Jumatatu, 25 Machi 2019

MATUKIO KATIKA PICHA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM MHE.JOB NDUGAI KUWASILI Z'BAR KWA ZIARA YA KICHAMA YA SIKU MBILI.


 VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa Bandarini Malindi baada ya kumpokea Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Job Ndugai aliyewasili Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kutembelea Mikoa ya Kaskazini Unguja na Kusini Unguja.
 MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Job Ndugai  akizungumza na Viongozi mbali mbali wa CCM Zanzibar katika ukumbi wa Afisi Kuu Kisiwandui.
  KATIBU Msaidizi wa CCM Zanzibar Ndugu Asha Mohamed Chum(aliyevaa mtandio mweusi) akitoa maelezo ya sehemu ya Historia alipouwawa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume.

 MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
 MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Job Ndugai pamoja na Viongozi mbali mbali wa CCM wakisoma Dua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, lililopo Kisiwandui Zanzibar.

 MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Job Ndugai akibadilisha mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi katika eneo la Kisiwandui.
Hakuna maoni:

Chapisha Maoni