Majira ya saa mbili asubuhi Nahodha aliingia kwenye ofisi za CCM kuchukua fomu hizo na baada ya kuchukua fomu alizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema anakishukuru chama kwa kumpatia heshima kubwa ya kuchukua fomu ya kuomba kupewa ridhaa na CCM kugombea nafasi hiyo ya urais wa Zanzibar.
Alisema ana uwakika watu wengi na wanachama wangetamani Mwenyezi Mungu awapatie fursa hiyo na kwamba wengine watafanikiwa na wengine hawatafanikiwa.
"Sasa mimi kwa hilo namshukuru sana Mungu na jambo lingine ninawapenda sana waandishi wa habari wamenilea,walinikuza si watu wengi wanajua kuwa nimetokea huko kwenye tasnia hiyo hivyo ninadhamini sana kazi mnazozifanya kwa mustakabali wa taifa letu,"alisema
Nahodha aliwaambia waandishi wa habari kuwa leo anajua wana kiu kubwa ya kutaka aseme na kwamba siku zijazo atazungumza nao na wajiandae kuandaa maswali magumu na mazuri zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni