Jumatano, 11 Januari 2017

MAKAMBA AULIZA KUNANI DIMANI?


Mhe. Januari Makamba amewauliza wananchi na wanachama wa CCM kunani Dimani? Swali hilo aliwauliza wakati akihutubia wananchi walifika hapo Dimani Misufini katika Mkutani wa Hadhara alipokuwa akihutubia mnamo 10/01/2017.

Aliwauliza iweje wapinzani wasusie Chaguzi za marudio zilizopita kwa vile wao hawaitabui Serikali na leo hii kuwa wamejitokeza kifua mbele katika Uchaguzi wa Dimani.

Hivyo aliwataka wananchi na wanachama kuwa wajitokeze kwa wingi kwenda kumchagua Ndugu Juma Ali Juma mnamo tarehe 22 januari 2017,  kwani kufanya hivyo ni kuiweka nchi hkatika hali ya usalama zaidi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni