UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) leo imefanya matembezi ya kuenzi miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yaliyoanzia Amaani na kuishia Viwanja vya Maisara Unguja.
Matembezi hayo yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Idrissa Kitwana yameudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali.
Maelfu ya Vijana wa UVCCM wameshiriki katika matembezi hayo huku wakionyesha uhodari na ukakamavu wao uliopambwa na nyimbo mbali mbali za kizalendo hasa zile zenye maudhui ya kuwaenzi Waasisi wa Mapinduzi Matukufu ya January 12,1964.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar zimeeleza kuwa matembezi hayo ni sehemu ya mazoezi ya kuweka sawa viungo vya mwili ikiwa ni maandalizi ya Matembezi Makubwa yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni Kisiwani Pemba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni