Jumanne, 30 Juni 2020

MHE.SAMIA AANZA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA KUSINI UNGUJA.


 MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja, katika ziara yake ya kuimarisha Chama,Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa SUZA Tunguu.
 WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa kusini Unguja,wakifuatilia maelekezo yanayotolewa na mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Samia Suluhu Hassan.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,amewasihi Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja kuendelea kuwa wamoja na kushikamana katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Dola mwaka huu.

Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na wajumbe hao huko katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA),amesema ushindi wa Chama Cha Mapinduzi utatokana na ushirikiano baina ya viongozi hao na wanachama wote.

Mhe.Samia alisema licha ya mkoa huo kuwa ngome ya Chama bado wanatakiwa kulinda heshima hiyo kwa kujipanga vizuri kuhakikisha Chama kinashinda.

"Nakuombeni tufanye kazi kwa mashirikiano makubwa kwani ushindi wa Chama chetu hautopatikana kwa maneno bali kwa juhudi za kila mmoja wetu", alisema Mhe.Samia.

Katika maelezo yake Mhe.Samia, aliwasihi wajumbe hao kufuata miongozo na kanuni za Chama wakati wa kufanya uteuzi wa wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi katika Mkoa huo.

Pamoja na hayo alikemea vitendo vya rushwa na makundi ya kukigawa kwani vitendo hivyo vinapelekea kupatikana kwa viongozi wasiokuwa na sifa za uongozi.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kupongeza mkoa huo kwa juhudi zao za kiutendaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kichama.

Alitoa pole kwa wananchi wa mkoa huo kwa kukumbwa na majanga mbali mbali yakiwemo ugonjwa wa corona pamoja na mafuriko na kuwasihi kuendelea kuchukua tahadhari.

Alisisitiza wananchi kuendelea kutunza mazingira ili kuepuka majanga mbali mbali yakiwemo mafuriko.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa huo Ramadhan Abdallah Ali,alimpongeza Mjumbe wa Kamati kuu Mhe.Samia kwa utendaji wake na kuwa karibu na mkoa huo kwa kutoa nasaha za kujenga Chama.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa huo Suleiman Mzee Suleiman,akisoma taarifa ya utekelezaji ya Chama kuanzia Januari hadi Machi 30 mwaka huu,alisema wamejipanga vizuri na watahakikisha wanashinda majimbo yote yaliyomo ndani ya mkoa huo.

Kupitia taarifa hiyo waliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Jumatano, 24 Juni 2020

FATMA KOMBO ACHUKUA FOMU YA KUOMBA RIDHAA YA URAIS WA ZANZIBAR.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Oganazesheni Cassian Gallos Nyimbo(kushoto), akimkabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Kada wa Chama Cha Mapinduzi Fatma Kombo Masoud(kulia),hafla iliyofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.




HASNA ATTAI ACHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR

KADA wa CCM Hasna Attai Masoud aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM akionyesha mkoba wenye fomu za kuwania Urais wa Zanzibar, mara baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallos Nyimbo, hafla hiyo imefanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwsandui,Zanzibar.




MBIO za kusaka Urais wa Zanzibar zimeendelea leo Juni 24,2020 kada wa CCM Hasna Attai Masoud(40), amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Hasna, akiwa ni mwanamke wa pili kujitokeza katika kinyang’anyiro hicho amewasili katika Ofisi za Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar majira ya 4:00 asubuhi na kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallos Nyimbo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuwaamini na kuwapatia fursa mbali mbali za uongozi na utendaji wanawake nchini.

Amesema Dk.Shein, amekuwa ni kiongozi wa kuigwa katika kuthamini kundi la wanawake ambao kwa miaka mingi walikuwa hawana uwakilishi mkubwa katika nafasi mbali mbali za uongozi kama ilivyo hivi sasa.

“ Serikali ya awamu ya saba chini ya uongozi wa Rais wetu mpendwa Dk.Shein imewaona wanawake na kuwapatia nafasi kubwa ya kuongoza katika vyombo vya kufanya maamuzi, hivyo nasi tumehamasika sana nasi kuingia katika ushindani wa kuwania nafasi mbali mbali za uongozi”, amesema.


Kada huyo ambaye ni msomi wa shahada ya pili ya masuala ya usimamizi wa biashara, anakuwa ni wa 25 kuchukua fomu hiyo ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Jumanne, 23 Juni 2020

MWANAMICHEZO HASHIM SALUM ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS WA ZANZIBAR.





KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hashim Salum Hashim leo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Kada huyo amewasili katika Ofisi za Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Kisiwandui Zanzibar majira ya saa 6:10 mchana na kupokelewa na maafisa wandamizi wanaoshughulikia mapokezi ya makada hao.

Hashim alikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallas Nyimbo, na kumtaka atafute wadhamini 250 wa Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu hizo Hashim, amesema endapo atapewa ridhaa na Chama atahakikisha kipaumbele chake ni kuimarisha sekta ya michezo nchini.

Amesema yeye ni mwanamichezo na amehudumu katika sekta hiyo kwa muda mrefu hivyo atahakikisha serikali inatoa  udhamini wa ligi kuu ya soka Zanzibar  kwa asilimia 100.

Amefafanua kuwa ligi hiyo inaendeshwa bila udhamini kwa muda mrefu toka kampuni ya Grand Malta isitishe udhamini wake mwaka 2013.

Ameongeza kwamba mbali na michezo pia ataendeleza maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 ya Serikali ya awamu ya saba chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

“Nampongeza Rais wetu Dk.Shein kwa kasi yake ya kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo endelevu hasa katika sekta za afya,elimu, miundombinu ya umeme na barabara, maji safi na salama pamoja na sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii”,amesema.

Pamoja na hayo kada huyo ambaye ni mtumishi wa SMZ katika Idara ya Mazingira amesema ataimarisha maendeleo katika Nyanja za kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya wananchi wote.


MOHAMED HIJA AREJESHA FOMU YA KUOMBA URAIS


 KADA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mohamed Hija amerejesha fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, na kumkabidhi Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazeni CCM Zanzibar Cassian Gallos Nyimbo.


RASHID, MASAUNI,RC AYOUB NA BHAA NAO WAJITOSA MBIO ZA URAIS ZNZ



MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni baadhi ya wanachama waliochukua fomu, kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya urais wa Zanzibar.

Wa kwanza aliyefika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui baada ya kufunguliwa ofisi hizo saa 2:00 asubuhi ni Mwakilishi wa Jimbo la Amani, Rashid Ali Juma (54).

 Alikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Idara ya Oganaizesheni, Cassian Gallos Nyimbo ambaye alimtaka kutafuta wadhamini 250 katika mikoa mitano ya Unguja na Pemba.

 Akizungumza na waandishi wa habari, Juma ambaye ni mchumi katika masuala ya kodi akiwa mwanzilishi wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), aliipongeza CCM kwa kuweka utaratibu mzuri katika uchukuaji wa fomu, kwa kutoa ruhusa kwa kila mwanachama kutumia demokrasia yake.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, aligombea jimbo la Amani na kuibuka na mshindi na kuteuliwa na Rais Dk Ali Mohamed Shein kuwa Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni na baadaye kuhamishiwa katika Wizara ya Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi.



 Mwingine aliyefika kuchukua fomu ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yussuf Masauni aliyeambatana na mkewe. Masauni ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Alikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya CCM, Gallos Nyimbo. Akizungumza na waandishi wa habari, Masauni alisema akipewa ridhaa kuongoza Zanzibar, atahakikisha anaendeleza mambo yote mazuri, yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar, Dk.Shein na Rais John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa na wahujumu wa uchumi.



 ‘’Leo mimi sina cha kusema kwa waandishi wa habari...lakini nikipewa ridhaa ya kuongoza nchi nitahakikisha nafuata nyayo za watangulizi wangu na Rais Shein katika mapambano dhidi ya rushwa na wahujumu uchumi,”alisema.



Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Khamis Mussa Omar alijitokeza na kuchukua fomu kuomba ridhaa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar.

Mussa ni msomi wa masuala ya kodi na amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa miaka 14 sasa.

Pia aliwahi kuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2002. Ni miongoni mwa waanzilishi wa Mamlaka ya Uwekezaji nchini (ZIPA) mwaka 2005-2006. 

 ZIPA ndiyo iliyoweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta mbalimbali, ikwemo uwekezaji wa hoteli za kitalii. ‘’Nimechukua fomu kuomba ridhaa ya nafasi ya urais wa Zanzibar, lakini si kwa gharama yoyote na sitanuna kama sitachaguliwa kushika wadhifa huo,’’alisema.

 Mwingine aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa kupeperusha bendera ya CCM ni Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Majawiri.



Mjawiri alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SUZA). ‘’Nimejitathmini kwa makini sana kwa kuzingatia kauli ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Magufuli kwa wale wanaokusudia kuchukua fomu na ndiyo maana nimechukua fomu hii,’’alisema Mjawiri, ambaye ni Mwakilishi wa jimbo la Mkoani katika kisiwa cha Pemba.



 Waziri mwingine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) aliyechukua fomu ya ni Mohamed Aboud Mohamed, anayeongoza Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, inayoratibu shughuli mbalimbali ikiwemo za Muungano.

Aboud amechukua fomu ya urais wa Zanzibar huku akisema “Hatukuja kushindanishwa wagombea katika kinyang’anyiro hicho.

Nimekuja kuchukua fomu kwa ajili ya kutekeleza demokrasia pana katika Chama Cha Mapinduzi” alisema.



Mwingine aliyechukua fomu ni kada wa CCM ambaye ni Mhadhiri wa vyuo mbalimbali nchini, Bakari Rashid Bakari (56).

Alikipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa kufungua milango ya kuchukua fomu na kuweka mazingira mazuri kwa kila mwanachama wa chama hicho mwenye sifa na uwezo.


Mwingine aliyechukua fomu ya CCM kuwania urais wa Zanzibar ni Hussein Ibrahim Makungu maarufu kama ‘’Bhaa’’.

Aliahidi kufanya mambo makubwa yenye maslahi kwa wananchi wa Zanzibar, ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 ‘’Nimefurahishwa na demokrasia iliyotukuka ndani ya Chama cha Mapinduzi, yenye kutoa fursa kubwa kwa kila mwanachama mwenye sifa na uwezo,’’alisema.

 Kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari, Hussein alizuru kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Shehe Abeid Amani Karume.

Hussein ni Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni. Kabla ya hapo alikuwa mwakilishi wa Jimbo la Bububu huku akiwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitia nafasi tano za Baraza la Wawakilishi.

 Mtu mwingine aliyechukua fomu ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohammed.

Jumapili, 21 Juni 2020

DK.KHALID ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS ZANZIBAR

 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallos  Nyimbo (kushoto) akisalimiana na Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed(kulia), aliyefika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

 Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar.
 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallos  Nyimbo (kushoto) akimkabidhi mkoba wenye fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed(kulia), hafla iliyofanyika Afisi Kuu CCM Kisiwandui Zanzibar. 




 Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed(kulia),akisalimiana na kada mkongwe wa CCM Baraka Shamte(kushoto), mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari.





           Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed,leo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallos Nyimbo, huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. 

Amesema endapo Chama kitamuona anafaa na kumpatia ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, atashirikiana na wananchi wote kuendeleza maendeleo yaliyofikiwa na Dk.Shein.

Amesema ameamua kuingia katika mchakato wa kuomba nafasi hiyo ya Urais baada ya kujitathimini na kuona anao uwezo na nguvu za kuwatumikia wananchi kwa uadilifu mkubwa.

Amefafanua kuwa akipewa nafasi hiyo ataongoza kwa kufuata kanuni,sera,miongozo na taratibu zilizopo nchini kisheria.

Katika maelezo yake Dkt.Khalid, ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Donge ameongeza kuwa atafuata Katiba zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Dkt.Khalid, ameeleza kuwa katika kuimarisha maendeleo ya nchi atahakikisha anafuata dira ya maendeleo ya nchini ili kwenda sambamba na mikakati ya kiuchumi katika nyanja za Kimataifa.

"Namshukru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema na kunipa uwezo wa kuja kuchukua fomu hii ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar, naendelea kuwaomba wananchi wenzangu mniombee duwa niweze kutimiza dhamira yangu hii ya kuwatumikia wananchi", amesema Dkt.Khalid.

Amesema maendeleo yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 10 ya Uongozi wa Dk.Ali Mohamed Shein, yamefikiwa kutokana na juhudi za kila mwananchi na yeye akiwa ni miongoni mwao.

Amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020, iliyoleta maendeleo mijini na vijijini.

Dkt.Khalid amekuwa ni Kada wa CCM wa 15 anayeomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar toka kuanza kwa zoezi la utoaji wa fomu hiyo katika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwanduzi Zanzibar Juni 15,mwaka 2020.   






Jumamosi, 20 Juni 2020

JECHA SALIM JECHA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani Zanzibar (ZEC), Ndg, Jecha Salim Jecha leo hii Amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi







Ijumaa, 19 Juni 2020

MAKADA WA CCM WANNE LEO WACHUKUA FOMU ZA URAS WA ZNZ

 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazeni CCM Zanzibar Cassian Galos Nyimbo (kushoto), akimkabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Waziri wa Maji Prof.Makame Mnyaa Mbarawa(kulia), hafla iliyofanyika leo Juni 19,2020 Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

 KADA wa Chama Cha Mapinduzi Mwatum Mussa Sultan, akionyesha mkoba wenye fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar, mara baada ya kukabidhiwa na KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazeni CCM Zanzibar Cassian Galos Nyimbo, hafla iliyofanyika leo Juni 19,mwaka 2020 Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

 KADA wa Chama Cha Mapinduzi Mwl.Haji Rashid Pandu(kulia), akionyesha mkoba wenye fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, mara baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazeni CCM Zanzibar Cassian Galos Nyimbo, hafla iliyofanyika leo Juni 19,mwaka 2020 Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Galos Nyimbo(kushoto), akimkabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Kada wa Chama Cha Mapinduzi Dk.Abdul-halim Mohamed Ali(kulia), hafla hiyo imefanyika leo Juni 19, mwaka 2020 Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.


  
MAKADA wengine wanne leo wameendelea wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar,ambao ni Waziri wa Maji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa,Kada wa CCM Mwatum Mussa Sultan,Kada wa CCM Mwl.Haji Rashid Pandu na Kada wa CCM Dk.Abdul-halim Mohamed Ali ambao wamefikisha idadi ya makada 13 waliochukua fumu hizo toka zoezi hilo lianze Juni 15,mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo, majira ya saa 4:00 asubuhi

Waziri wa Maji Prof.Makame Mnyaa Mbarawa,hafla hiyo imefanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Amesema anamshukru Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia uwezo na nguvu za kushiriki katika mchakato huo ambao ni muhimu katika hisoria mpya ya maisha yake.

Amesisitiza kwamba jambo muhimu kwa sasa ni kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kufungua milango ya neema katika zoezi hilo liendelee kufanyika kwa ufasini na afikie malengo yake ya kuwa Rais wa Zanzibar.

Aidha amesema atazungumza kwa upana mambo mbali mbali juu ya mbio zake za kuwania Urais wa Zanzibar pindi atakapokamilisha zoezi la kujaza fomu hizo.

Naye Mwatum akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo, alikipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa ukomavu wake wa demokrasia ya kuwaruhusu makada wake wa jinsia zote kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi kupitia Chama hicho.

Amewataka Wanawake nchini kuendelea kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ili kufikia asilimia 50 kwa 50 katika vyombo vya kufanya maamuzi.

Amesema amechukua fomu hiyo ili kuwahamasisha wanawake wengine wajitokeze katika kuwania nafasi mbali mbali za uongozi kama walivyo wanaume.

"Nachukua nafasi hii kumuomba Mwenyezi Mungu anisimamie katika safari yangu hii ya kuomba ridhaa ya kuwa Rais wa Zanzibar", amesema Mwatum.

Pamoja na hayo amesema hatoweza kutoa maelezo mengi kwa waandishi wa habari mpaka atakapokamilisha   zoezi la kujaza fomu hiyo.

Kwa upande wake kada wa CCM Mwl.Haji Rashid Pandu,akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo amesema lengo lake ni kutetea maslahi ya wakulima ambao mchango wao ni mkubwa katika maendeleo ya nchi.

Kada huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu,amesema lengo lake ni kusimamia kwa vitendo falsafa ya mapinduzi ya kilimo nchini.

Akizungumza kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Abdul-halim Mohamed Ali aliyechukukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM,amesema lengo ni kuhakikisha Zanzibar inakuwa na maendeleo endelevu.

Dkt.Abdulhalim, amesema endapo Chama Cha Mapinduzi kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kuwania kiti cha Urais, atakuwa mstari wa mbele kutatua changamoto za wananchi bila ubaguzi.

Alhamisi, 18 Juni 2020

MEJA JENERAL MSTAFU: ISSA SULEIMAN NASSOR

Kada mwingine aliyejitosa katika kinyanga'nyiro hicho ni Meja Jenerali Mstaafu Issa Suleiman 
Nassor alisema anakishukuru chama kwa utaratibu walioweka wa demokrasia ya kila mwanachama kujitokeza kugombea nafasi hiyo.

Alisema amefurahia utaratibu uliowekwa na CCM  na kwamba endapo akipatiwa ridhaa na chama  kupeperesha bendera ya kinyanga'nyiro atatekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya chama.

"Ikiwemo kusimamia hali ya amani tulionayo na  sisitiza hicho kitu umoja na uzalendo nataka kila
mtu hajue ana nafasi ya kuhakikisha ataifanyia nini Zanzibar,"alisema

Alisema yeye ni muhumini wa muungano na nitaendeleza muungano uliopo kwa mujibu wa katiba inavyoeleza ataimarisha uchumi kadri itakavyokwenda na kadri ilani ya CCM inavyozungumza.

"Na nitaendeleza yale yote yaliyofanywa na viongozi waliotangulia kama nitapata ridhaa ya wananchi basi tutahakikisha uchumi wa Zanzibar una kuwa kwa maslahi ya wananchi kwa jumla na si kwa maslahi ya watu wachache au mtu binafsi,"alisema








BALOZI MOHAMMED HIJA MOHAMMED

Kada mwingine aliyejitokeza majira ya saa saba kuchukua fomu hiyo ni Balozi Mohamed Hija 
Mohamed alisema anaishukuru CCM kwa kutoa nafasi ya kipekee kwa wanachama wake kujitokeza kuchukua fomu na kwamba yeye ni mmoja wao.

Alisema amechomoza kuchukua fomu hiyo na kwamba  amekuja kwa lengo la kuchukua fomu ili aisome na kuelewa kutokana kuwa bado safari ni ndefu.

"Naomba nipeni muda wa kusoma hizi fomu ni rudi nyumbani nizisome alafu tuone hali itakavyokuwa mbele ya safari tutakaa tuzungumze mambo mengi zaidi,"alisema