Jumatatu, 25 Machi 2019

MHE.NDUGAI: ATUA ZANZIBAR KWA ZIARA YA SIKU MBILI KICHAMA.


MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Mhe,Job Ndugai akizungumza na Viongozi mbali mbali wa CCM Zanzibar. 

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Ndugu Job Ndugai,amewataka Wanachama na Viongozi wa CCM Visiwani Zanzibar kuendeleza harakati za kuandaa mazingira rafiki ya kukipatia ushindi Chama mwaka 2020.

Rai hiyo ameitoa mara baada ya kuwasili leo Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kutembelea Mikoa miwili ya kichama ambayo ni Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mkoa wa Kusini Unguja.

Mhe.Ndugai ambaye ni Mlezi wa Mikoa hiyo,amesema kila mwanachama anatakiwa kujipanga kuhakikisha CCM inaendelea kubaki madarakani kwa ridhaa ya wananchi.

Katika maelezo yake Ndugai, amewashukru viongozi na wanachama wa CCM wa Mikoa hiyo kwa mapokezi makubwa jambo aliloeleza kuwa hali hiyo imemuongezea ari,hamasa na ujasiri wa kufanya ziara yake ufanisi mkubwa.

Amewasisitiza wanachama wa Mikoa hiyo kuendeleza sifa na heshima ya maeneo yao yanayosifika kwa kuwa ngome imara za Chama Cha Mapinduzi.

Aidha Ndugai ameeleza kuwa CCM inaendelea kuimarika Kisiasa, Kiuchumi, Kidemokrasia na kimfumo huku baadhi ya vyama vya siasa vikiendelea kudhoofika kisera na kisiasa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, amemhakikishia Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa hali ya kisiasa katika Mikoa anayoilea ipo shwari kutokana na historia nzuri ya maeneo hayo ambayo ndio yenye azna kubwa ya mtaji wa kisiasa wa CCM.

Amesema kuwa jukumu la ulezi wa Mikoa ni kubwa hivyo anaamini kuwa Mhe.Job Ndugai atafanya atafanya ziara yake hiyo ya kujitambulisha kwa wanachama pamoja na kuwapatia nasaha mbali mbali za kuwaongezea hamasa ya kuendelea kuwa wazalendo wa CCM na Taifa kwa ujumla.

Ziara hiyo ya Mhe.Ndugai ni ya siku tatu atatembelea maeneo mbali mbali na kuzungumza na wanachama kupitia vikao vya ndani sambamba na kukagua miradi iliyotekelezwa kupitia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni