa CUF kuwa suala la kuapishwa Maalim Seif Sharrif kuwa ni ndoto za mchana kwani Tume imeshatangaza kufutwa kwa Uchaguzi huo, na kinachofanywa na CUFni kuwadanganya wananchi tu na sio jengine