Jumamosi, 23 Machi 2019

MATUKIO KATIKA PICHA DK.MABODI AKIKABIDHI GARI MILIONI 29.5 LILILOTOLEWA NA MBUNGE WA MAGOMENI MHE.JAMAL KASSIM ALI.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi(wa kwanza kushoto), Mbunge wa Jimbo la Magomeni Unguja Mhe.Jamal Kassim Ali(wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mhe.Rashid Shamsi wakikata utepe kuashiria mabidhiano rasmi ya Gari ya Jimbo hilo yenye Thamani ya Shilingi Milioni 29.5 iliyonunuliwa na Mbunge Mhe.Jamal kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo hilo.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akiendesha Gari hiyo aina ya Basi kwa ajili ya kuikabidhi rasmi kwa Uongozi wa Jimbo la Magomeni Unguja ambalo ni miongoni mwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM Zanzibar.

 Picha ya Basi lililotolewa na  Mbunge wa Jimbo la Magomeni Unguja Mhe.Jamal Kassim Ali ikiwa ni mwendelezo wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo hilo kwa kuwaondoshea wananchi usumbufu wa usafiri na huduma mbali mbali za Kijamii.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akiwa na Viongozi mbali mbali wa Jimbo la Magomeni katika hafla ya kukabidhi Gari kwa Uongozi wa Jimbo hilo.

  NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akiimba nyimbo za hamasa pamoja na vijana mbali mbali(hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi Gari ya Jimbo hilo.

 VIONGOZI mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake wakiwa katika Hafla hiyo.

 MBUNGE wa Jimbo la Magomeni Unguja Mhe.Jamal Kassim Ali akizungumza namna alivyotekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa kuimarisha huduma mbali mbali za Kijamii,Kisiasa na Kiuchumi.

 MWAKILISHI wa Jimbo la Magomeni Unguja akizungumzia na kuainisha miradi ya maendeleo aliyoitekeleza kupitia  Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 katika Jimbo hilo. 
 KATIBU wa CCM Mkoa wa Mjini Ndugu Mohamed Nyawenga akizungumza katika hafla hiyo.

 KATIBU wa CCM Wilaya ya Amani Ndugu Ali Salum Suleiman akizungumza katika hafla hiyo.

 MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Ndugu Nadra Mohamed akiwasihi Vijana kuwa wamoja na wenye msimamo usioyumba katika kulinda Amani na Utulivu wa Nchi.

 MWAKILISHI Mstaafu wa Jimbo la Magomeni Unguja Bi.Hafsa Said akitoa salamu za Wazee wa Jimbo hilo kupitia hafla hiyo ya kukabidhi Gari.

   NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar katika hafla ya kukabidhi Gari la Jimbo.

  MBUNGE wa Jimbo la Magomeni Unguja Mhe.Jamal Kassim Ali (kushoto), akimkabidhi  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi  Kadi ya umiliki wa Gari hilo la CCM pamoja na Ufunguo.

   NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akionyesha wananchi wa jimbo la Magomeni Kadi pamoja na ufunguo wa Gari.

   NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM wa Jimbo la Magomeni Unguja Ufunguo na Kadi ya Umiliki wa Gari.

   NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akisalimiana na Wanachama wa CCM walioshiriki katika Hafla hiyo.

 BAADHI ya Viongozi wakiwa katika hafla hiyo.

 

 MBUNGE wa Jimbo la Magomeni Unguja Mhe.Jamal Kassim Ali akimtuza fedha Msanii wa Ngoma ya Asili ya Kibati waliotumbwiza katika hafla hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni