Jumatatu, 31 Desemba 2018

NAIBU KATIBU MKUU JUMUIYA YA WAZAZI NDG.OTHMAN AKABIDHIWA OFISI RASMI.



 NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya wazazi Zanzibar Mhe.Najma Giga akimkabidhi miongozo mbali mbali ya Jumuiya hiyo zikiwemo Kanuni ya fedha ya Chama na Jumuiya , Kanuni ya Wazazi, Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 na Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo jimpya la mwaka 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Ndugu Othman Ally Maulid.
 NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Ndugu Othman Ally Maulid akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ofisi rasmi katika hafla iliyofanyika leo katika Afisi Kuu ya Wazazi Kikwajuni Unguja.


 NAIBU Katibu Mkuu mtaafu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar  Mhe.Najma Giga akitoa nasaha kwa viongozi na watendaji wa Jumuiya hiyo.

 BAADHI ya Viongozi na Watendaji wa Jumuiya ya Wazazi wakifuatilia kwa makini nasaha mbali mbali zinazotolewa katika hafla hiyo ya makabidhiano.


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Ndugu Othman Ally Maulid amesema atasimamia kwa vitendo ibara ya Tano ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo jipya la mwaka 2017 inayoelekeza kuwa Ushindi wa CCM ni lazima kwa kila Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Chaguzi ndogo ndogo na Uchaguzi Mkuu.

Kauli hiyo ameitoa leo katika hafla ya makabidhiano ya Ofisi baina yake na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhe. Najma Giga huko katika Afisi ya Wazazi iliyopo Mpirani Kikwajuni Zanzibar.

Ndugu Othman amesema kwamba pamoja na majukumu mbali mbali ya kiutendaji yanayoikabili Jumuiya hiyo bado ana jukumu la msingi la kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Ameeleza kuwa kila Taasisi nchini ina malengo yake hivyo kwa upande wa CCM ambayo ni taasisi ya Kisiasa ni lazima iwekeze mipango yake katika kuhakikisha inashinda na kuendelea kuongoza wananchi kwa misingi ya uadilifu.

Katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo ameahidi kushirikiana na Watendaji, Viongozi na Wanachama wote wa Jumuiya na Chama kwa ujumla ili kuleta ufanisi wa kiutendaji ndani ya Jumuiya hiyo.

Aidha amewasisitiza viongozi na watendaji wa Jumuiya hiyo kuvitumia vyombo vya Habari nchini kutangaza miradi mbali mbali inayotekelezwa na Serikali chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Dkt.John Pombe Magufuli.

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo amesema atatumia miongozo mbali mbali ya CCM na Jumuiya ya Wazazi kubuni mipango mbali mbali ya maendeleo itakayosaidia kuleta ufanisi.

Naye Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Wazazi Najma Giga, amewashukru viongozi na watendaji wote wa jumuiya ya wazazi kwa ushirikiano waliompa wakati wote alipokuwa kiongozi wa Taasisi hiyo.

Aliwasisitiza Watendaji wa Taasisi hiyo kushirikiana vizuri na Naibu Katibu mpya ili kuendeleza mafanikio yaliyopo ndani ya Jumuiya hiyo.

Aidha ameeleza kuwa licha ya kumaliza muda wake wa kiuongozi ndani ya Jumuiya hiyo bado ataendelea kuwa karibu katika kushiriki masuala mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya hiyo.

Akitoa shukrani Mkuu wa Utawala msaidizi Ndugu Mustafa Rashid, amesema kwa niaba ya watendaji wenzake watafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Naibu Katibu Mkuu huyo ili kufikia malengo endelevu yaliyowekwa na jumuiya hiyo katika kuimarika kisiasa, kiuchumi na kijamii.

WANEC WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KAMISHENI YA UTALII Z'BAR.



 BAADHI ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakisoma machapisho mbali mbali yanayotolewa na Kamisheni ya Utalii hapo katika Kituo cha mawasiliano, Utafiti na Takwimu cha Kamisheni ya Utalii Zanzibar kilichopo  Uwanja wa Ndege wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Zanzibar.

 WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakipatiwa maelezo juu ya huduma zinazopatikana katika ukumbi wa mikutano wa Holeli Kimataifa ya Verde iliyopo Mtoni Marine Unguja, katika ziara yao ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 katika Kamisheni ya Utalii Zanzibar.

 WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakikagua boti na vifaa vya kisasa vilivyopo katika Hoteli ya Kimataifa ya Verde huko Mtoni Marine Zanzibar.

 MKURUGENZI Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt. Miraji Ussi akitoa maelezo ya ramani ya ujenzi wa mradi mkubwa wa miundombinu ya kisasa katika eneo la Makumbusho ya Kihistoria la Bihole lililopo Bungi Mkoa wa Kusini Unguja.
 WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakipatiwa maelezo juu ya Mradi wa Ufugaji wa Kasa uko Mnarani Nungwi, ambapo ni sehemu ya mradi unaoendeshwa na wananchi wakishirikiana na kamisheni ya Utalii Zanzibar.


NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

WAJUMBE  wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Zanzibar wamesema CCM itaendelea kuisimamia Serikali ikusanye kwa wingi mapato bila kuruhusu uvujaji wa rasilimali fedha.

Wamebainisha kuwa hatua hiyo itasaidia nchi kujitegemea na kuondokana na mfumo wa kutegemea baadhi ya fedha za wadau wa maendeleo zenye masharti yanayokwenda kinyume na Ustawi wa kijamii na Utamaduni wa wananchi wa Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya Wajumbe hao, Mjumbe wa NEC Ndugu Amini Salmin Amour huko katika Kituo cha ufugaji wa Kasa Mnarani Nungwi, ameeleza kwamba endapo Serikali itazidisha kasi ya usimamizi na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato Zanzibar itakuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi mkubwa.

Ndugu Amini ameeleza kwamba Sekta ya Utalii ni moja ya Taasisi muhimu zinazochangia kwa kiwango kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia fedha za kigeni.

Alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Sekta ya Utalii na maeneo ya Uwekezaji kwa lengo la kushauri na kutoa maelekezo kwa baadhi ya sehemu zenye changamoto za kiutendaji.

Aliipongeza Kamisheni ya Utalii Zanzibar kwa utendaji wao mzuri uliochangia kuimarika kwa taasisi hiyo na kufanikiwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa Ilani ya CCM.

Pamoja na hayo aliwasihi wananchi kuendeleza Utamaduni wa kufanya Utalii wa ndani ili wajionee vivutio mbali mbali vya utalii vilivyopo nchini pamoja na kufahamu historia na hatua za kimaendeleo zilizofikiwa kupitia Sekta ya Utalii nchini.

Pamoja na hayo aliwapongeza Marais wote wawili ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kudhibiti vitendo vya ubadhilifu wa mali za umma huku wakibuni na kutekeleza mikakati ya ukuaji wa Uchumi wa nchi.

Naye Kamishna wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar  Mhe. Khamis Mbeto amesema kamisheni hiyo kwa sasa tayari imevuka malengo ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM iliyoelekeza kuwa ifikapo mwaka 2020 Zanzibar itakuwa na Watalii 500,000 ambapi kwa sasa tayari idadi ya Watalii inakaribia kufikia 600,000 kabla ya mwaka 2020.

Ameeleza kuwa lengo la Kamisheni hiyo ni kutengeneza mazingira rafiki ya kukarabati baadhi ya miundombinu iliyopo katika Vivutio vya Utalii nchini ili wageni na wenyeji mbali mbali wanaotembelea maeneo hayo wawe mabalozi wazuri wa kuendelea kutangaza vivutio hivyo kwa wananchi wengine.

Akieleza mikakati mbali mbali ya kiutendaji inayotekelezwa na Kamisheni hiyo, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt.Abdallah Mohamed Juma amesema kamisheni hiyo inashirikiana vizuri na taasisi za kimataifa zinazoshughulikia masuala ya Utalii ili kupata mbinu za kisasa zitakazoleta ufanisi wa kimaendeleo ndani ya sekta hiyo.

Aliitaja miongoni mwa mikakati hiyo ni uwepo wa Vituo maalum vya Matangazo na Uratibu wa takwimu na taarifa za masuala mbali mbali ya Utalii katika Viwanja vya Ndege pamoja na Bandari Kuu ya Zanzibar Malindi pamoja na Vituo vidogo vidogo katika maeneo mbali mbali nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni hiyo, Dkt. Miraji Ussi, alieleza kuwa kamisheni hiyo inafanya ukarabati mkubwa katika Vivutio mbali mbali vilivyopo nchini hasa katika eneo la Kihistoria linalolojulikana kama Bihole lililopo katika Kijiji cha Bungi katika Mkoa wa Kusini Unguja ili wananchi wa maeneo hayo na maeneo mengine wapate sehemu nzuri ya kutembelea na kufanya shughuli za kibiashara.

Dkt. Miraji alifafanua kwamba mpaka sasa tayari wamekamilisha ramani ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa kama Soko la ujasiriamali,hoteli na bustani ya kisasa na eneo maalum michezo ya watoto na makumbusho ambayo itakarabatiwa kwa kufuata vigezo vya awali vya eneo.

Wajumbe hao walitembelea maeneo mbali mbali yakiwemo eneo la Uwekezaji wa Hoteli ya Kisasa ya Verde, Uwanja wa Ndege wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,Bandari Kuu ya Zanzibar, Eneo la Kihistoria la Bihole pamoja na Kituo cha kufuga Kasa kilichopo Nungwi katika Mkoa.

Jumamosi, 29 Desemba 2018

UVCCM YAANZA KUJINOA KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 55 YA MAPINDUZI.

 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa (wa pili kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndugu Latifa Khamis Juakali(wa kwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Idrissa Kitwana( wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Ndugu Kamaria Suleiman Nassor wakionyesha uwezo wao katika fani ya mazoezi ya viungo vya mwili.
(PICHA NA IS-HAKA OMAR-AFISI KUU YA CCM ZANZIBAR)

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) leo imefanya matembezi ya kuenzi miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yaliyoanzia Amaani na kuishia Viwanja vya Maisara Unguja.

Matembezi hayo yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Idrissa Kitwana yameudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali.

Maelfu ya Vijana wa UVCCM wameshiriki katika matembezi hayo huku wakionyesha uhodari na ukakamavu wao uliopambwa na nyimbo mbali mbali za kizalendo hasa zile zenye maudhui ya kuwaenzi Waasisi wa Mapinduzi Matukufu ya January 12,1964.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar zimeeleza kuwa matembezi hayo ni sehemu ya mazoezi ya kuweka sawa viungo vya mwili ikiwa ni maandalizi ya Matembezi Makubwa yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni Kisiwani Pemba.


MATUKIO KATIKA PICHA MATEMBEZI YA UVCCM Z'BAR KUENZI MIAKA 55 YA MAPINDUZI.
















Jumamosi, 22 Desemba 2018

NAIBU KATIBU MKUU WA UVCCM ZANZIBAR NDG.MUSSA HAJI MUSSA AWAUHUTUBIA VIJANA WA UVCCM .

NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Mussa Haji Mussa akiwahutubia vijana wa UVCCM Zanzibar katika hafla ya mapokezi yake.


NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) anayefanyia kazi zake Zanzibar  Ndugu Mussa Ali Mussa leo amewasili nchini kwa mara ya kwanza toka ateuliwe kushika nafasi hiyo ya uongozi ndani ya Taasisi hiyo.

Mara baada ya kuwasili Zanzibar Naibu huyo amepokelewa na viongozi wandamizi wa Jumuiya hiyo pamoja na Familia yake kwa shangwe na furaha kubwa, huku wakimpa maneno ya kumtia ari na hamasa ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Hafla ya mapokezi hayo imefanyika katika Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar katika Uwanja wa Gymkhana Kikwajuni ambapo kiongozi huyo amezungumza na viongozi,watendaji na wanachama wa ngazi mbali mbali za Taasisi hiyo ya Vijana.

Ndugu Mussa akiwahutubia wanachama hao amesema ataendeleza mambo mema ya kuleta maendeleo endelevu ndani ya Jumuiya na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla, huku akisisitiza kuwa atashirikiana na viongozi wenzake wa jumuia kwa ngazi zote.

MATUKIO KATIKA PICHA MAPOKEZI YA NAIBU KATIBU MKUU WA UVCCM Z'BAR NDG.MUSSA HAJI MUSSA YALIYOFANYIKA GYMKHANA.

 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akiwahutubia Vijana wa UVCCM katika hafla ya Mapokezi yake iliyofanyika leo katika Viwanja vya Gymkana unguja.

 VIONGOZI mbali mbali wa UVCCM wakiwa katika hafla ya mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu wa Vijana Mussa Haji Mussa.

 
VIONGOZI mbali mbali wa UVCCM wakiwa katika hafla ya mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu wa Vijana Mussa Haji Mussa.


 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akishuka Boti Bandarini Malindi  mara baada ya kuwasili nchini.


 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akisalimiana na Afisa mwandamizi wa UVCCM Afisi Kuu Zanzibar Ndugu Iddi mara baada ya kuwasili nchini.

 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akiwa na viongozi mbali mbali wa UVCCM mara baada ya kuwasili nchini.
 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akibadilishana mawazo na uzoefu na mmoja wa viongozi.
 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akizungumza na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Mjini Ndugu Kamaria Suleiman Nassor.


 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akipewa zawadi.

NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akivishwa mashada ya maua ikiwa ni ishara ya mapokezi. 

 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wandamizi wa UVCCM Zanzibar.

Akisalimiana na Mama yake Mzazi mara baada ya kuwasili nchini.

 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akiwa katika Picha ya Pamoja na Familia yake.

MATUKIO KATIKA PICHA MAPOKEZI YA NAIBU KATIBU MKUU WAZAZI NDG.OTHMAN ALLY ALIPOWASILI ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Othman Ally Maulid akisalimiana na Viongozi wa Chama na Jumuiya hiyo mara baada ya kuwasili Zanzibar kwa mara ya kwanza toka alipoteuliwa.

  NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Othman Ally Maulid akiwa na Viongozi wandamizi wa Jumuiya hiyo mara baada ya mapokezi yake.

  NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Othman Ally Maulid akiwapungia mkono viongozi na watendaji wa jumuiya hiyo mara baada ya kufika katika viwanja vya Afisi Kuu ya Wazazi iliyopo Mpirani Kikwajuni Zanzibar.

 MSAFARA wa Naibu  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Othman Ally Maulid ukiwasili Kisiwandui kwa ajili ya kujitambulisha kwa viongozi, watendaji na Wanachama wa CCM na Jumuiya hiyo.


NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Othman Ally Maulid akivishwa koja na vijana wa chipukizi.



NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Othman Ally Maulid akielekea katika kaburi la Mwasisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambaye pia alikuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Hayati Marehemu Mzee Abeid Aman Karume.



 NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Othman Ally Maulid pamoja na viongozi wengine wakisoma Dua katika kaburi la Marehemu Mzee Karume.



 NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Othman Ally Maulid akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.


  NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Othman Ally Maulid pamoja na viongozi wengine wakiwapungia mkono wanachama wa CCM.

 NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Othman Ally Maulid akieleza namna atakavyotumia Katiba ya CCM na Kanuni ya Wazazi kuiongoza Jumuiya hiyo kwa ufanisi.

 BAADHI ya Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi wakisikiliza hotuba na nasaha za mgeni rasmi katika hafla hiyo.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza katika hafla hiyo.


 NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya hiyo Ndugu Najma Giga akieleza namna alivyoongoza Jumuiya hiyo kwa mafanikio na kuhakikisha anaiacha katika Mikono Salama.