Ijumaa, 27 Januari 2017

WanaCCM wajitokeza kwa wingi katika kufanya Usafi maeneo ya Darajani Mjini Zanzibar. leo 28/1/2017

 




































MKUTANO NA WANDISHI WA HABARI




UTANGULIZI:

ASSALAM ALEYKUM, 

Ndugu Wandishi wa Vyombo mbali mbali vya Habari.
Awali ya yote, napenda nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu, ardhi na vyote viliomo ndani yake, kwa kutujaalia uzima na afya njema. Aidha, nachukua nafasi hii kwa mara nyengine tena kuwashukuru nyinyi waandishi wa vyombo mbali mbali kwa kukubali wito wetu na kuhudhuria kikao hiki.

Ndugu wandishi wa Habari.
Mnafahamu fika kwamba kila ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari ya kila mwaka, Chama Cha Mapinduzi huwa kimo katika vuguvgu la kuadhimisha kuzaliwa kwake tangu vyama vya TANU na ASP vilipoungana na kuunda Chama kimoja (CCM) tarehe 5, Februari 1977 tukio ambalo lilifanyika katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.



Ndugu wandishi wa Habari.
Sasa Maadhimisho hayo yatafanyika katika ngazi za Mikoa, na tayari kila Mkoa umeshaandaa ratiba za shughuli mbali mbali ambazo watazifanya katika Mikoa yao.
Shughuli hizo ni kama zifuatazo:-
Kutakuwa na zoezi la Usafi wa Mazingira katika maeneo ya Mikoani, Wilayani, Majimboni, Matawini na Maskani za CCM.
1.  Shughuli za kukagua Wagonjwa na kuwafariji Wazee wasiojiweza.
2. Kutakuwa na Mikutano Mikuu ya Ngazi mbali mbali.
3.  Mikutano ya Kamati za Siasa.
4.  Mikutano ya Halmashauri  Kuu za Jimbo.
5.  Zoezi la kupanda miti  katika maeneo mbali mbali ya kijamii  na vyanzo vya Maji.
6.  Kutakuwa na michezo ya aina mbali mbali kama vile  mashindano ya resi za baiskeli, michezo ya nage, michezo ya Bao, Mpira wa Basketboli pamoja na    Mpira wa Miguu.
7.  Makongamano yatakayoelezea historia ya CCM, mafanikio ya miaka 40 ya CCM pamoja na Utekelezaji wa  Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2015 – 2020.

Ndugu Wandishi wa Habari.
Pamoja na mambo yote hayo tuliyoeleza lakini pia yanaweza kujitokeza mengine ambayo hayakutajwa katika taarifa hii, lakini Mikoa watayafanya katika kuadhimisha kuzaliwa kwa CCM kwani mwaka wote huu wa 2017 ni mwaka wa kuadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa kwa Chama hicho.

Ndugu Wandishi wa Habari.
Mwisho naomba kutoa wito kwa Wana CCM wote kushiriki kwa wingi katika Mikoa yao kuadhimisha siku hiyo muhimu ya kuzaliwa kwa Chama chetu cha CCM. Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinawashukuru kwa dhati kabisa Wana CCM na Wananchi wote wa Jimbo la Dimani pamoja na Kata za  Mikoa ya Tanzania Bara iliofanya Uchaguzi  kwa kupiga kura kwa amani na utulivu mkubwa hatimae kukichagua kwa kishindo kikubwa  Chama Cha CCM, kwa kujua kwamba CCM ndio kimbilio la wanyonge na ni Chama kinachotekeleza Ilani yake ya Uchaguzi kwa makini na kwa wakati.

Baada ya maelezo hayo, nikushukuruni tena kwa kunisikiliza na nikutakieni kila la kheri katika majukumu ya kazi zenu.
Ahsanteni sana.

“KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI”

CCM Z'BAR YAWAPONGEZA WANANCHI WA JIMBO LA DIMANI

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewaahidi Wananchi wa Jimbo la Dimani na maeneo mengine nchini kuwa kitasimamia Serikali Kuu Kuhakikisha inatekeleza  kwa vitendo ahadi zote walizoahidiwa wananchi hao.

Ahadi hiyo imetolewa na  Katibu wa Idara Maalum ya NEC, Itikadi na Uenezi Zanzibar wakati akitoa Pongezi kwa Wafuasi wa CCM na Wananchi wa Jimbo la Dimani kupitia taarifa kwa vyombo vya habari hapo Ofisi kwake Kisiwandui Zanzibar.

Alisema Chama hicho kimejengwa katika misingi ya ukweli na uwazi katika utekelezaji wa ahadi zake kwa umma hivyo ni lazima kiisimamie serikali kwa kuikumbusha utekelezaji wa ahadi ambazo hazijafanyiwa kazi kwa baadhi ya maeneo.

Kupitia Taarifa hiyo aliwapongeza kwa dhati Wanachama wa Chama hicho na wananchi kwa ujumla jimboni humo kwa kuonyesha imani na mapenzi makubwa juu ya CCM hatua iliyofanikisha ushindi kwa Juma Ali Juma aliyepata kura 4,860 na kumshinda mpinzani wake kutoka CUF, Abdulrazak Khatib Ramadhan aliepata kura 1,234.

 Katika Uchaguzi huo wapiga kura walikuwa 6, 172 kati ya wapiga kura 9,275 waliojiandikisha katika Daftari la Wapiga kura Jimboni humo.

Alisema ushindi wa mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi huo umekuwa mkubwa kuliko ule wa uchaguzi wa mwaka 2015, ishara inayotoa matumaini ya kuwa wananchi wa jimbo hilo wanaendelea kuiunga mkono CCM.

Aliwapongeza viongozi na  watumishi wa CCM Zanzibar kwa ngazi mbali mbali waliosaidia kwa njia moja ama nyingine kufanikisha uchaguzi huo.

Pia alisifu juhudi zilizofanywa na vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kulinda Amani na Utulivu katika maeneo yaliyofanyika Uchaguzi ndani ya jimbo hilo kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo lakini wamesaidia kulinda  amani kwa ufanisi mkubwa.

Waride alisema ushindi huo umetokana na sera na mipango endelevu vinavyotekelezwa na chama hicho kwa vitendo katika maeneo mbali mbali nchini hasa katika Jimbo la Dimani.

“ Siri ya ushindi wetu ni ukweli, utu na kusimamia misingi ya haki bila ya ubaguzi vinavyofanywa na viongozi wa CCM kwa kuwatumikia wananchi wetu bila ubaguzi.

Pia Mgombea wetu alikuwa na vigezo vyote vya kuwa kiongozi wa jimbo hilo kutokana na sifa zake za utendaji unaoambatana uadilifu katika kutekeleza ahadi anazotoa kwa jamii.”, alifafanua Waride na kuwataka viongozi, watendaji na Wana CCM kuendelea kujipanga kikamilifu katika Chaguzi zingine zijazo.

Aidha aliahidi kuwa CCM itasimamia kikamilifu viongozi wake wanaotokana na ridhaa za Wananchi hasa Wabunge, Wawakilishi na Madiwani ili waweze kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2015/2020  kwa mujibu wa mahitaji halisi ya wananchi.

Akizungumzia tathimini ya CCM katika Uchaguzi huo alisema umefanyika katika mazingira yaliyokuwa  huru na Kidemokrasia kwa kuzingatia maelekezo na masharti ya NEC yaliyotolewa kabla ya kuanza zoezi hilo.

Alisema licha ya kuwepo kwa kasoro ndogo ndogo zilizoundwa na wafuasi wanaosadikiwa kuwa wa Chama Cha CUF kwa nia ya kuvuruga uchaguzi huo kwa baadhi ya maeneo lakini Vyombo vya ulinzi vimetekeleza wajibu bila kusababisha vurugu.

Uchaguzi huo uliofanyika Juzi kwa lengo la kuziba nafasi ya Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani marehemu Hafidh Ali Tahir aliyefariki akiwa mbungeni Dodoma mwaka jana, hatimaye limepata mrithi wake kutoka ndani ya CCM.

Jumapili, 22 Januari 2017

UCHAGUZI DIMANI

UCHAGUZI DIMANI TUKIMUONA MGOMBEA WETU NDUGU JUMA ALI JUMA AKIJUMUIKA NA WANANCHI KWENDA KUPIGA KURA.

EWE MOLA MJALIE KILA LA KHEIR NDUGU JUMA ALI JUMA AWEZE KUIBUKA NA USHINDI KATIKA UCHAGUZI HUU