Alhamisi, 8 Oktoba 2020

DK.MWINYI- ATAKA WAWEKEZAJI WACHANGIE MAENDELEOMGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM amesema endapo atapewa ridhaa ya kuwa rais wa zanzibar,atahakikisha wawekezaji wanachangia maendeleo ya jamii inayowazuka.

 Alisema katika utawala wake ni lazima kila mwekezaji anachangia maendeleo ya kijamii kwa kujenga shule,hospitali na miundombinu ya maji safi na salama. 

 Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii ya wafanyabiashara wadogowadogo wakiwemo mama lishe,walinzi wa mahoteli, wavuvi na wafanyabisha za maduka ya vileo katika Kijiji cha Kiwengwa Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja. 

 Dk.Mwinyi, alisema haiwezekani wawekezaji wanufaike na rasilimali za nchi huku wenyeji wakibaki katika lindi la umaskini. 

 "Sekta ya utalii ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, hivyo ni lazima matokeo ya uwepo wa sekta hiyo yaonekane kuanzia kwa jamii zilizopo katika ukanda wa utalii ziwe na miundombinu bora na rafiki ya kijamii. 

 sio dhambi wawekezaji kusaidia maendeleo katika maeneo waliyowekeza japokuwa wapo baadhi wanatoa wanaotoa michango yao lakini wengi bado hawajahamasika",alisema Dk.Mwinyi.

 Akizungumzia suala la ajira kwa walinzi wa mahoteli Dk.Mwinyi, alisema atahakikisha watu hao wanapatiwa mikataba inayozingatia haki na maslahi yao pindi wanapomaliza mikataba hiyo ama kustaafu.

 Aidha,akizungumzia suala la Kodi na leseni kwa wafanyabiashara ndogondogo,alifafanua kuwa atahakikisha panatengenezwa mfumo mmoja wa ulipaji wa kodi kulingana na kipato cha mfanyabiashara sambamba na kupatiwa kipambulisho maalum kitakacholipiwa kila mwaka.

 "Nimeambiwa tayari serikali imeanza mchakato wa kutoa vitambulisho kwa kila mfanyabiashara na kuweka kiwango maalum cha ulipaji wa Kodi ambacho kitaondosha kero hiyo.",alisema Dk.Mwinyi.

 Akijibu hoja za wananchi Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi,alisema lengo la ziara hiyo ni kusikiliza changamoto za wafanyabiashara wadogo wadogo.

 Alisema kero za wafanyabiashara amezisikia hasa kuhusu suala la Kodi hivyo amesema kuwa akipata ridhaa naa kuwa rais suala Hilo atalitafutia ufumbuzi. 

 Alisema lengo la kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar ni kuhakikisha kila mwananchi anapata haki na kudhibiti vitendo vyote vya dhuruma. 

 Aliwambia wananchi hao kuwa katika utawala wake hatoruhusu vitendo vya uvunjaji wa sheria kwa wananchi vinavyosadikiwa kufanywa na viongozi ama watendaji wa serikali. 

 Alisema vitendo vya ubaguzi hatoruhusu viendelee kwani wananchi wa Tanzania ni wamoja na kwamba ubaguzi ni adui wa maendeleo. 

 Akizungumzia wajasiriamali alisema katika serikali yake watapatiwa mafunzo,watapewa mikopo na mitaji ya masharti nafuu na kuwatafutia masoko ya uhakika. 

 Dk.Mwinyi, akizungumza na waendesha pikipiki wa wilaya hiyo(bodaboda), aliwambia atahakikisha wanatambuliwa kisheria,kupewa mikopo ya masharti nafuu na kupatiwa huduma ya bima ya Afya ili pindi wanapopata ajali wawe na uhakika wa kupata matibabu.

 Katika maelezo yake Dk.Hussein,alisema suala la uvuvi wa kisasa ni sehemu ya ajenda ya serikali ijayo kupitia mfumo wa uchumi wa blue(blue economy), kwa kufanya uvuvi wa kisasa mpaka ufugaji wa samaki sambamba na kuwawezesha nyenzo za kisasa za uvuvi.

 Aliwambia wajasiriamali wa kuanika na kuuza dagaa kuwa atatatua changamoto zao kwa kuwawekea miundombinu rafiki katika utendaji wa kazi zao za kila siku.

 Pia alikemea tabia ya rushwa kwa baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo wanaotuhumiwa na kujihusisha na rushwa. 

 Alitumia nafasi hiyo kuomba kura na kuwaombea wagombea wote wa CCM kura za ndio ifikapo octobar 20, mwaka huu ili Chama kiendelee kuongoza dola. 

 Mama lishe Zainab Hussein,amesema wanakabiliwa na changamoto ya Halmashauri kuwatoza fedha nyingi ambazo ni shilingi 5000 kwa mwezi. 

 Alisema kila mwaka wanalipa shilingi 10,000 kwa leseni,wahudumu wa migahawa wanapimwa Afya kwa gharama za shilingi 60,000. 

 kwa upande wa Mama lishe Zuwena Kassim, wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 20. 

 Alisema wanakabiliwa na changamoto ya kuwa vibarua bila kupewa mikataba ya kulinda maslahi yao na kukosa michango ya kuweka katika mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) na kiinua mgongo.

 "Tunabaguliwa sana sisi jamii ya wamasai Kama vile sio binadamu Kama walivyo wengine tunaomba sana ukiwa rais uweke mazingira ya kulinda haki zetu,''alisema john. 

 Alisema kuwa katika eneo la Kiwengwa maeneo mengi hayana vyoo Jambo ambalo ni hatari kiafya.

 Alisema kuwepo kwa utalii ni Jambo Jema lakini wengine wanauza hadi chakula cha mama lishe na wengine kufanya kazi ambazo wenyeji wanaweza kufanya.

 Katibu wa jumuiya ya waanika dagaa Saleh Khatib Makame, kuwa na eneo maalum la godown,kujengewa ofisi ya jumuiya ya waanika dagaa na kupunguziwa Kodi na Halmashauri ya wilaya hiyo.

DK.MWINYI-ASEMA ATATATUA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI

 


MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema akipata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar, ataweka misingi imara kwa wafanyabiashara ili wafanye biashara zitakazoleta tija nchini.

Dk. Mwinyi alisema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara kusikiliza changamoto zinazowakabili ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za mgombea huyo, mkutano uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Malindi.

Alisema sekta biashara ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kuongeza pato la taifa hivyo atahakikisha anafungua milango ili wafanyabiashara waitumie kuimarisha mifumo ya biashara.

Dk. Mwinyi alisema ni vyema kwa wafanyabiashara wa ndani kuwa tayari kuitumia milango hiyo kwa kufanya biashara kubwa ndani ya nchi na kutokaa pembeni kupoteza fursa zitakazojitokeza.

“Ninagombea nafasi hii, kwa lengo la kuwatumikia wananchi na wafanyabiashara ni sehemu muhimu ya wananchi hivyo ninawaomba mjipanga vyema tukashirikiane na kwenda sambamba na matakwa ya wanachi wetu,” alieleza Dk. Mwinyi.

Alisema ili kufikia azma hiyo, serikali atakayoiongoza itashirikiana na jumuiya za wafanyabiashara na kuangalia sheria, kanuni, masuala ya kodi na ukataji wa leseni za biashara ili kuondoa vikwazo katika shughuli za biashara na viwanda nchini.

Akizungumzia sekta ya utalii, Dk. Mwinyi alisema ataiendeleza ili kuinua kiwango cha idadi ya watalii wanaoingia nchini lakini pia kuongeza thamani na aina za utalii kama njia moja wapo ya kuongeza mapato yanayotokana na sekta hiyo.

Alisema pamoja na Zanzibar kuendelea kuwa sekta kiongozi katika kuchangia pato la taifa, bado inapaswa kutangaza vivutio ilivyonavyo zikiwemo fukwe na kwa kuwekewa mipango madhubuti itakayowavutia watalii kuongezeka.

Kwa upande wa maendeleo ya viwanda, Dk. Mwinyi alisema sekta hiyo inahitaji mapinduzi makubwa ili isaidia ustawi wa wananchi wote wakiwemo wawekezaji wazawa kuwekeza kupitia sekta hiyo.

“Sekta ya viwanda itakapoimarika, wakulima na wafanyabiashara wadogo wataweza kutumia viwanda kwa kazi tofauti ili zilete tija kwao na taifa kwa ujumla,” aliemeza Dk. Mwinyi.

Mapema Akiwazungumza katika mkutano huyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC), Ally Amour, alisema serikali ya awamu ya saba imefanya mengi kwa wafanyabiashara hali ambayo imepelekea kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi wa nchi.

Alisema ni vyema anapoingia madarakani kiongozi huyo kusaidia kutayarisha mazingira mazuri ya biashara ili nchi iweze kusonga mbele zaidi kimaendeleo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, walimuomba kiongozi huyo kuzipa kipaumbele baadhi ya changamoto zilizobakia hususani kupitia sekta ya kilimo kwa kukipa kipaumbele kilimo cha umwagiliaji maji ili kuongeza uzalishaji utakaokidhi mahitaji ya ndani chakula.

Mbali na hayo walimuomba akiingia madarakani kulipatia ufumbuzi tatizo ufungaji wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ya watu binafsi kwani imechangia kuvuruga mfumo wa maisha na biashara za baadhi nya wafanyabiashara wanaofanya shughuli hizo.


DK.HUSSEIN-AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA

 


MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema akipata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar, ataweka misingi imara kwa wafanyabiashara ili wafanye biashara zitakazoleta tija nchini.

Dk. Mwinyi alisema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara kusikiliza changamoto zinazowakabili ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za mgombea huyo, mkutano uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Malindi.

Alisema sekta biashara ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kuongeza pato la taifa hivyo atahakikisha anafungua milango ili wafanyabiashara waitumie kuimarisha mifumo ya biashara.

Dk. Mwinyi alisema ni vyema kwa wafanyabiashara wa ndani kuwa tayari kuitumia milango hiyo kwa kufanya biashara kubwa ndani ya nchi na kutokaa pembeni kupoteza fursa zitakazojitokeza.

“Ninagombea nafasi hii, kwa lengo la kuwatumikia wananchi na wafanyabiashara ni sehemu muhimu ya wananchi hivyo ninawaomba mjipanga vyema tukashirikiane na kwenda sambamba na matakwa ya wanachi wetu,” alieleza Dk. Mwinyi.

Alisema ili kufikia azma hiyo, serikali atakayoiongoza itashirikiana na jumuiya za wafanyabiashara na kuangalia sheria, kanuni, masuala ya kodi na ukataji wa leseni za biashara ili kuondoa vikwazo katika shughuli za biashara na viwanda nchini.

Akizungumzia sekta ya utalii, Dk. Mwinyi alisema ataiendeleza ili kuinua kiwango cha idadi ya watalii wanaoingia nchini lakini pia kuongeza thamani na aina za utalii kama njia moja wapo ya kuongeza mapato yanayotokana na sekta hiyo.

Alisema pamoja na Zanzibar kuendelea kuwa sekta kiongozi katika kuchangia pato la taifa, bado inapaswa kutangaza vivutio ilivyonavyo zikiwemo fukwe na kwa kuwekewa mipango madhubuti itakayowavutia watalii kuongezeka.

Kwa upande wa maendeleo ya viwanda, Dk. Mwinyi alisema sekta hiyo inahitaji mapinduzi makubwa ili isaidia ustawi wa wananchi wote wakiwemo wawekezaji wazawa kuwekeza kupitia sekta hiyo.

“Sekta ya viwanda itakapoimarika, wakulima na wafanyabiashara wadogo wataweza kutumia viwanda kwa kazi tofauti ili zilete tija kwao na taifa kwa ujumla,” aliemeza Dk. Mwinyi.

Mapema Akiwazungumza katika mkutano huyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC), Ally Amour, alisema serikali ya awamu ya saba imefanya mengi kwa wafanyabiashara hali ambayo imepelekea kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi wa nchi.

Alisema ni vyema anapoingia madarakani kiongozi huyo kusaidia kutayarisha mazingira mazuri ya biashara ili nchi iweze kusonga mbele zaidi kimaendeleo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, walimuomba kiongozi huyo kuzipa kipaumbele baadhi ya changamoto zilizobakia hususani kupitia sekta ya kilimo kwa kukipa kipaumbele kilimo cha umwagiliaji maji ili kuongeza uzalishaji utakaokidhi mahitaji ya ndani chakula.

Mbali na hayo walimuomba akiingia madarakani kulipatia ufumbuzi tatizo ufungaji wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ya watu binafsi kwani imechangia kuvuruga mfumo wa maisha na biashara za baadhi nya wafanyabiashara wanaofanya shughuli hizo.DK.MWINYI -AWEKA WAZI NEEMA KWA WANANCHI WA KASKAZI 'B' UNGUJAMGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema endapo atakuwa rais wa Zanzibar atahakikisha anajenga bandari mpya ya kisasa ya mafuta na gesi asililia ili kukuza uchumi wa nchi. 

 Alisema ujenzi wa bandari hiyo hautoathiri shughuli za wananchi hasa wanaojishughulisha na uvuvi katika maeneo ya wilaya hiyo. 

Ahadi hiyo ameitoa katika mwendelezo wa mikutano ya kampeni za CCM katika wilaya ya Kaskazini ‘B’ huko katika skuli ya bumbwini Wilaya ya kaskazini ‘B’ Unguja.

 Alisema bandari hiyo ikikamilika itakuwa ndio kitovu cha uchumi wa nchi kwani itasaidia kutoa ajira nyingi.

 Aidha, alisema atavipa kipaumbele vikundi vya ujasiriamali kwa kuvipatia mikopo na mafunzo ili wanufaike na fursa hizo. 

 Alisema atahakikisha wananchi wa wilaya hiyo wananufaika na ufugaji wa kisasa wa samaki ili waende sambamba na dhana ya uchumi.

 Pia alijiombea kura na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM ili CCM iendelee kuongoza dola.

Pamoja na hayo aliwataka wananchi walinde amani ya nchi na wasikubali kuchokozeka na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wapinzani.

Alisema atajenga hospitali ya wilaya,kununua vifaa tiba vya kisasa na kuajiri wafanyakazi wa sekta ya afya ili huduma zitakazotolewa zikidhi mahitaji ya wakaazi wa wilaya ya kaskazini ‘B’ Unguja. 

 Pia ameahidi kujenga barabara ya bumbwini hadi mahonda ili kukuza uchumi wa wananchi wa maeneo hayo.

 Aidha alisema watajenga skuli ya ghorofa na daharia pamoja na kuthibiti changamoto ya wizi wa mifugo ili wananchi wanufaike na fursa za ufugaji.

 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alisema historia ya Zanzibar imeanzia mbali kwani toka utawala wa wareno na waoman.  

Dk.Shein, alisema toka mwa 1957 zilifanyika chaguzi mbalimbali lakini wazawa hawakuwahi kushinda uchaguzi huo kutokana na kuwepo kwa njama za ukandamizaji.

 Alisema baada ya utawala wa ukandamizaji wa wakati huo,Wazee wa kiafrika chini ya uongozi wa marehemu Abeid Amani Karume wakaamua kuondosha utawala huo kupitia mapinduzi ya mwaka 1964.

 Dk.Shein, alisema baada ya mapinduzi hayo nchi ilikuwa huru na kuweka viongozi kwa awamu mbalimbali toka awamu ya kwanza mpaka hivi sasa tunaelekea awamu ya nane.

 Alisema kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa wanajifanya hawatambui mapinduzi kutokana na sababu zao za kisiasa. 

Alisema kwa sasa nchi ipo katika harakati za uchaguzi hivyo wananchi, wasikubali kuongozwa na watu wabaguzi wa kidini.kikabila na kisiasa. 

Alieleza kuwa CCM imemteua Dk.Mwinyi kwa kuwa ana sifa zinazokubalika ndani ya jamii yake sambamba na kuwa na sifa za ziada za kuwa mpole,mvumilifu,mcheshi,mcha mungu na mwadilifu.

 Alisema Dk.Hussein, ana sifa nyingine tofauti na wagombea wengine mwani ana uzoefu wa kiutendaji ndani ya serikali na ni msomi wa fani ya udaktari. 

 Alieleza kuwa CCM imemkabidhi Dk.Mwinyi, bendera na ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 ili vimuongoze katika kusimamia maslahi ya CCM. 

Dk.Shein, alisema ushindi wa CCM wa mwaka huu ni mkubwa ambao utakuwa ni wa kihistoria katika siasa za afrika mashariki kwani CCM imejipanga vizuri kuhakikisha inashindwa kwa njia za kidemokradsia. 

Alisema hakuna njia ya mkatoa ya kuingia ikulu na kwamba ni lazima chama kishinde kupitia uchaguzi huru na wa haki. 

Alieleza kuwa kwa mara ya kwanza Zanzibar itaendesha uchaguzi kwa fedha zake za ndani bila ya kutegemea ufadhili, hatua ambayo ni kubwa kimaendeleo.

Pamoja na hayo aliwaombea kura za ndio wagombea wote wa CCM wakiwemo wagombea wa nafasi za Urais,wabunge,wawakilishi na madiwani.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla, alisema kuwa CCM imetekeleza ilani yake kwa zaidi ya asilimia 100 kwa kuwafikishia wananchi huduma zote za msingi.

Alisema Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Shein, aliasisi mfumo wa kupunguza masafa baina ya chama na serikali kwa kwa kufuatana na viongozi wa CCM kila anapofanya ziara zake za kikazi.

Alisema CCM inaendelea kufanya kampani zake za kisayansi za kuwafuata wananchi katika maeneo yao na kuwaeleza sera zake na namna kitakavyotekeleza miradi mipya ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi wote. 

“ Tumetekeleza kwa kiwango kikubwa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 na mengine mazuri yamo katika ilani mpya ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025”, alisema Dk.Mabodi. 

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Unguja ,Idd Ali Ame alisema wananchi wa mkoa huo wanamshukru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/2020. 

Alisema serikali ya awamu ya saba imetekeleza mambo mengi ya maendeleo zikiwemo utengenezaji wa barabara za kisasa,vituo vya afya,majengo ya kisasa ya skuli za msingi na sekondari, ujenzi wa kituo cha mafunzo ya amali, huduma za maji safi na salama. 

Alisema wananchi wa mkoa huo watafikisha shukrani zao kupitia upigaji wa kura za ndio kwa kuwachagua wagombea wa CCM ili chama kishinde na kuendelea kuongoza dola.

Akizungumza kwa niaba ya wagombea wa nafasi ya uwakilishi, mgombea uwakilishi jimbo la Donge, Dkt.Khalid Salum Mohamed alisema wanamshukru Rais wa Zanzibar Dk.Shein kwa kuasisi ujenzi wa bandari kubwa katika maeneo ya bumbwini kwani itasaidia kuongeza ajira kwa wananchi wa maeneo hayo na vijiji jirani.

Pia alisema wamejipanga kutekeleza kwa vitendo falsafa ya uchumi wa kupitia rasilimali za bahari(blue economy), na kwamba wananchi wa maeneo hayo ya kaskazini Unguja wananufaika na bahari. 

Pamoja na hayo aliwasihi wananchi kuwapigia kura za ndio wagombea wote waliosimamishwa na Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha wanashinda.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Anna Agata msuya ,amesema amani ya Tanzania inategemea Zanzibar hivyo ni muhimu wananchi kuwapigia kura nyingi za ndio wagombea walioteuliwa na CCM.

Jumatano, 7 Oktoba 2020

KUMEKUCHA BUMBWINI, DK.MWINYI KUMWAGA SERA, DK.SHEIN KUWATAMBULISHA WAGOMBEA.


MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika kiwanja cha skuli ya Bumbwini kwa ajili ya Mkutano wa kampeni za CCM ambao mgeni rasmi ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein,  Wilaya ya Kaskazini 'B' Mkoa wa Kaskazini Unguja 

BAADHI ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa kundi la hamasa wakiburudisha kwa kuimba nyimbo mbalimbali katika mkutano huo wa kampeni za CCM.


VIONGOZI mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa wamekaa jukwaa kuu wakisubiri mgeni rasmi awasili kwa lengo la kuanza kwa mkutano huo wa kampeni za CCM.


MAELFU ya Wana CCM na wananchi kwa ujumla wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya skuli ya Bumbwini kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kampeni za CCM za kuwanadi,kuwatambulisha na kuwaombea kura za ndio  wagombea wa CCM kwa ngazi za Urais wa Zanzibar na jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge, Wawakilishi,madiwani na wagombea kupitia viti maalum.

Mkutano huo ni miongoni mwa mwendelezo wa kampeni za CCM zinazofanyika nchini na kuhudhuriwa na wananchi wengi.

Kupitia mkutano huo mgeni rasmi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, atawatambulisha  na kuwaombea kura za ndio wagombea wote wa CCM.

Pia Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi ataomba kura na kueleza kwa kina sera na vipaumbele vyake ili wananchi wa wilaya ya kaskazini 'B' wafanye maamuzi sahihi ya kuchagua wagombea wanaotoka katika chama chenye sera zinazotekelezeka.

tutaendelea kupata taarifa mbalimbali kupitia blog hii,,,,,,

Imeandaliwa na Kitengo cha Habari Afisi Kuu CCM Zanzibar.

Jumatano, 15 Julai 2020

MAELFU YA WANA CCM WAMPOKEA DK.HUSSEIN MWINYI ZANZIBAR.


 MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk.Abdullah Juma Saadalla Mabodi mara baada ya kuwasili Zanzibar kwa mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa Mgombea wa CCM.

 MAELFU ya Wana CCM wakiwa katika msafara wa mapokezi ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar.

 Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi ,akizungumza na Wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla katika mapokezi yake hafla iliyofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. 

 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumzav na Wana CCM katika mapokezi ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi, hafla iliyofanyika Kisiwandui Zanzibar.

MAELFU ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Wananchi kwa ujumla kisiwani wamejitokeza kumpokea Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dkt.Hussein Ali Hassan Mwinyi,aliyewasili nchini kwa mara ya kwanza toka achaguliwe kushika nafasi hiyo.

Dkt.Hussein amewasili katika Kisiwa cha Unguja leo majira ya saa 3:43 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na kupokelewa na viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

Baada ya kupokelewa makundi mbali mbali ya wanachama yakiwemo ya sanaa pamoja na vijana wa CCM wakiongozwa na kikundi cha pikipiki maalum waliongoza msafara wa kuelekea katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwanduzi Zanzibar, ambapo hafla ya mapokezi ndipo ilipofanyika.

Alipofika katika viunga vya Ofisi hiyo alipokelewa na vijana maalum wa chipukizi na kumvisha sikafu kwa ajili ya kumkaribisha na baada ya hapo alikabidhiwa vifaa mbali mbali na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi na akazuru kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza katika hafla hiyo amesema baadhi ya watu wanadai kuwa Dkt.Hussein sio mzawa wa Zanzibar wanapotosha kwani kiongozi huyo kwa mujibu wa sheria za nchi ni mzaliwa wa Zanzibar na wazazi wake wote wapo.

"Kuna watu tayari wameanza siasa chafu za kuchafuana eti Dkt.Hussein sio mzawa je wao wamezaliwa wapi, wakati sote tunamjua kiongozi huyu kuwa hapa ndio kwao",. amehoji Dk.Shein.

Amesema sifa alizonazo Dkt.Hussein ni nyingi sana zikiwemo upole,uadilifu,utiifu na kuheshimu kila mtu kwa nafasi yake mambo ambayo ni sifa za msingi za kiongozi bora.

Amesema kuchaguliwa kwa Dkt.Hussein kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ndio maendeleo ya CCM ya sasa na yajayo yatakayoendelea kuipaisha nchi kiuchumi.

Pamoja na hayo ameeleza wazi kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa fedha za ndani za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),mara Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) itakapotangaza muda rasmi wa kuanza mchakato wa uchaguzi.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi, akizungumza katika mapokezi hayo alisema CCM itaendelea kuwa kinara wa Demokrasia.

Naye Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dkt.Hussein Ali Hassan Mwinyi, amewahakikishia wananchi kuwa endapo atapata ridhaa ya kuwa Rais wa Zanzibar ataendelea kulinda Amani na Utulivu wa Zanzibar kwani ndio msingi wa maendeleo yote.

Amesema atalinda na kuenzi tunu za taifa zikiwemo Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Amesema uchaguzi ndani ya CCM tayari umeisha na makundi yote yameisha na kwa sasa limebaki kundi moja la kuiletea ushindi CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

" Nitahakikisha suala la upemba,uunguja,ukaskazini na ukusini havipewi nafasi kwani vinaweza kukwambisha kasi ya maendeleo yetu", amesema Dk.Hussein.

Amesema nia ya kuwania Urais huo ni kuwatumikia Wananchi wote bila ya ubaguzi kwa kuhakikisha ya wananchi yakuwa bora.

Ameahidi kuwa katika safari ya maendeleo hayo hatovumilia vitendo vya rushwa,ufisadi,wahujumu wa mali za umma na viongozi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

Wakizungumza kwa wakati tofauti baadhi ya makada wa CCM walioshiriki katika kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya  kuchaguliwa Urais wa Zanzibar kupitia CCM,walisema kuwa mchakato wa kumpata mgombea huyo umefanyika kwa ufanisi mkubwa na watamuunga mkono.

Akizungumza Shamsi Vuai Nahodha, ambaye ni miongoni mwa makada walioshiriki mchakato wa kuomba ridhaa ya Urais kupitia Chama alisema atamuunga mkono mgombea huyo hadi ashinde na kuwa Rais wa Zanzibar.

Kwa upande wake Dkt.Khalid Salum Mohamed, ambaye ni miongoni mwa makada walioshiriki mchakato wa kuomba ridhaa ya Urais kupitia Chama, amesema ushindi alioupata Dk.Hussein ni ushindi wa Wana CCM wote hivyo kazi iliyobaki ni kuhakikisha anashinda.

Naye Prof.Makame Mnyaa mbawara, amewaomba wananchi visiwani humo kutambua kuwa wamepata bahati ya kuwa na mgombea mwenye sifa za kuwa kiongozi bora.

Katika mchakato wa uchaguzi ndani ya Chama, Dk. Hussein, ambaye ni mtoto wa rais wa awamu ya pili Al-Hajji Ali Hassan Mwinyi, aliwashinda wagombea wengine waliofika katika mchujo wa mwisho, ambao ni waziri kiongozi wa zamani Shamsi Vuai Nahodha na Khalid Salum Mohamed.

Katika mchakato wa ndani wa uchaguzi, Dk.Hussein alipata jumla ya kura 129, ambazo ni sawa na asilimia 78.65, dhidi ya kura 16 za Nahodha na 19 za Khalid Mohamed.

Awali, kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar, ilipendekeza  majina matano na kuyawasilisha kwa kamati Kuu. Pamoja na watatu waliofika duru ya mwisho, wengine walikuwa Makame Mbarawa na Khamis Mussa Omar.  
  

Jumamosi, 4 Julai 2020

KAMATI MAALUM Z'BAR YAPENDEKEZA MAJINA MATANO YA MAKADA WANAOWANIA URAIS


KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Zanzibar leo imependekeza majina matano ya makada wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kati ya makada 31.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi, alisema kamati hiyo ni sehemu muhimu ya maandalizi na uchujaji wa majina ya wagombea watano wanaotakiwa kuwasilishwa katika Kamati Kuu kwa ajili ya kujadiliwa tena na kumtafuta mgombea mzuri mwenye sifa 12 zikiwemo hekima,kuaminika,kuthamini muungano na Mapinduzi ya Zanzibar.

Dk.Mabodi alisema baada ya Kamati kuu kujadili kwa kina majina hayo matano itapendekeza majina matatu na kuyapeleka Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambayo itachagua jina la mtu mmoja ambaye atapeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya Urais wa Zanzibar.

Alisema kuwa baada ya hatua hiyo mgombea huyo atapelekwa katika Mkutano Mkuu wa CCM kwa ajili ya kudhibitishwa na kupata baraka za Wajumbe wote wa kamati kuu na kuendelea na michakato mingine.

Dk.Mabodi, alisema baada ya kukamilika kwa mchakato huo itaendelea awamu ya pili ya uchukuaji wa fomu kwa nafasi za Ubunge, uwakilishi na Udiwani na kufuata utaratibu wa miongozo ya CCM.

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo, amewasifu viongozi kwa ukomavu wao wa kisiasa Kwa kufuata Katiba,miongozo na Kanuni za CCM kwa kutobeba wagombea mifukoni.

Alisema kuwa kikao hicho kimesisitiza usiri kwa wagombea hao kwani ndani ya Chama ikibainika miongoni mwao kuna mtu kakiuka utaratibu anaweza kuondolewa na kuchaguliwa mtu mwingine.

"Lazima tuenzi siri za vikao hivyo ni muhimu sana watu wote kuheshimu maamuzi ya vikao na kufuata utaratibu uliowekwa ndani ya CCM," alisema Dk.Mabodi.

Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu ulianza Juni 15 hadi 30, mwaka huu ambapo jumla ya makada 32 walijitokeza kuchukua fomu hiyo ambao ni Mbwana Bakari Juma, Ali Abeid Karume,Mbwana Yahya Mwinyi,Omar Sheha Mussa,Hussein Ali Mwinyi,Shamsi Vuai Nahodha,Mohamed Jafar Jumanne Mohamed Hijja Mohamed,Issa Suleiman Nassor.

Wengine ni Prof.Makame Mnyaa Mbarawa,Mwatum Mussa Sultan,Haji Rashid Pandu,Abdulhalim Mohamed Ali,Jecha Salum Jecha,Dk.Khalid Salum Mohamed,Rashid Ali Juma,Khamis Mussa Omar,Mmanga Mjengo Mjawiri,Hamad Yussuf Masauni Mohamed Aboud Mohamed, Bakari Rashid Bakar,Mgeni Hassan Juma, Ayoub Mohamed Mahmoud,Hashim Salum Hashim,Fatma Kombo Masoud,Hasna Attai Masoud, Maalim Hamad Idd Hamad Idd,Pereira Ame Silima,Shaame Mcha,Mussa Aboud Jumbe na Moudline Cyrus Castico.


Jumanne, 30 Juni 2020

MHE.SAMIA AANZA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA KUSINI UNGUJA.


 MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja, katika ziara yake ya kuimarisha Chama,Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa SUZA Tunguu.
 WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa kusini Unguja,wakifuatilia maelekezo yanayotolewa na mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Samia Suluhu Hassan.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,amewasihi Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja kuendelea kuwa wamoja na kushikamana katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Dola mwaka huu.

Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na wajumbe hao huko katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA),amesema ushindi wa Chama Cha Mapinduzi utatokana na ushirikiano baina ya viongozi hao na wanachama wote.

Mhe.Samia alisema licha ya mkoa huo kuwa ngome ya Chama bado wanatakiwa kulinda heshima hiyo kwa kujipanga vizuri kuhakikisha Chama kinashinda.

"Nakuombeni tufanye kazi kwa mashirikiano makubwa kwani ushindi wa Chama chetu hautopatikana kwa maneno bali kwa juhudi za kila mmoja wetu", alisema Mhe.Samia.

Katika maelezo yake Mhe.Samia, aliwasihi wajumbe hao kufuata miongozo na kanuni za Chama wakati wa kufanya uteuzi wa wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi katika Mkoa huo.

Pamoja na hayo alikemea vitendo vya rushwa na makundi ya kukigawa kwani vitendo hivyo vinapelekea kupatikana kwa viongozi wasiokuwa na sifa za uongozi.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kupongeza mkoa huo kwa juhudi zao za kiutendaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kichama.

Alitoa pole kwa wananchi wa mkoa huo kwa kukumbwa na majanga mbali mbali yakiwemo ugonjwa wa corona pamoja na mafuriko na kuwasihi kuendelea kuchukua tahadhari.

Alisisitiza wananchi kuendelea kutunza mazingira ili kuepuka majanga mbali mbali yakiwemo mafuriko.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa huo Ramadhan Abdallah Ali,alimpongeza Mjumbe wa Kamati kuu Mhe.Samia kwa utendaji wake na kuwa karibu na mkoa huo kwa kutoa nasaha za kujenga Chama.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa huo Suleiman Mzee Suleiman,akisoma taarifa ya utekelezaji ya Chama kuanzia Januari hadi Machi 30 mwaka huu,alisema wamejipanga vizuri na watahakikisha wanashinda majimbo yote yaliyomo ndani ya mkoa huo.

Kupitia taarifa hiyo waliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Jumatano, 24 Juni 2020

FATMA KOMBO ACHUKUA FOMU YA KUOMBA RIDHAA YA URAIS WA ZANZIBAR.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Oganazesheni Cassian Gallos Nyimbo(kushoto), akimkabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Kada wa Chama Cha Mapinduzi Fatma Kombo Masoud(kulia),hafla iliyofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
HASNA ATTAI ACHUKUA FOMU YA URAIS ZANZIBAR

KADA wa CCM Hasna Attai Masoud aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM akionyesha mkoba wenye fomu za kuwania Urais wa Zanzibar, mara baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallos Nyimbo, hafla hiyo imefanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwsandui,Zanzibar.
MBIO za kusaka Urais wa Zanzibar zimeendelea leo Juni 24,2020 kada wa CCM Hasna Attai Masoud(40), amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Hasna, akiwa ni mwanamke wa pili kujitokeza katika kinyang’anyiro hicho amewasili katika Ofisi za Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar majira ya 4:00 asubuhi na kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallos Nyimbo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuwaamini na kuwapatia fursa mbali mbali za uongozi na utendaji wanawake nchini.

Amesema Dk.Shein, amekuwa ni kiongozi wa kuigwa katika kuthamini kundi la wanawake ambao kwa miaka mingi walikuwa hawana uwakilishi mkubwa katika nafasi mbali mbali za uongozi kama ilivyo hivi sasa.

“ Serikali ya awamu ya saba chini ya uongozi wa Rais wetu mpendwa Dk.Shein imewaona wanawake na kuwapatia nafasi kubwa ya kuongoza katika vyombo vya kufanya maamuzi, hivyo nasi tumehamasika sana nasi kuingia katika ushindani wa kuwania nafasi mbali mbali za uongozi”, amesema.


Kada huyo ambaye ni msomi wa shahada ya pili ya masuala ya usimamizi wa biashara, anakuwa ni wa 25 kuchukua fomu hiyo ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Jumanne, 23 Juni 2020

MWANAMICHEZO HASHIM SALUM ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS WA ZANZIBAR.

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hashim Salum Hashim leo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Kada huyo amewasili katika Ofisi za Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Kisiwandui Zanzibar majira ya saa 6:10 mchana na kupokelewa na maafisa wandamizi wanaoshughulikia mapokezi ya makada hao.

Hashim alikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallas Nyimbo, na kumtaka atafute wadhamini 250 wa Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu hizo Hashim, amesema endapo atapewa ridhaa na Chama atahakikisha kipaumbele chake ni kuimarisha sekta ya michezo nchini.

Amesema yeye ni mwanamichezo na amehudumu katika sekta hiyo kwa muda mrefu hivyo atahakikisha serikali inatoa  udhamini wa ligi kuu ya soka Zanzibar  kwa asilimia 100.

Amefafanua kuwa ligi hiyo inaendeshwa bila udhamini kwa muda mrefu toka kampuni ya Grand Malta isitishe udhamini wake mwaka 2013.

Ameongeza kwamba mbali na michezo pia ataendeleza maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 ya Serikali ya awamu ya saba chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

“Nampongeza Rais wetu Dk.Shein kwa kasi yake ya kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo endelevu hasa katika sekta za afya,elimu, miundombinu ya umeme na barabara, maji safi na salama pamoja na sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii”,amesema.

Pamoja na hayo kada huyo ambaye ni mtumishi wa SMZ katika Idara ya Mazingira amesema ataimarisha maendeleo katika Nyanja za kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya wananchi wote.


MOHAMED HIJA AREJESHA FOMU YA KUOMBA URAIS


 KADA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mohamed Hija amerejesha fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, na kumkabidhi Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazeni CCM Zanzibar Cassian Gallos Nyimbo.


RASHID, MASAUNI,RC AYOUB NA BHAA NAO WAJITOSA MBIO ZA URAIS ZNZMAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni baadhi ya wanachama waliochukua fomu, kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya urais wa Zanzibar.

Wa kwanza aliyefika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui baada ya kufunguliwa ofisi hizo saa 2:00 asubuhi ni Mwakilishi wa Jimbo la Amani, Rashid Ali Juma (54).

 Alikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Idara ya Oganaizesheni, Cassian Gallos Nyimbo ambaye alimtaka kutafuta wadhamini 250 katika mikoa mitano ya Unguja na Pemba.

 Akizungumza na waandishi wa habari, Juma ambaye ni mchumi katika masuala ya kodi akiwa mwanzilishi wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), aliipongeza CCM kwa kuweka utaratibu mzuri katika uchukuaji wa fomu, kwa kutoa ruhusa kwa kila mwanachama kutumia demokrasia yake.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, aligombea jimbo la Amani na kuibuka na mshindi na kuteuliwa na Rais Dk Ali Mohamed Shein kuwa Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni na baadaye kuhamishiwa katika Wizara ya Kilimo,Maliasili, Mifugo na Uvuvi. Mwingine aliyefika kuchukua fomu ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yussuf Masauni aliyeambatana na mkewe. Masauni ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Alikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya CCM, Gallos Nyimbo. Akizungumza na waandishi wa habari, Masauni alisema akipewa ridhaa kuongoza Zanzibar, atahakikisha anaendeleza mambo yote mazuri, yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar, Dk.Shein na Rais John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa na wahujumu wa uchumi. ‘’Leo mimi sina cha kusema kwa waandishi wa habari...lakini nikipewa ridhaa ya kuongoza nchi nitahakikisha nafuata nyayo za watangulizi wangu na Rais Shein katika mapambano dhidi ya rushwa na wahujumu uchumi,”alisema.Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Khamis Mussa Omar alijitokeza na kuchukua fomu kuomba ridhaa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar.

Mussa ni msomi wa masuala ya kodi na amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa miaka 14 sasa.

Pia aliwahi kuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2002. Ni miongoni mwa waanzilishi wa Mamlaka ya Uwekezaji nchini (ZIPA) mwaka 2005-2006. 

 ZIPA ndiyo iliyoweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta mbalimbali, ikwemo uwekezaji wa hoteli za kitalii. ‘’Nimechukua fomu kuomba ridhaa ya nafasi ya urais wa Zanzibar, lakini si kwa gharama yoyote na sitanuna kama sitachaguliwa kushika wadhifa huo,’’alisema.

 Mwingine aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa kupeperusha bendera ya CCM ni Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Majawiri.Mjawiri alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SUZA). ‘’Nimejitathmini kwa makini sana kwa kuzingatia kauli ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Magufuli kwa wale wanaokusudia kuchukua fomu na ndiyo maana nimechukua fomu hii,’’alisema Mjawiri, ambaye ni Mwakilishi wa jimbo la Mkoani katika kisiwa cha Pemba. Waziri mwingine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) aliyechukua fomu ya ni Mohamed Aboud Mohamed, anayeongoza Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, inayoratibu shughuli mbalimbali ikiwemo za Muungano.

Aboud amechukua fomu ya urais wa Zanzibar huku akisema “Hatukuja kushindanishwa wagombea katika kinyang’anyiro hicho.

Nimekuja kuchukua fomu kwa ajili ya kutekeleza demokrasia pana katika Chama Cha Mapinduzi” alisema.Mwingine aliyechukua fomu ni kada wa CCM ambaye ni Mhadhiri wa vyuo mbalimbali nchini, Bakari Rashid Bakari (56).

Alikipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa kufungua milango ya kuchukua fomu na kuweka mazingira mazuri kwa kila mwanachama wa chama hicho mwenye sifa na uwezo.


Mwingine aliyechukua fomu ya CCM kuwania urais wa Zanzibar ni Hussein Ibrahim Makungu maarufu kama ‘’Bhaa’’.

Aliahidi kufanya mambo makubwa yenye maslahi kwa wananchi wa Zanzibar, ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 ‘’Nimefurahishwa na demokrasia iliyotukuka ndani ya Chama cha Mapinduzi, yenye kutoa fursa kubwa kwa kila mwanachama mwenye sifa na uwezo,’’alisema.

 Kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari, Hussein alizuru kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Shehe Abeid Amani Karume.

Hussein ni Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni. Kabla ya hapo alikuwa mwakilishi wa Jimbo la Bububu huku akiwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitia nafasi tano za Baraza la Wawakilishi.

 Mtu mwingine aliyechukua fomu ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohammed.