Jumanne, 28 Mei 2019

CCM WILAYA YA KUSINI UNGUJA YAKAGUA VITUO VYA AFYA MAKUNDUCHI.

  MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Abdulaziz Hamad Ibrahim(wa Tatu kushoto) akizungumza na Uongozi wa Kituo cha Afya cha Kajengwa katika ziara ya Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo ya Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Vituo vya Afya vilivyopo katika Jimbo la Makunduchi.

 Katibu wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Ndg. Hafidh Hamad Mkadam(wa kwanza  kushoto aliyesimama) akifafanua lengo la ziara hiyo kuwa ni ya Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kusini Unguja wakiongozwa na  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Abdulaziz Hamad Ibrahim akikagua  Ujenzi wa Nyumba ya Madaktari katika Hosapitali ya Kajengwa. 

 MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Abdulaziz Hamad Ibrahim akiwa na Kamati ya Siasa wakikagua Sehemu ya Kuchomea Takataka (Kinu Moshi) za Kituo cha Afya Kibuteni katika ziara hiyo ya kukagua Utekelezaji wa Ilani.

 KAMATI ya Siasa Wilaya ya Kusini Unguja wakipatiwa maelezo kutoka kwa Uongozi wa Kituo cha Afya cha Kizimkazi Mkunguni.

 BAADHI ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kusini Unguja wakisikiliza kwa makini maelezo  Afisa Utabibu Kituo cha Afya Mtende.


 KAMATI ya Siasa Wilaya ya Kusini Unguja wakikagua Shimo la Kuchomea Taka za Kituo cha Afya cha Kizimkazi Mkunguni linalohitaji matengenezo ya kujengewa kutokana na kuwa wazi.



MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Abdulaziz Hamad Ibrahim, ameitaka Halmashauri ya Wilaya hiyo kutatua Changamoto zinazovikabili Vituo vya Afya katika Jimbo la Makunduchi ili kwenda sambamba na Matakwa ya Ugatuzi  katika Sekta ya Afya Nchi.

Maelekezo hayo ameyatoa leo katika Ziara ya Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2015/2020 katika Vituo vya Afya Vilivyomo ndani ya Jimbo la Makunduchi Unguja.

Amesema Serikali imefikia uamuzi wa kufanya Ugatuzi katika Sekta ya Afya kwa kuzipatia Mamlaka ya usimamizi Halmashauri za Wilaya kwa lengo la kuimarisha Huduma za Afya ili Wananchi wapate huduma bora na kwa wakati mwafaka.

Mwenyekiti huyo ameipongeza Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kuimarisha upatikanaji wa Vifaa Tiba na huduma mbali mbali za msingi za Afya licha ya kuwepo kwa baadhi ya Vituo vinavyokabiliwa na Changamoto ya Miundombinu Duni ya Majengo hali inayosababisha usumbufu kwa Wananchi na Watumishi wa Afya.

Abdulaziz ameusisitiza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kufanya ziara za mara kwa mara katika Vituo vya Afya kwa lengo la kuratibu changamoto zinazovikabili Vituo hivyo na kuzitatua  ili viendelee kutoa Huduma Bora za Afya.

Katika maelezo yake Mwenyekiti huyo kwa niaba ya Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, amemshukru  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa kusimamia ipasavyo Mfumo wa Utoaji wa Huduma za Afya Bure kwa Wananchi.

"Tumetembelea Vituo vya Afya mbali mbali vilivyopo katika Jimbo la Makunduchi na kujionea namna vinavyotoa Huduma za Afya kwa Wananchi lakini pia tumebaini uwepo wa Changamoto ndogo ndogo na tumetoa maelekezo kwa wahusika zitatuliwe kabla ya Mwaka 2020."amesema Mwenyekiti huyo wa CCM Abdulaziz.

Aidha amesema Chama Cha Mapinduzi Wilayani humo kitaendea kuisimamia Serikali itekeleze kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi hasa katika masusla ya utoaji wa Huduma za Afya ili kila Mwananchi apate fursa hiyo bila vikwazo.

Wakizungumza kwa Wakati tofauti Maafisa Utabibu wa Vituo vya Afya katika Jimbo hilo wameipongeza Serikali Kuu kwa kufanya Ugatuzi ambao  umeongeza upatikanaji wa Huduma Bora za Afya kwa Wananchi wa Vijijini.

Maafisa hao walizitaja Changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na Uchakavu wa Majengo ya Vituo, Ukosefu wa Uzio, Ukosefu wa Huduma za Usafiri kwa Watumishi wanaoishi mbali na Vituo hivyo, ukosefu wa Walinzi kwa baadhi ya Vituo pamoja na upungufu wa Watumishi kwa baadhi ya Vituo.

Ziara hiyo imefanyika katika Vituo vya Afya vya Mtende,Kibuteni,Kizimkazi Mkunguni, Kizimkazi Dimbani pamoja na Muyuni.















































































































































Jumapili, 26 Mei 2019

DK.MABODI AONGOZA MAELFU YA WANANCHI MAZISHI YA MWENYEKITI MROPE -MAY 26,2019.


 VIJANA Maalum wa UVCCM wakiwa na Jeneza la aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Amani, Marehemu Abdi Ali Mzee 'Mrope'  kwa ajili ya Mazishi yake huko Kijijini kwao Jumbi Unguja.

 WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Wananchi mbali mbali wakiwa katika Mazishi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Amani, Marehemu Abdi Ali Mzee 'Mrope'  kwa ajili ya Mazishi yake huko Kijijini kwao Jumbi Unguja.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akiweka udongo katika Kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Amani Marehemu Abdi Ali Mzee huko Jumbi.

Katibu wa UVCCM Wilaya ya Amani Ndugu Mohamed Ali Mohamed,akisoma Wasifu wa Marehemu mara baada ya Mazishi yaliyofanyika Kijijini Kwao Jumbi. 


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi, leo ameongoza Maelfu ya Wananchi katika Mazishi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Amani Unguja Marehemu Abdi Ali Mzee ‘Mrope’ aliyefariki Jana akiwa katika Matibabu huko Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es saalam na amezikwa leo kijijini kwao Jumbi Mkoa wa Kusini Unguja.
Viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wameshiriki Mazishi hayo wakiwemo Katibu wa NEC,Idara ya Organazasheni Makao Makuu Ndugu Pereira Ame Silima,Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Mwl.Kombo Hassan Juma pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid.
Wengine ni  Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Wabunge na Wawakilishi,Wakurugenzi wa Idara mbali mbali za SMZ,Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa ngazi mbali mbali, Wana CCM na Wananchi kwa ujumla.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Amani Ndugu Mohamed Ali Mohamed,akisoma Wasifu wa Marehemu huyo amesema CCM na Jumuiya zake wamepokea kwa Huzuni na Masikitiko Taarifa ya Kifo cha Mwenyekiti huyo wa CCM Wilaya ya Amani Unguja.
Amesema Mwenyekiti Abdi Ali Mzee alizaliwa mwaka 1964 katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na kupata Elimu yake ya Msingi kuanzia mwaka 1978 katika Skuli ya Msingi Kidongo Chekundu pamoja na Elimu ya Sekondari katika Skuli ya Shangani mwaka 1981.
Amesema mwaka 1984 Abdi alijiunga na Chuo cha Ufundi wa Chuma huko Chang’ombe Dar es saalam na kuhitimu mafunzo hayo na akajiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi Mwaka 1983 katika Tawi la CCM Sogea.
Katika maelezo yake Katibu huyo, ameeleza kuwa Marehemu Enzi za Uhai wake alishika nyadhifa mbali mbali za Uongozi katika Chama Mwaka 1992 hadi 2007 alikuwa Balozi  wa Nyumba 10 Shina namba 7 katika Tawi la CCM Sogea,Mwaka 1997 hadi 2007 alikuwa Mwenyekiti wa CCM Tawi la Sogea,Mwaka 2007 hadi Mwaka 2012 alikuwa ni Mwenyekiti wa Jimbo la Magombeni.
Amesema Mnamo Mwaka  2012 hadi 2019 alikukuwa ndiye Mwenyekiti wa CCM wa mwanzo wa Wilaya ya Amani toka ilipoanzishwa na pia alikuwa Mkufunzi wa Makada katika Chuo cha Itikadi cha CCM Zanzibar na Mjumbe wa Bodi ya kudhibiti Kodi za Nyumba  Zanzibar.
Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo licha ya kuwa Mwanasiasa pia alikuwa ni Mwanamichezo Mstaafu wa Mpira wa Miguu aliyewahi kuchezea Timu za African Kids,Wazee Sports Club hadi umauti unamkuta alikuwa ni Mwalimu wa Timu ya New Boko kutoka Mtaa wa Boko Zanzibar.
Sambamba na hayo Chama Cha Mapinduzi Taifa kupitia Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wanatoa Salamu za Pole kwa Wafiwa na Watu wote walioguswa na Msiba huo na kuwaomba waendelee kuwa na subra katika kipindi hiki cha Maombolezo.
Marehemu ameacha Vizuka Wawili na Watoto Saba.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amin.
  
 
 

Jumamosi, 25 Mei 2019

VIONGOZI WA WADI HADI WILAYA ZA UWT MKOA WA MAGHARIB WAPEWA MAFUNZO.

 
 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao(wa Pili kushoto anayezungumza) akitoa Mada ya Wanawake na Uongozi katika Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Viongozi wa UWT Ngazi za Wadi hadi Wilaya za UWT Mkoa wa Magharibi Unguja huko katika Ukumbi wa UWT Wilaya ya Dimani Kiembesamaki.
 BAADHI ya Viongozi wa UWT wa Ngazi za Wadi hadi Wilaya wakifuatilia kwa makini Mafunzo hayo ya Siku Moja ya kuwajengea uwezo juu ya masuala mbali mbali ya Uongozi na Siasa.



VIONGOZI wa Ngazi mbali mbali za Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Tanzania Mkoa wa Magharibi wametakiwa kueleza Changamoto zinazowakabili Wanachama wa CCM ili zitafutiwe ufumbuzi wa kudumu.

Rai hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao wakati akitoa Mada ya  Wanawake na Uongozi wakati akifungua Mafunzo ya kuwajengea Uwezo  Viongozi wa UWT ngazi za Wadi hadi Wilaya za UWT Mkoa wa Magharibi Unguja.

Ndugu Catherine amesema baadhi ya Viongozi wa Kamati hizo hawasemi changamoto zilizopo katika maeneo wanayoyaongoza hali inayosababisha kukwama kwa baadhi ya majukumu ya Kiutendaji.

Amesisitiza suala la ushirikiano katika masuala ya kiutendaji ili kazi mbali mbali za UWT ziweze kwenda sambamba na matakwa ya Katiba na Kanuzi za Umoja huo na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla.

Katika maelezo yake Bi.Catherine amewasihi  Viongozi hao kutojihusisha na masuala ya makundi yasiyofaa ya kusaka Wagombea Urais,Ubunge,Uwakilishi na Udiwani kabla ya muda uliopangwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2017,  pamoja na miongozo na Kanuni mbali mbali za Chama.

Amesema kazi kubwa iliyopo mbele ya Umoja huo kwa sasa ni kujipanga vizuri kwa  kuongeza Wanachama wapya ndani ya CCM ambao ndio Mtaji madhubuti wa Kisiasa utakaoweza kufanikisha Ushindi wa CCM mwaka 2020.

Kupitia Mafunzo hayo amesema mwaka 2019 ni muda wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa Tanzania Bara ambao utakuwa ni kipimo halisi cha maandalizi ya Ushindi wa 2020 ,hivyo kila Kiongozi wa Umoja huo ajipange kuwamasisha Wanawake wajitokeze kwa wingi wakati utakapofika kuwania nafasi za Uongozi na kuhakikisha Wagombea wa CCM wanashinda.

Naye Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi Zainab Ali Maulid amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuwakumbusha Viongozi hao Majukumu yao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Dola Mwaka Ujao.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Viti Maalum kupitia Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar  Mhe.Amina Idd Mabrouk amesema Mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuwajengea Uwezo wa Kisiasa na kuwaunganisha pamoja ili wanufaike na fursa za zilizopo za Kijamii na Kichumi.

Amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuwaamini Wanawake kwa kuwateuwa katika nafasi mbali mbali za Uongozi ambazo wamekuwa wakizitendea haki kwa kutekeleza majukumu wanayopewa kwa ufanisi.

Mafunzo hayo elekezi ya siku moja kwa Viongozi wa UWT kuanzia ngazi za Wadi hadi Wilaya za Umoja huo yameandaliwa na Wawakilishi na Wabunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Magharibi Unguja.


Ijumaa, 17 Mei 2019

MHE.BALOZI SEIF ALI IDD AONGOZA MAZISHI YA MNEC MAREHEMU RAMADHAN ABDALLA SHAABAN.

VIJANA Maalum wa UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa wamebeba Jeneza la aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Marehemu Ramadhan Abdallah  Shaaban kwa ajili ya Mazishi yake yaliyoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Idd yaliyofanyika leo Kijijini kwako Uzini Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. 

MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiongoza mazishi kwa kuweka udongo katika Kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Marehemu Ramadhan Abdallah Shaaban aliyefariki jana akiwa katika Matibabu katika Hospitali ya Agakhan Jijini Dar es saalam.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akiweka udongo katika Kaburi la Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Marehemu Ramadhan AbdallaH Shaaban aliyefariki jana akiwa katika Matibabu katika Hospitali ya Agakhan Jijini Dar es saalam.

 ALIYEKUWA Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Marehemu Ramadhan Abdallah Shaaban Enzi za Uhai wake.


MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, leo ameongoza Maelfu ya Wananchi katika Mazishi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Marehemu Ramadhan Abdallah Shaaban aliyefariki jana May 16,2019  akiwa katika Matibabu Hospitali ya Agakhan  Jijini Dar es saalam na amezikwa leo kijijini kwao Uzini Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Mazishi hayo yameudhuriwa na Viongozi na Watendaji mbali mbali wa CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamy wa Pili wa Rais Aboud Mohamed Aboud.

Viongozi wengine ni  Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Wabunge na Wawakilishi,Wakurugenzi wa Idara mbali mbali za SMZ,Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa ngazi mbali mbali pamoja na Wana CCM na Wananchi.

Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Mzee Suleiman, akisoma wasifu wa marehemu  amesema CCM imepokea kwa mshtuko na huzuni  mkubwa taarifa ya Kifo cha Ramadhan Abdallah Shaaban ambaye alikuwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Kusini Unguja na Mkurugenzo wa Uratibu wa Uchaguzi Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

Amesema Marehemu Ramadhan Abdalla Shaaban alizaliwa mwaka 1948 katika Mkoa wa Kusini Unguja Wilaya ya Kati katika Kijiji cha Uzini na kupata Elimu yake ya Msingi kuanzia mwaka 1964 hadi 1967 katika Skuli ya Msingi Ndijani Wilayani humo.

Pia alieleza kwamba Marehemu aliendelea na Elimu yake ya Sekondari katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba mwaka 1968 hadi 1976 alipomaliza Kidato cha Nne na kujiunga na Chuo cha Ualimu cha Nkuruma na kuhitimu Diploma ya Ualimu, na kujiendeleza kielimu katika Vyuo Vikuu mbali mbali vya ndani na nje ya Nchi.

Kupitia risala hiyo imeeleza kuwa Marehemu enzi za uhai wake alikuwa Mwanachama na Kiongozi Mtiifu wa kuaminika lakini pia alikuwa Mshauri ,Mkufunzi na mpiganaji na kamanda mzuri aliyelinda maslahi ya CCM na Muumini mzuri wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Katika maelezo yake Katibu huyo, ameeleza kuwa Marehemu Enzi za Uhai wake aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali katika Chama na Serikali ambapo alikuwa ni miongoni mwa Makada Watiifu wa Afro-Shirazi Party Yourth Legue na Mwanachama wa ASP.

Alisema mwaka 1977 alikuwa ni Balozi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Tawi la Uzini, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kati na mwaka 1980 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na kuwa Waziri wa Biashara Zanzibar.

Nyadhifa nyingine alizowahi kushika Marehemu Ramadhan enzi za uhai wake mwaka 1980 hadi 1985 alikuwa Mbunge na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1988 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la JUWATA Tanzania.

Mnamo mwaka 2005 hadi 2015 tena kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri katika Wizara mbali mbali za SMZ zikiwemo Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba,Maji na Nishati na hadi kifo chake alikuwa Mjumbe wa NEC CCM Taifa na Mkurugenzi wa Uratibu wa Uchaguzi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

Sambamba na hayo Katibu huyo alieleza kuwa Marehemu Ramadhan ataendelea kukumbukwa kwa Mchango wake Mkubwa katika uhai wake ndani ya CCM na Serikali zote mbili ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Fikra zake zitaenziwa kwa Vitendo katika mapambano ya Siasa za Ujamaa na Kujitegemea.

Marehemu ameacha Vizuka wawili na Watoto Tisa.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala Pema Peponi Amin.

Alhamisi, 9 Mei 2019

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA MLEZI WA CCM RUVUMA MKOA WA RUVUMA DK.ABDULLA JUMA MABODI. 06/05/2019.


 MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya ziara yake ya kuimarisha Chama katika Wilaya za CCM Mkoani humo.

 MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi akivishwa Sikafu na Kijana wa UVCCM mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Ruvuma. 

  MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Kuruthum Mhagama mara baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Mkoa wa Ruvuma.

  MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi akiangalia Kikundi cha Sanaa cha Jakaya Kata ya Lizaboni Wilaya ya Songea Mjini.

  MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Mkoa na Wilaya ya Songea Mjini na Songea Vijijini baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Mkoa wa Ruvuma.
 MWENYEKITI wa Shina no.17 Tawi la CCM Namtumbo  'A' Wilaya ya Namtumbo mbele akifungua Kikao Cha Mkutano wa ndani mbele ya Mgeni rasmi  Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi alipowasili katika eneo hilo.


 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Killian Mwisho akizungumza na Wana CCM wa Shina no.17 katika ziara ya Mlezi wa CCM wa Mkoa huo.

  MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza na Wana CCM wa Tawi hilo la Namtumbo 'A' katika Ziara yake ya kikazi ya  kuimarisha Chama Cha Mapinduzi Wilayani Namtumbo.

 MZEE wa CCM katika Shina hilo namba 17  Mzee Awabu Kilambo,akitoa Shukrani kwa Mgeni rasmi na kuahidi kuwa Wananchi wa Eneo hilo Wataendelea kuamini na kuunga mkono Chama Cha Mapinduzi.

  MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwa na Wana CCM wa Shina no.17 katika ziara yake Wilayani Namtumbo.

   MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi .

   MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwa na Wajumbe mbali mbali wa CCM wakikagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.

   MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwa na Wajumbe mbali mbali wa CCM wakikagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.

   MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwa na Wajumbe mbali mbali wa CCM akisikiliza Taarifa ya Mradi wa Maji Safi na Salama katika Mradi wa Maji  Mto Rwinga.
   MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akisikiliza Taarifa ya Mradi wa Ujeni wa Soko la Wilaya ya Namtumbo.

 WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Namtumbo, Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Namtumbo na  Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Namtumbo wakisikiliza nasaha za   Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa  (hayupo pichani) katika ziara yake Wilayani humo.

   MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi  akizungumza na  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Namtumbo, Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Namtumbo na  Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Namtumbo

 BAADHI ya Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Namtumbo wakisikiliza nasaha za Mgeni rasmi  Mlezi  wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi.

Jumamosi, 4 Mei 2019

MATUKIO KATIKA HAFLA YA KARAMU YA TAWI LA CCM FUONI MICHENZANI.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akikaribishwa  na  Vijana wa Chipukizi Tawi la CCM Fuoni Michenzani,mara baada ya kuwasili katika Tawi hilo kwa ajili ya hafla ya Karamu. 

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akivishwa sikafu na Vijana wa Chipukizi Tawi la CCM Fuoni Michenzani. 

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Mohamed Rajab Soud.

 VIONGOZI na Wanachama wa CCM walioudhuria katika hafla hiyo ya Karamu ya Wana CCM wa Tawi la CCM Fuoni Michenzani.

Wanachama wa CCM walioudhuria katika hafla hiyo ya Karamu ya Wana CCM wa Tawi la CCM Fuoni Michenzani.

 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Magharib Mohamed Rajab akizungumza katika hafla hiyo.

 MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Dimani Hussein Ali Mjema akizungumza katika hafla hiyo.

MWENYEKITI wa Tawi la CCM Fuoni Michenzani akizungumza na kufungua Mkutano huo wa ndani ulioambatana na hafla ya Karamu.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizunfumza katika hafla hiyo


 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akisalimiana na Wanachama.




MSHAURI wa Rais wa Zanzibar  wa masuala ya Utamaduni na Utalii Mhe.Chimbeni Kheri Chimbeni. akitoa shukrani.