Jumamosi, 4 Mei 2019

DK.MABODI-ATAJA SIRI YA MAFANIKIO YA ZANZIBAR.


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla akizungumza na Wana CCM wa Tawi la CCM Fuoni Michenzani akimwakilisha  Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein   katika hafla ya Karamu ambayo ni ahadi iliyotekelewa na Dk.Shein.

  WANACHAMA na Viongozi mbali mbali wa Tawi la CCM Fuoni Michenzani wakila Karamu iliyoandaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.



 WANACHAMA wa CCM Fuoni Michenzani wakisikiliza nasaha za Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi.



NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’amesema Maendeleo yanayopatikana Nchini katika Nyanja za Kiuchumi,Kisiasa na Kijamii yanatokana na uwepo wa Amani na Utulivu inayosimamiwa kwa ufanisi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

Hayo aliyasema leo wakati akimwakilisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika Hafla ya Karamu  huko Tawi la CCM la Fuoni Michenzani Unguja.

Dk.Mabodi amesema kuimarika kwa Sekta mbali mbali zikiwemo za Elimu, Afya, Kilimo, Utawala, Haki za Binadamu, Ustawi wa Jamii, Miundombinu ya Anga, Nchi kavu na Baharini yote hayo ni vielelezo tosha vya utendaji bora na uliotukuka unaoacha Alama nzuri  kwa Vizazi vya sasa na vijavyo uliotekelezwa na Dk.Shein katika Utawala wake wa Awamu ya Saba.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi amesema Dk.Shein ametekeleza mambo mengi yaliyoandika Historia ya kipekee Duniani ikiwemo Penchini ya Shilingi 20,000 kwa Wazee wenye Umri wa Miaka 70,Afya bure na Elimu bure mambo ambayo Mataifa mengi Duniani wameshindwa kuyatekeleza kwa Wananchi wao.

Ameeleza kuwa Dk.Shein amesimamia na kulinda Amani ya Nchi isitoweke na kuhakikisha Wananchi wanaishi kwa upendo, huku wakiwa na Uhuru wa kweli wa kufanya kazi halali za kuingia kipato sehemu yoyote ndani na nje ya Zanzibar bila vikwazo.

Amesema Mafanikio hayo hayakuja kama ndoto potofu  bali yametoka na Sera imara za CCM chini ya Ilani yake ya mwaka 2015/2020 inayotekelewa kwa kasi kubwa kwa lengo la kumaliza changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi katika maeneo yao kabla ya mwaka 2020.

Amewasihi Wananchi Visiwani humo bila ya kujali tofauti zao za Kidini,Kisisasa na Kikabila waunge mkonge mkono na kuthamini kwa vitendo juhudi za Dk.Shein za kulinda Amani,Utulivu pamoja na Rasilimali za Nchi.

Amesema ni lazima Wananchi wafikie wakati waishi kwa misimamo imara ya kulinda Amani pamoja na Tunu za Taifa zikiwemo Mapinduzi ya mwaka 1964,Muungano na Uhuru.

“Maendeleo ya Zanzibar yapo mikononi mwa Wananchi wenyewe kwani ndio walinzi wakubwa wa Amani na Utulivu wa Nchi, tusikubali kugawanywa misingi ya kuichafua Nchi yetu sote hili ni Taifa letu lazima tuwe Wamoja.”amesema Dk.Mabodi.

Pamoja na hayo Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar,amesema kuwa Dk.Shein amekuwa akiisimamia kwa Vitendo  Falsafa yake ya  kuwataka Viongozi na Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla washuke kwa Wananchi wa ngazi zote kwa kuratibu Changamoto zao kasha kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Dk.Mabodi amesema CCM imeendeleza utaratibu wake wa Viongozi kupitia Kamati za Siasa za ngazi mbali mbali kukagua,kutathimini na kutoa maelekezo katika miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali Kuu,Serikali za Mitaa pamoja na Chama kuhakikisha inawafikia kwa wakati na kuwanufaisha Wananchi wote bila ya ubaguzi.

Amesema kwamba kasi hiyo haitokuwa na kizuizi mpaka mwaka 2020,ambapo Mamilioni ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla kwa hiari zao waitapa ridhaa CCM Kidemokrasia ishinde na kuendelea kuongoza Dola.

Akizungumzia hafla hiyo Dk.Mabodi amemshukru Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kwa Busara,Upendo na Hekima zake kwa kuwaahidi kuliwa Karamu katika Tawi hilo ikiwa ni Sadaka kwa Wana CCM na Wananchi wa eneo hilo.

Katika Risala ya Wanachama wa Tawi hilo la CCM, wameshukru na kupongeza Utekelezaji wa ahadi hiyo kwa vitendo iliyotolewa na Dk.Shein siku za hivi karibuni katika ufunguzi wa Tawi hilo.

Wamesema wanaridhishwa na Utendaji wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Shein katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM, na waliahidi kuendelea kukitumikia Chama ili kishinde kwa kila Uchaguzi wa Kidemokrasia.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni