Jumamosi, 7 Januari 2017

CCM YAENDELEA NA KAMPENI ZAKE FUONI KIBONDENI.





Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Dimani Unguja wametakiwa  kuendele kufuata sheria na Katiba ya nchi ili uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uweze kufanyika kwa Amani na Utulivu.
Rai hiyo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai katika mwendelezo wa kampeni za chama hicho huko Fuoni Kibondeni.

Amesema Chama hicho ni kinara wa ustaarabu hivyo wanachama wake wanatakiwa kudumisha utamaduni huo kwa vitendo.

Vuai amewaomba wafuasi wa CCM na wananchi kwa ujumla katika jimbo hilo kumchagua mgombea wa chama hicho Nd.Juma Ali Juma ili aweze kuwaletea .
Alieleza kwamba kumchagua mgombea wa chama hicho ni kuendeleza juhudi za maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo na nchi kwa ujumla.

Amesema Mgombea huyo ana uzoefu na sifa zinazokubalika ndani ya chama na serikali zitakazomuwezesha kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo.
" Wakati wa uzinduzi wa kampeni zetu katibu mkuu wa CCM alitupa Ilani ya CCM na katiba ambavyo ndio muogozo wetu katika uchaguzi huu.

Pia nakuombeni wananchi mmchague Juma Ali Juma ili aweze kukutumikieni kwa vitendo."alisema Vuai.
Aliyekuwa mgombea mwenza katika uchaguzi wa kura za maoni na kushika nafasi ya pili Abdallah Sheria amemuombea kura mgombea huyo na kuwataka wafuasi wa CCM katika jimbo hilo kumchagua ili aweze kuwaletea maendeleo.

Kwa upande wake Mgombea huyo Juma Ali Juma amesema endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo ataweza kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho kwa ufanisi.
Ali amevitaja vibaumbele vyake kwa wananchi hao kuwa ni pamoja na kuwatengenezea miundombinu ya barabara, usafiri, afya, kuanzisha vikundi

Vya ujasiriamali pamoja na kununua boti za kisasa ili vijana waweze kujiajiri wenyewe.
Hata hivyo amesema kipaumbele vingine ni elimu pamoja na  kunzisha mafunzo ya kilimo kwa njia za kisasa ili wakaazi wa eneo hilo wapate chakula cha uhakika.

Katika kampeni hizo zimeudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi Tanzania, Nagma Giga, Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini, Bora Afya Silima, Mwenyekiti wa Mkoa Magharib Kichama Yussuf Mohamed Yussuf pamoja na Naibu Mgeni Hassan Juma.























Hakuna maoni:

Chapisha Maoni