Jumatano, 7 Oktoba 2020

KUMEKUCHA BUMBWINI, DK.MWINYI KUMWAGA SERA, DK.SHEIN KUWATAMBULISHA WAGOMBEA.


MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika kiwanja cha skuli ya Bumbwini kwa ajili ya Mkutano wa kampeni za CCM ambao mgeni rasmi ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein,  Wilaya ya Kaskazini 'B' Mkoa wa Kaskazini Unguja 

BAADHI ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa kundi la hamasa wakiburudisha kwa kuimba nyimbo mbalimbali katika mkutano huo wa kampeni za CCM.


VIONGOZI mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa wamekaa jukwaa kuu wakisubiri mgeni rasmi awasili kwa lengo la kuanza kwa mkutano huo wa kampeni za CCM.


MAELFU ya Wana CCM na wananchi kwa ujumla wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya skuli ya Bumbwini kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kampeni za CCM za kuwanadi,kuwatambulisha na kuwaombea kura za ndio  wagombea wa CCM kwa ngazi za Urais wa Zanzibar na jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge, Wawakilishi,madiwani na wagombea kupitia viti maalum.

Mkutano huo ni miongoni mwa mwendelezo wa kampeni za CCM zinazofanyika nchini na kuhudhuriwa na wananchi wengi.

Kupitia mkutano huo mgeni rasmi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, atawatambulisha  na kuwaombea kura za ndio wagombea wote wa CCM.

Pia Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi ataomba kura na kueleza kwa kina sera na vipaumbele vyake ili wananchi wa wilaya ya kaskazini 'B' wafanye maamuzi sahihi ya kuchagua wagombea wanaotoka katika chama chenye sera zinazotekelezeka.

tutaendelea kupata taarifa mbalimbali kupitia blog hii,,,,,,

Imeandaliwa na Kitengo cha Habari Afisi Kuu CCM Zanzibar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni