Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Sufiani Khamis akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo Elekezi kwa viongozi na Watendaji wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mjini. |
Jumapili, 31 Machi 2019
MMATUKIO KATIKA PICHA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MAGHARIB AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI YA JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA AMANI.
MANISPAA YA MAGHARIB 'B' YAAHIDI NEEMA KWA VIJANA, YASIFU UZALENDO WA UVCCM JIMBO LA M/KWEREKWE.
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR
VIJANA nchini wameshauriwa kuanzisha vikundi vya usafi wa mazingira ili wanufaike na fursa zilizowazunguka katika mazingira wanayoishi zikiwemo kujiajiri wenyewe kupitia vikundi hivyo.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa ya Magharibi 'B' Ali Abdalla Said Natepe mara baada ya kukamilika zoezi la Usafi katika soko la Mwanakwerekwe Zanzibar.
Amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakilalamikia changamoto ya ukosefu wa ajira hali ya kuwa bado hawajatumia vizuri fursa za ajira hasa zile zilizowazunguja zikiwemo za kufanya usafi na masuala mbali mbali ya ujasiriamali.
Amesema Manispaa ya Magharibi 'B' ipo tayari kufanya kazi na vijana kwa kuwapatia nyenzo za kufanyia kazi zikiwemo vifaa vya usafi pamoja na ruzuku ndogo ya kujikimu ili washiriki katika harakati mbali mbali za kusafisha maeneo mbali mbali ya manispaa hiyo.
Amebainisha kuwa endapo vijana hao wa UVCCM wataunda vikundi rasmi vinavyotambulikana kisheria uongozi wa Manispaa hiyo utahakikisha unawapa ushirikiano kwani kundi la vijana ndio nguvu kazi ya Taifa.
Katika maelezo yake Mkurugenzi huyo Natepe, ameeleza kuwa dhana ya vijana kujiajiri wenyewe kupitia vikundi vya usafi imeasisiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud anayeagiza vijana waunde vikundi kisha wapewe nyenzo za kufanyia kazi, lakini bado muamko wa kundi hilo ni mdogo na hauridhishi.
Mkurugenzi huyo, amewashukru wadau mbali mbali wakiwemo wanachana na viongozi wa UVCCM na CCM kwa kushiriki katika zoezi muhimu la ujenzi wa taifa la kufanya usafi katika soko la Mwanakwerekwe sehemu inayotumiwa na wananchi wote kutafuta riziki zao za kujikimu kimaisha.
Ametoa wito kwa wananchi kufanya usafi wa kina katika maeneo wanayoishi kwani mvua za masika zimeanza kunyesha hali inayotakiwa jamii kuchukua tahadhari juu ya maisha yao hasa katika suala zima la kutunza mazingira.
Akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ased Nyonje, amesema CCM itaendelea kuwa Taasisi bora ya kisiasa kwani wanachama wake wakikuwa wakitekeleza kwa vitendo falsafa ya ujamaa na kujitegemea kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii.
Amewataka vijana kufanya kazi kwa juhudi kubwa hasa kushiriki katika matukio muhimu ya ujenzi wa Taifa ili CCM iendelee kuaminiwa na jamii hatimaye ifikapo mwaka 2020 wananchi waichague kwa kura nyingi CCM ibaki madarakani.
Naye Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa kupitia Mkoa wa Magharib kichama Kassim Hassan Haji, ameeleza kuwa vijana wa UVCCM wamekuwa mstari wa mbele katika kushiriki katika masuala mbali ya kijamii kwa nia ya kuwasaidia wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Jimbo la Mwanakwerekwe Fatma Ramadhan Hussein amesema zoezi hilo la usafi ni sehemu ya kampeni ya kizalendo ya AMSHA AMSHA inayoratibiwa na Vijana wa Jimbo hilo kwa lengo la kuwahamasisha vijana wenzao na jamii kwa ujumla kushiriki katika masuala ya ujenzi wa Taifa.
Akizungumza Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Taifa, Zahoro Saleh amesema usafi ni jambo muhimu katika maisha ya mwanadamu hivyo wananchi wanatakiwa kutekeleza zoezi hilo katika maeneo yao bila ya kushurutishwa.
Ameeleza kuwa kutokana na umuhimu wa usafi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amekuwa akihimiza jamii ijenge utamaduni wa kuweka mazingira ya nchi katika hali ya usafi hadi serikali ikaamua kutenga siku za kila mwisho wa mwezi kufanyika usafi nchi nzima.
Fatma a meongeza kuwa kampeni hiyo inaambata na upandishaji wa Bendera za CCM katika maskani na maeneo mbali ya Mabalozi wa CCM,kuzindua madarasa ya Itikadi, kuwatembelea wazee na watu wenye mahitaji maalum sambamba na kupokea wanachama wapya wenye nia ya kujiunga na CCM pamoja na Jumuiya zake ili wanufaike na Siasa zenye Tija.
Naye mshiriki katika zoezi hilo Jamila Hamza amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele kufanya usafi katika mazingira wanayoishi kwani ni wadau muhimu wa maendeleo ya kijamii.
Aidha amesema suala la usafi ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwani ni sehemu muhimu ya masuala ya Afya ya jamii.
MATUKIO KATIKA PICHA KAMPENI YA 'AMSHA AMSHA' UVCCM JIMBO LA MWANAKWEREKWE TAREHE 31/03/2019.
MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita akizungumza na Vijana wa Jimbo la Mwanakwerekwe mara baada ya kuhitimisha kampeni ya AMSHA AMSHA katika maeneo mbali mbali ndani ya Jimbo hilo. |
KATIBU wa CCM Jimbo la Mwanakwerekwe Ramadhan Fatawi Issa akizungumza na Vijana wa UVCCM wa Jimbo hilo. |
MJUMBE wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Zahor Saleh akizungumza na vijana hao huko Tawi la CCM Mwanakwerekwe 'B'. |
MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita akiwatunuku cheti kwa vKatibu wa UVCCM wa Jimbo la Mwanakwerekwe Ali Vuai Abdalla 'Ali Mbunge' akiwa ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kampeni hiyo. |
MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita akitoa Cheti kwa Katibu wa Hamasa wa UVCCM Jimbo la Mwanakwerekwe. |
MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita Pamoja na vijana na viongozi mbali mbali wa CCM na jumuiya zake katika kampeni ya AMSHA AMSHA. |
VIJANA wa UVCCM wa Jimbo la Mwanakwerekwe wakipandisha bendera ya CCM katika Tawi la CCM Magogoni Kidatu. |
VIJANA wa UVCCM wa Jimbo la Mwanakwerekwe wakitoa zawadi kwa Mzee Adnani ikiwa ni sehemu ya kuwasaidia Wazee na Waasisi wa Chama Cha Mapinduzi. |
VIJANA wapya wa Darasa la Itikadi katika Jimbo la Mwanakwerekwe wakisikiliza kwa makini nasaha za viongozi mbali mbali wa UVCCM |
MKURUGENZI wa Baraza la Manispaa ya Magharib ‘B’ ndugu Ali Abdallah Said Natepe akizungumza mbele ya Vijana wa UVCCM mara baada ya kukamilisha zoezi la Usafi wa mazingira katika soko la Mwanakwerekwe. |
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ased Nyonje akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo. |
MJUMBE wa Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Magharibi Ndugu Kassim Hassan Haji |
MSHIRIKI wa zoezi la Usafi katika soko la Mwanakwerekwe kutoka UVCCM Ndugu Jamila Hamza |
Jumamosi, 30 Machi 2019
MHE.RAMADHAN: ATAKA USAFI WA MAZINGIRA UPEWE KIPAUMBELE JANG'OMBE, MHE.SAID ATAJA MIKAKATI YA MANISPAA YA MJINI.
MKURUGENZI
wa Manispaa ya Mjini Unguja (wa tatu kutoka kushoto),Mwakilishi wa Jimbo la
Jang’ombe Mhe.Ramadhani Hamza Chande(wa Nne kutoka kusho),Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib(wa pili kutoka kushoto), Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa
wa Mjini Kamaria Nassor (wa kwanza kushoto) wakikabidhi mfuko wa Sabuni ya
kufulia nguo na vifaa vya usafi Katibu wa Hospitali ya Kidongo Chekundu Bi.Bhai
Ibrahim mara baada ya kukamilika zoezi la usafi wa mazingira. |
VIONGOZI wa UVCCM Wilaya ya Mjini wakifanya Usafi katika Chumba cha Wagonjwa Wanawake wenye matatizo ya Akili katika Hospitali ya Kidongo Chekundu. |
VIONGOZI
mbali mbali wa CCM,UVCCM na Baraza la Manispaa wakifanya usafi katika Jengo la
kupumzikia Wagonjwa wa kiume wa matatizo ya Akili katika Hospitali ya
Kidongo Chekundu. |
VIJANA wa UVCCM wakifanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidongo Chekundu Zanzibar. |
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
WANANCHI wa Jimbo la Jang’ombe wametakiwa kufanya Usafi wa Mazingira mara kwa mara ili kuepuka madhara yanayosababishwa na uchafu yakiwemo maradhi ya miripuko.
Rai hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe Zanzibar Mhe.Ramadhan Hamza Chande katika shughuli ya kufanya usafi katika Hospitali ya Matibabu ya Wagonjwa wa Akili ya Kidongo Chekundu Zanzibar.
Amesema kila mwananchi ana jukumu la kufanya usafi katika mazingira anayoishi kwa kuhakikisha yanakuwa safi muda wote kwa lengo la kuepuka maradhi yakiwemo kipundupindu,kichocho na malaria.
Ameeleza kuwa lengo la kufanya usafi katika eneo hilo la hospitali ni kutoa msaada wa kijamii wa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum ambao ni wagonjwa wa akili wanaohitaji huduma muhimu za kijamii zikiwemo zikiwemo kuishi katika mazingira safi.
Ameongeza kuwa zoezi hilo la usafi ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 iliyoainisha utekelezwaji wa mambo mbali mbali katika sekta ya Afya ikiwemo usafi na ulinzi wa mazingira.
Katika maelezo yake Mwakilishi huyo Ramadhan, amebainisha kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu na kutekelezwa kwa hatua mbili ambazo hatua ya kwanza ni kutoa elimu kwa jamii na hatua ya pili ni kuhamasisha wananchi wafanye usafi kwa hiari.
“Naomba wananchi watambue na kuamini kuwa ‘usafi’ ni tabia hivyo tubnatakiwa kuweka safi mazingira yetu na yale wanayoishi watu wenye mahitaji maalum ili nao waishi kwa amani,utulivu na usalama wa afya zao kama wanavyoishi watu wengine.”,amesema Chande.
Ameshauri Serikali kupitia Baraza la Manispaa ya Mjini kuhakikisha wanasimamia Sheria ndogo ndogo za ulinzi wa usafi wa mazingira ili watu wanaochafua mazingira watozwe faini za papo kwa papo kwa lengo la kubadilisha jamii kitabia kutambua umuhimu wa kulinda mazingira.
Ametaja mikakati ya Jimbo la Jang’ombe katika kusimamia suala la usafi alifafanua kuwa wana mipango ya kuanzisha mashindano ya kuimarisha usafi katika shehia zote za jimbo hilo kwa kila shehia kuipatia zawadi ili kuhamasisha jamii kusafisha mazingira wanayoishi.
Akizungumza katika zoezi hilo Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa ya Mjini Mhe.Said Juma Ahmada, amesema Baraza hilo linasimamia shughuli za usafi katika maeneo mbali mbali ili kuhakikisha Mji unakuwa Safi na unaoendana na hadhi ya Zanzibar.
Amewambia wananchi hao kuwa wanatakiwa kuheshimu sharia za Manispaa kwa kuhakikisha maeneo ya mjini yanakuwa safi muda wote ili kurejesha sifa ya Zanzibar ya kuwa mjini safi na wenye watu wastaarabu katika kulinda na kutunza mazingira yaliyowazunguka.
Amesema lengo la Manispaa hiyo ni kufikia kiwango cha Mji wa Zanzibar kutajwa katika miji Safi, Kimataifa, Kikanda na Kitaifa kama inavyotajwa miji baasdhi ya Miji ya Tanzania bara fano Arusha na Mwanza.
Amesema kupitia mipango endelevu iliyowekwa na Manispaa hiyo mji wa Zanzibar utakuwa miongoni mwa orodha ya miji safi Duniani kwani baadhi ya maeneo wananchi wameanza kuelimika.
Katika maelezo yake Mkurugenzi huyo, amesema Baraza hilo linaendelea kutekeleza kwa ufanisi Ilani ya CCM kwa kuviwezesha vikundi mbali mbali vya kijamii vinavyofanya shughuli za usafi wa mazingira kwa kuvipatia misaada mbali mbali ya vifaa ikiwa ni sehemu ya kurejesha faida ya mapato yanayokusanywa na Manispaa kwa jamii.
“Nawapongeza sana UVCCM na CCM Jimbo la Jang’ombe kwa ubunifu wao wa kufanya usafi katika maeneo haya ya Hospitali ambayo ni sehemu muhimu kijamii kwani watu wanaoletwa kupatiwa matibabu katika maeneo haya wanatoka katika jamii zetu."amesema Said.
Aidha ametoa wito kwa Vijana mbali mbali katika Manispaa hiyo kuanzisha Vikundi rasmi vya usafi wa mazingira ili wapewe nyenzo za usafi na wanufaike na miradi ya usafi inayoratibiwa na Taasisi hiyo ili kuepuka kujiunga na vikundi viovu vinavyopelekea kuharibu maisha yao.
Amesema wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kubwa ya kuweka mazingira katika hali ya usafi hasa katika kipindi hichi cha mvua za masika ambacho,hujitokeza maradhi mengi yanayotokana na uchafu pamoja na kufanya usafi katika mitaro ya kusafirisha maji taka.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Jimbo la Jang’ombe, Ali Ahmad Ibrahim ‘Abeid’, amesema licha ya Chama Cha Mapinduzi kuwa Taasisi y Kisiasa kimeendelea kuwa mdau mkubwa wa kushiriki,kulinda,kutetea na kutoa miongozo ya uhamasishaji wa jamii kujenga utamaduni wa wananchi kuweka mazingira wanayoishi katika hali ya usafi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini, Kamaria Suleiman Nassor alisema suala la usafi halina itikadi za kisiasa bali linawahusu wananchi wote hivyo ni muhimu vijana wote kuungana na kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kwa kuhakikisha mazingira wanayoishi yanabaki salama.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mjini, Hudhaima Mbarouk Tahir amewashukru vijana na wadau mbali mbali walioshiriki katika zoezi hilo la usafi, kueleza kuwa huo ni mwanzo wa maandalizi ya shughuli za kijamii za Umoja huo katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Majimbo yote ya Wilaya hiyo.
Kwa upande wake Katibu wa UVCCM wa Jimbo hilo,Zainab Hassan King amesema jimbo hilo limejipanga kufanya shughuli mbali mbali za kimaendeleo zitakazoisaidia jamii zikiwemo masuala ya usafi.
Naye Katibu wa Hospitali ya Kidongo Chekundu, Bhai Ibrahim amewashukru wadau walioshiriki zoezi la usafi pamoja na kutoa msaada wa vifaaa vya usafi na kueleza kuwa wamesaidia kuweka katika hali ya usafi mazingira ya hospitali hiyo.
Zoezi hilo la usafi limetekelezwa na UVCCM na CCM Jimbo la Jang’ombe kwa kushirikiana na Baraza la Manispaa ya Mjini ambao wametoa mchango wa Vifaa mbali mbali vya Usafi katika Hospitali hiyo.
Alhamisi, 28 Machi 2019
MHE.NDUGAI ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MKOA KUSINI UNGUJA.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu Job Ndugai akiangalia ulazaji wa mipira katika mradi mkubwa wa Maji unaojengwa katika Kijiji hicho kwa lengo la kumaliza tatizo la maji safi na salama,katika ziara yake Mkoa wa Kusini Unguja. |
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Job Ndugai amesema ameridhishwa na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) ambao unaofanywa kwa upande wa maeneo ya visiwani humu.
Amesema kwa upande wake akiwa mlezi wa CCM wa mikoa ya Kaskazini Unguja na Kusini Unguja ameridhishwa na mipango ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) inavyofanywa katika maeneo ya Cheju na Chwaka ikiwemo katika kuhakikisha inawaletea maji na kuimarisha kilimo cha mpunga.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akitembelea maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kusini ambapo alisema katika upande wa kilimo amejionea mwenyewe kuwa serikali ya SMZ imeweka mipango mizuri ya kuhakikisha kiwango cha kilimo cha umwagiliaji kinaongezeka.
Alisema Serikali ya SMZ imeweka mpango mzuri kupitia mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha pamoja(PADEPU) wa zao la mpunga ambapo kilimo hicho kinatumia eneo dogo,mbegu ndogo kwa kuzalisha kiwango kikubwa cha zao hilo.
"Mpango huu ni mzuri kutokana na kuwa utawezesha Zanzibar kuwa na uwakika wa kujitegemea wa chakula cha mpunga na kuacha kuagiza kutoka nje ya visiwa hivi vya Zanzibar,"alisema
Katika maelezo yake alisema mbali na hatua hiyo,pia ameridhishwa na matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo unavyotumika kwa kufanya maendeleo makubwa katika maeeneo ya mkoa huo.
"Ninaomba uongozi wa CCM kufuatilia kwa karibu fedha za mfuko wa jimbo ili kujua namna fedha hizo zinavyotumika na kwamba haipendezi kuona fedha hizo zinatumika vibaya lakini ninardhishwa na utekelezaji wa mipango ya ilani ya CCM kwa SMZ na matumizi ya fedha za jimbo,"alisema Spika Ndugai.
Alisema kwa upande wa sekta ya maji Serikali ya SMZ inatekeleza vyema ilani ya uchaguzi kwa kuhakikisha wananchi wa maeneo ya jimbo la Chwaka wanapata maji safi na salama ya uwakika kutoka katika kisima cha Bambi.
"Ninaomba utandikaji wa bomba za maji katika maeneo ya Chwaka ambao ni urefu wa kilomita 7 umalizike kwa wakati ili wananchi hawa wapate maji kutokana na kuwa ni muda mrefu wamekuwa hawapati maji safi na salama na badala yake wamekuwa wakitumia maji ya chumvi hivyo kama CCM ilivyohaidi katika ilani yake hakuna haja ya kutekeleza kwa wakati,"alisema Ndugai
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo Maliasili na Uvuvi, Dk.Makame Ali Ussi alisema katika mradi huo wa PADEPU unatarajia kuwezesha Zanzibar kuongeza kiwango cha shughuli za kilimo cha umwagiliaji wa zao la mpunga ambapo katika mradi huo kutakuwa na visima 44 vya maji kuhakikisha maji ya kutosha yanakuwepo.
Alisema hatua hiyo ni sehemu ya ilani ya uchaguzi ya ibara 72 kifungu C ambapo CCM inaelekeza serikali ya SMZ kuongeza hekta 1500 za uzalishaji wa kilimo cha mpunga katika maeneo ya visiwani humu ikiwemo Cheju.
"Tunaendelea na mpango huu wa kuongeza kiwango cha shughuli za kilimo cha umwagiliaji ambapo mpaka sasa katika kipindi cha miaka 10 tumeweza kupiga hatua kubwa ya kuongeza uzalishaji wa kilimo cha umwagiliaji cha mpunga,"alisema
Aliongeza kuwa Serikali ya SMZ itaendeleza mapinduzi ya kilimo cha umwagiliaji kwa kipindi chote kama ilivyokuwa katika mipango yake na ya Chama tawala.
Jumatano, 27 Machi 2019
MHE.NDUGAI: AANZA ZIARA YAKE MKOA KASKAZINI UNGUJA,ATAKA USHINDI WA MAJIMBO YOTE 2020.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Job Ndugai akiwahutubia Wanachama na Viongozi wa Mkoa huo katika ziara yake ya kujitambulisha katika Mkoa. |
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MLEZI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kichama ndugu Job Ndugai, amewataka Wana CCM wa Mkoa huo kutambua kuwa njia pekee ya kulinda Mapinduzi ya mwaka 1964 ni kuhakikisha CCM inashinda na kubaki madarakani kwa kila Uchaguzi wa Dola.
Amesema kila mwanachama atumie nafasi yake kuhakikisha CCM inaendelea kustawi kisiasa, kiuchumi na kijamii na kukubalika kwa wananchi wote.
Kauli hiyo ameitoa katika ziara yake ya kujitambulisha na kuimarisha Chama katika Mkoa huo anaoulea akiwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.
Amesema suala la ushindi wa CCM sio mzaha bali ni jambo linalotakiwa kupewa kipaumbele kwa lengo la kulinda heshima,hadhi na urithi uliotukuka wa Waasisi wa Muungano na Mapinduzi ya mwaka 1964.
Ameeleza kitendo cha CCM kukosa jimbo moja la uchaguzi ni sawa na kusaliti juhudi za viongozi waliokomboa nchi kutoka kwenye kiza cha ukoloni,utumwa,udhalilishaji na kuiweka katika mwaka wa maendeleo,mafanikio chini ya falsafa ya ujamaa na kujitegemea.
Amewataka viongozi waliopewa dhamana na CCM katika Mkoa huo wafanye kazi kwa bidii na kuufuta upinzani ndani ya eneo hilo ambalo ni ngome ya CCM.
Ndugai ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema hatokuwa tayari kufanya kazi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa mkoa huo ambao watakuwa wazembe katika ulezi wake.
Amesisitiza kuwa katika ulezi wake hatoweza kukubali kufanya kazi na wanachama hao na kwamba atakuwa mkali zaidi.
Mlezi huyo amesema kuna baadhi ya watu hao wamekuwa wakibebwa huku wakishindwa kufanya kazi ipasavyo ya kuisaidia chama na hatimaye kusababisha kuangusha utendaji wa CCM katika maeneo ya mkoa huo.
Amesema katika nafasi yake ya kuwa mlezi atahakikisha anaendelea kuimarisha mkoa huo wa Kaskazini kuwa ngome ya CCM ili kushika nafasi za ngazi za udiwani,ubunge na uwakilisha.
Amefafanua kuwa kwa upande wa Wabunge na Wawakilishi ambao wanatoka katika maeneo ya mkoa huo wanapaswa kutekeleza hadi za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM na kwamba kufanya hivyo ndio njia pekee ya kuirejesha CCM madarakani.
Spika Ndugai amesema hata hivyo jukumu la utekelezaji wa hadi ya ilani ya uchaguzi linahitaji ushirikiano wa karibu na wanachama pamoja na kamati za wajumbe wa CCM kupitia Baraza la Wawakilishi na kamati za wajumbe wa CCM kupitia Bunge.
Amesema historia ya Zanzibar itakuwa na manufaa kwa vizazi vijavyo endapo watu viongozi wa sasa watafanya mambo ya maendeleo yenye kuacha alama bora ya uongozi wenye tija.
Katika maelezo yake,Ndugai amewasihi Wazazi na walezi wa Mkoa huo kujenga utamaduni ya kuwaruhusu vijana wao wachangamkie fursa mbali mbali za kimaendeleo zilizopo katika maeneo mbali mbali ya Tanzania bara na Afrika mashariki.
Amewataka baadhi ya viongozi na wanachama ambao bado wanaendekeza makundi yasiyofaa ya kukigawa chama waache tabia hiyo na badala yake washikamane kuleta maendeleo endelevu ndani ya taasisi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Mkoa huo Iddi Ali Ame amesema kaskazini ni ngome ya CCM na kwamba watahakikisha hawapotezi jimbo hilo kuanzia ngazi ya udiwani,Uwakilishi hadi Ubunge.
Amewataka wanachama wa Mkoa huo wanapaswa kuwa mstari wa mbele kwa kukijenga chama na kwamba kuna mambo mengi yameaidiwa katika kutatua kero mbalimbali za wananchi.
"Bado tunasafari ndefu tunatakiwa tukiimarishe chama kwa vitendo katika kutatua kero za wananchi na mambo tulioyahaidi katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015,"alisema
Jumatatu, 25 Machi 2019
MHE.NDUGAI: ATUA ZANZIBAR KWA ZIARA YA SIKU MBILI KICHAMA.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Mhe,Job Ndugai akizungumza na Viongozi mbali mbali wa CCM Zanzibar. |
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Ndugu Job Ndugai,amewataka Wanachama na Viongozi wa CCM Visiwani Zanzibar kuendeleza harakati za kuandaa mazingira rafiki ya kukipatia ushindi Chama mwaka 2020.
Rai hiyo ameitoa mara baada ya kuwasili leo Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kutembelea Mikoa miwili ya kichama ambayo ni Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mkoa wa Kusini Unguja.
Mhe.Ndugai ambaye ni Mlezi wa Mikoa hiyo,amesema kila mwanachama anatakiwa kujipanga kuhakikisha CCM inaendelea kubaki madarakani kwa ridhaa ya wananchi.
Katika maelezo yake Ndugai, amewashukru viongozi na wanachama wa CCM wa Mikoa hiyo kwa mapokezi makubwa jambo aliloeleza kuwa hali hiyo imemuongezea ari,hamasa na ujasiri wa kufanya ziara yake ufanisi mkubwa.
Amewasisitiza wanachama wa Mikoa hiyo kuendeleza sifa na heshima ya maeneo yao yanayosifika kwa kuwa ngome imara za Chama Cha Mapinduzi.
Aidha Ndugai ameeleza kuwa CCM inaendelea kuimarika Kisiasa, Kiuchumi, Kidemokrasia na kimfumo huku baadhi ya vyama vya siasa vikiendelea kudhoofika kisera na kisiasa.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, amemhakikishia Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa hali ya kisiasa katika Mikoa anayoilea ipo shwari kutokana na historia nzuri ya maeneo hayo ambayo ndio yenye azna kubwa ya mtaji wa kisiasa wa CCM.
Amesema kuwa jukumu la ulezi wa Mikoa ni kubwa hivyo anaamini kuwa Mhe.Job Ndugai atafanya atafanya ziara yake hiyo ya kujitambulisha kwa wanachama pamoja na kuwapatia nasaha mbali mbali za kuwaongezea hamasa ya kuendelea kuwa wazalendo wa CCM na Taifa kwa ujumla.
Ziara hiyo ya Mhe.Ndugai ni ya siku tatu atatembelea maeneo mbali mbali na kuzungumza na wanachama kupitia vikao vya ndani sambamba na kukagua miradi iliyotekelezwa kupitia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.
MATUKIO KATIKA PICHA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM MHE.JOB NDUGAI KUWASILI Z'BAR KWA ZIARA YA KICHAMA YA SIKU MBILI.
VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa Bandarini Malindi baada ya kumpokea Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Job Ndugai aliyewasili Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kutembelea Mikoa ya Kaskazini Unguja na Kusini Unguja. |
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Job Ndugai akizungumza na Viongozi mbali mbali wa CCM Zanzibar katika ukumbi wa Afisi Kuu Kisiwandui. |
KATIBU Msaidizi wa CCM Zanzibar Ndugu Asha Mohamed Chum(aliyevaa mtandio mweusi) akitoa maelezo ya sehemu ya Historia alipouwawa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume. |
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. |
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Job Ndugai pamoja na Viongozi mbali mbali wa CCM wakisoma Dua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, lililopo Kisiwandui Zanzibar. |
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Job Ndugai akibadilisha mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi katika eneo la Kisiwandui. |
Jumapili, 24 Machi 2019
DK.MABODI: AVIONYA VYAMA VYA SIASA VINAVYOHATARISHA AMANI, MHE,JAMAL AKABIDHI GARI LA MILIONI 29.5.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Magomeni kupitia Mkutano wa Ndani wa CCM. |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaonya baadhi ya Viongozi wa kisiasa wanaotumia vibaya uhuru wa kidemokrasia kuhatarisha hali ya amani ya nchi.
Kimewataka viongozi wa siasa wa chama cha ACT-Wazalendo na CUF kutotumia mipasuko na migogoro ya ndani ya vyama vyao kuhatarisha hali hiyo ya amani na kwamba wazanzibar na Watanzania hawapo tayari kuingia katika machafuko ya kisiasa kwa sababu ya maslahi binafsi ya watu wachache.
Onyo hilo limetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Sadala 'Mabodi',wakati akizungumza katika Kikao cha ndani kilichoambatana na hafla ya kukabidhi gari la aina ya basi kwa uongozi wa Jimbo la Magomeni mjini Unguja lililotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Jamal Kassim Ali.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema CCM haina muda wa kushughulikia sera za vyama vingine na kwamba itaendelea kusimama imara na kupaza sauti inapoona baadhi ya watu wachache wanavunja sheria za nchi kwa makusudi bila ya kujali misingi ya utu na haki za binadamu.
Ameongeza kuwa mpasuko wa kisiasa ulioko baina ya viongozi wa CUF na ACT-Wazalendo baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF,Seif Sharif Hamadi kufukuzwa ndani ya chama hicho na kujiunga na ACT-Wazalendo ambapo imeshuhudiwa namna wa wafuasi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakifanya vitendo vya uvunjifu wa sheria kwa makusudi.
Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa wanachama wa ATC-Wazalendo wamefanya uharibifu wa mali za chama cha CUF ikiwemo kuchoma nguo za chama hicho,bendera, kung'oa samani zilizoko katika Ofisi mbali mbali sambamba na kutumia dini katika harakati za Chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema mambo yote hayo ni ishara za wazi zinazochochea vurugu na migogoro baina ya wanachama wa vyama hivyo viwili, zinazoweza kuingiza nchi katika athari kubwa ya machafuko.
Hata hivyo,Dk.Mabodi amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuchukua hatua stahiki mapema, kwani dhana ya hali ya amani na utulivu wa nchi haviuzwi katika maduka kama bidhaa bali imeletwa na sera bora za CCM.
Amesema nchi zilizoingia katika machafuko ya kisiasa na vita vya wenyewe kwa wenyewe zilianza taratibu huku Taasisi na Mamlaka zenye dhamana ya ulinzi na usalama zikipuuza kuchukua hatua katika hali hizo na badala yake mataifa hayo yamejikuta yakingia katika vita hivyo kwa kipindi cha muda mrefu.
Naibu huyo Katibu Mkuu aliongeza kuwa CCM itaendelea kushindana kwa sera za maendeleo na kuwapelekea wananchi mahitaji muhimu ya msingi na si kujiingiza katika siasa za ubabe na uharibifu wa mali za umma.
"Wito wangu kwa viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nchini tuwaongoze na kuwaelekeza mambo mema wanachama wetu, kwa kuwajengea mazingira ya kuamini ushindani wa sera na badala ya Siasa za Ovyo na machafuko", amesema Naibu Katibu Mkuu.
Katika maelezo yake Dk.Mabodi amemsihi Msajili wa Vyama vya siasa nchini, kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha Chama kinachovunja Sheria na Katiba za nchi na ambavyo vikienda kinyume na masharti ya usajili wa Vyama vya Siasa wachukuliwe hatua za kisheria.
Pia, amemtaka Msajili huyo wa vyama vya siasa kuwa anatakiwa kufanya uhakiki wa michango ya fedha za wahanga wa mafuriko Zanzibar zilizokuwa zikichangishwa na viongozi wa CUF chini ya Seif Sharif Hamad na kutolewa ufafanuzi wa kina juu ya matumizi yake kama ziliwafikia walengwa.
Amesema kwamba kuna baadhi ya vyama vya siasa nchini vinajiendesha kupitia mifumo haramu ya ufisadi, utapeli na migogoro kwa lengo la kukidhi maslahi ya watu wachache ambao ni viongozi wa ngazi za juu za vyama hivyo.
Dk.Mabodi amesema vyama vya aina hiyo havitakiwi kupewa nafasi wala kuaminiwa na wananchi kwani haviwezi kuwakilisha na kusimamia maslahi ya wanachama wao badala yake wanajinufaisha wenyewe.
Naibu Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kupuuza kauli za Seif Sharif Hamad za kudai kuwa migogoro ya vyama vyao inachochewa na Serikali jambo ambalo si kweli bali anaendeleza ulaghai na Siasa za fitna.
"Niwaweke wazi kwamba mfumo wa siasa za ujamaa na Kujitegemea ndio chimbuko la maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwani, unawawezesha wananchi kujikomboa katika hali ya umaskini uliokithiri na kuwa katika hali ya maendeleo na kujitegemea wenyewe kiuchumi na kijamii,"amesema Dk.Mabodi
Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM, aliwapongeza Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wa Jimbo la Magomeni Unguja kwa kasi kubwa ya kutatua kero za wananchi ndani ya Jimbo hilo na maeneo yake.
Dk.Mabodi amesema kuwa kibali cha kuirejesha CCM madarani mwaka 2020 ni kutekeleza ahadi zote zilizoahidiwa katika uchaguzi wa mwaka 2015 na kwamba kila kiongozi wa Serikali na Chama anayejua kuwa amepewa dhamana ya kutimiza dhamira hiyo wanapaswa kutekeleza kwa wakati ahadi hizo.
Amewataka baadhi ya Wabunge,Wawakilishi ambao wanashindwa kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi wanapaswa kutambua kuwa CCM haitokuwa haibu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kwamba itatoa fursa kwa watu wanaotekeleza ilani na miongozi ya CCM kwa vitendo.
"Leo tunakumbushana tu kuwa wananchi wanahitaji maendeleo sio porojo hivyo kama wewe unajijua upo Serikali au katika Chama na tulikupa dhamana ya kuwatumikia wananchi na hukutekeleza dhamana hiyo, basi ujue kuwa utang'oka utake usitake.", amesema.
Dk.Mabodi ametoa agizo kwa viongozi wa majimbo nchini wakiwemo Wabunge na wawakilishi kufanya mikutano ya ndani ya kuwaeleza wana-CCM na wananchi kwa ujumla utekelezaji wa ilani unaofanywa na Serikali ili waone mafanikio yaliyofikiwa katika nyanja za kijamii,kichumi na kisiasa.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Magomeni,Jamal Kassim Ali, amesema basi hilo limegharimu sh.milioni 29.5 ni miongoni mwa sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kuwaondoshea kero za usafiri wananchi wa jimbo hilo.
Amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ametatua kero za ukosefu wa maji safi na salama kwa kuchimba visiwa tisa ambavyo vinatoa huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya Shehia zote za Jimbo hilo.
Mbunge huyo ameongeza kuwa kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Jimbo hilo wameanzisha kituo cha mafunzo ya amali kinachotoa mafunzo ya ujasiriamali na ufundi kwa vijana wa jimbo hilo.
Amesema sakata la Seif Sharif Hamad kufukuzwa ndani ya CUF, inatokana na dhambi zinazomtafuna za usaliti,uchu wa madaraka pamoja na visasi na chuki.
"Kwani alidai kusema kuwa yeye anaongoza mapambano ndani ya CUF inayofuata falsafa za mfumo wa Kiliberali ili kuin'goa CCM inayofuata mfumo wa Kijamaa aliodai umepitwa na wakati,"ameeleza.
Jamal amesema kuwa anashangaa kumuona kiongozi huyo aliyetamba kwa mbwembwe na kukashifu mfumo wa ujamaa anajiunga na ACT-Wazalendo kinachofuata mfumo huo wa ujamaa.
"Mimi nawambia wananchi hasa ambao bado ni mateka wa kifkra kwa Seif kuwa waamke na kujikomboa na utumwa wa mwanasiasa huyo wajiunge na CCM kwani hajali maisha ya watu bali anajali maslahi yake."amesema Jamal.
Naye Mwakilishi wa Jimbo hilo,Rashid Makame Shamsi amesema kuwa ameshiriki katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya jimbo kwa kununua vifaa vya samani vya ofisi na kukarabati Ofisi za Makatibu wa matawi ya chama yalioko katika Jimbo hilo.
Amesema katika kutatua changamoto ya usafiri siku za hivi karibuni amenunua gari aina ya Fuso kwa ajili ya shughuli mbalimbali za wananchi wa jimbo hilo na kwamba amechimba visima na kusambaza mipira ya maji.
Mwakilishi huyo amesema kuna ushirikiano mkubwa kati yake viongozi wenzake wakiwemo Mbunge na Madiwani wa Jimbo hilo katika shughuli mbalimbali za maendeleo ili kumaliza changamoto za wananchi wa jimbo hilo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)