MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania(UWT) Ndugu Gaudensia Kabaka akisalimiana na wanachama wa CCM katika shule ya sekondari Wara. |
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania(UWT) Ndugu Gaudensia Kabaka akikagua shule ya Sekondari Wara ambayo ni Utekeleaji wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2015/2020.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania(UWT) Ndugu Gaudensia Kabaka akizungumza na wanachama wa CCM mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya kisasa ya Wara katika Wilaya ya Chake Chake Pemba. |
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania(UWT) Ndugu Gaudensia Kabaka akichota udongo wa kujengea Tawi la CCM Kangani Wilaya ya Mkoani. |
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania(UWT) Ndugu Gaudensia Kabaka akijenga Tawi la CCM la Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba. |
MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwaiba Kisasi akijenga Tawi la CCM Kangani. |
KATIBU wa UWT Taifa Mwl.Queen Mlozi akijenga Tawi la CCM Kangani. |
NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Bara ndugu Jesca Mbogo akijenga Tawi la CCM Kangani. |
NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu akijenga Tawi la CCM Kangani. |
MBUNGE wa Viti Maalum Mhe. Munira Mohamed akikabidhi Fedha kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba. |
MBUNGE wa Viti Maalum Mhe.Faida Mohamed Bakari akichangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la CCM Kangani Pemba. |
NA IS-HAKA OMAR,PEMBA.
WANAWAKE wa Chama Cha Mapinduzi kisiwani Pemba wametakiwa kufanya Mapinduzi
ya kisiasa kwa kuhakikisha CCM inavunja na kusambaratisha ngome ya CUF na
hatimaye kushinda majimbo yote ya Uchaguzi ya mwaka 2020.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka katika
mwendelezo wa ziara yake huko Shule ya Sekondari ya Mohamed Juma Pindua Wilaya
ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, alisema ni wakati wa wanawake kuonyesha uwezo
wao na kutekeleza kwa vitendo falsafa ya 'Wanawake ni jeshi la ukombozi la
CCM'.
Amesema hakuna chama cha siasa, wala taasisi yoyote itakayoweza kuzuia
ushindi wa CCM mwaka 2020 kisiwani Pemba endapo wanawake wataamua kuungana kwa
pamoja ili kufanikisha ushindi wa CCM.
Katika maelezo yake Ndugu Gaudensia amesema Jeshi la UWT la Chama Cha
Mapinduzi litakuwa mstari wa mbele kupambana vita ya kisiasa kwa mbinu zote ili
kuandika historia mpya katika uwanja wa siasa za ushindani Tanzania kwa
kuhakikisha CCM inashinda kwa kiwango kikubwa Zanzibar na Tanzania bara.
“Wanawake tuna nguvu, uwezo, ujasiri, mikakati,nyenzo na mbinu za medali za
kisiasa hivyo hatuna sababu ya kuyaachia majimbo ya Pemba yaendelee kubaki kwa
wapinzani bali yatarudi mikononi mwa CCM.”,amesema Bi.Gaudensia.
Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia, amepongeza hatua za
kimaendeleo zilizofikiwa katika Sekta ya Elimu Pemba hasa katika suala zima la
miundombinu ya Majengo ya Kisasa ya kiwango cha Ghorofa.
Aidha ameyataja mageuzi makubwa katika miundombinu ya Barabara za kisasa mijini
na Vijiji kuwa ni ya kiwango bora cha kuridhisha hatua ambayo wananchi wa
kisiwa cha Pemba wanastahiki kuithamini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
mambo mema yaliyotekelezwa.
Pamoja na hayo amewasisitiza hakina Mama Visiwani Pemba bila kujali tofauti
zao za kisiasa kushiriki katika kongamano la Kitaifa litakalofanyika Machi 9
mwaka 2019, katika Kiwanja cha Tibirinzi Wilaya ya Chake Chake Pemba.
Ameeleza kuwa Kongamano hilo lililoandaliwa na UWT ni la kupongeza
utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 pamoja na masuala mbali
mbali ya kimaendeleo yaliyoasisiwa na Serikali za CCM kwa awamu tofauti za
Uongozi.
Pamoja na hayo amewapongeza Wabunge na Wawakilishi wa Viti Maalum Pemba kwa
kazi nzuri wanazozifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Naye Katibu Mkuu wa UWT Taifa Mwl.Queen Mlozi amekemea vitendo vya udhalilishaji
wa Kijinsia kwa Watoto wa Kike vinavyochangia kukwamisha maendeleo ya wanawake
katika kunufaika na fursa za elimu.
Mwl.Queen amewasihi Wazazi,Walezi pamoja viongozi wa dini na kisiasa
kusimamia ajenda za kulinda na kutetea haki za wanawake hasa vijana na watoto
ili wanufaike na fursa mbali mbali ndani ya jamii.
Akizungumzia changamoto za dawa za kulevya kwa vijana, Naibu Katibu Mkuu wa
UWT Tanzania bara Ndugu Jesca Mbogo amesema baadhi ya vijana kisiwani Pemba
wameingia katika changamoto za kutumia dawa za kulevya hali ambayo ni hatari
katika ustawi wa maendeleo ya nchi.
Mapema Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kusini Pemba, ndugu Bimkubwa Khamis
Mohamed ameelea kuwa hali ya kisiasa ndani ya mkoa huo imeendelea kuimarika na
wanawake wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kujiunga na CCM.
Amesema Pemba ya Sasa sio Pemba ya zamani kwani wananchi wengi wameanza
kutambua ukweli baada ya kuona kwa vitendo mambo mema yanayotekelezwa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayotokana na Chama Cha Mapinduzi.
Kupitia ziara hiyo jumla ya Wanachama Wapya 507 wamejiunga na UWT na kukabidhiwa kadi za uanachama watu 10 kwa niaba ya Wenzao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni