Jumamosi, 30 Januari 2016

CCM Zanzibar Kuazimisha Sherehe ya miaka 39 ya kuzaliwa kwake

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kesho kitaadhimisha sherehe ya miaka 39 ya kuzaliwa kwake, kwa kufanya mkutano wa hadhara ikiwa ni uzinduzi wa maadhimisho hayo. ke na maamamuzi ya Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani.
Kimesema kuwa maamuzi hayo ya kufanyika uchaguzi huo Machi 20 mwaka huu, yanaenda sambamba na matakwa ya wananchi waliokuwa wengi katika kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa mujibu wa miongozo ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu alisema kwamba CCM inaungana na vyama vingine vya kisiasa nchini vilivyobaini kasoro za uchaguzi mkuu uliopita kuwa na kasoro kwa kuunga mkono maamuzi ya ZEC kuwa ni sahihi kwani yamefuata hatua muhimu za Kikatiba.
Waride alisema msimamo wa CCM katika Mkwamo wa kisiasa uliopo Zanzibar ni kurudi katika uchaguzi wa marudio ili kila chama cha kisiasa kinachoriki katika uchaguzi uliopita kiweze kupata haki ya kungia madarakani kwa njia za halali na zinazokubalika kisheria.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo  Waride alieleza kwamba maamuzi hayo ndiyo kipimo sahihi cha kuweka uzani wa ukomavu wa kisiasa na demokrasia katika mfumo wa vyama vingi kwani lazima kila chama chenye haki ya kushiriki katika uchaguzi kiridhike na hatua zote zinazofanywa mpaka kupatikana kwa mshindi atakayekuwa anaongoza kwa wingi wa kura halali.
“ Tunachukua fursa hii kuwaomba wananchi wote wenye haki ya kupiga kura hasa wafuasi wa CCM pamoja na wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura  Machi 20 mwaka huu.
Tukumbuke kwamba maamuzi hayo yamefanywa na Chombo chenye Mamlaka ya kusimamia masuala yote ya Uchaguzi nchini baada ya kujiridhisha kuwa kuna kasoro zilizotokea katika uchaguzi uliofutwa na kuona kuna haja ya kila mwananchi kupata haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa njia huru, wazi na zinazokubalika kisheria”. Alifafanua Waride na kuongeza kuwa uchaguzi huo ndiyo njia mwafaka ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar.
Katibu huyo aliongeza kwamba pia wanaunga mkono msimamo wa vyama vya vyote vya kisiasa vilivyokubali kushiriki uchaguzi wa marudio pamoja ushauri wa Msajili wa Vyama vya Sisasa nchini , Frances Mtungi kwa kuvitaka vyama vyenye usajili kushiriki katika mchakato huo ili kudumisha Demokrasia na malengo na malengo ya vyama kutumia uchaguzi kushika Dola.
Akizungumzia suala la CUF kususia Uchaguzi wa marudio alisema kwamba walichofanya ni mwendelezo wa migomo na kususa kwa mipango  ya maendeleo inayofanywa na mamlaka za serikali katika kufanya mipango mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi.
Alisema kwamba upinzani wa aina hiyo hauna nia njema ya kujenga maendeleo ya nchi bali una nia malengo ya kukwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi kwa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoweka mbele tamaa ya madaraka kuliko maisha ya wananchi.

“ Kila chama kina sera zake na misimamo yake sasa wao kama wameona kususia uchaguzi wa marudio ndiyo njia ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar hiyo ni juu yao,  lakini sisi tutashiriki kikamilifu ili chama chetu kipate ridhaa ya wananchi kurudi madarakani ya kidemokrasia.

Aidha alisema  chama hicho kinaamini kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka 2015 ulikuwa na kasoro nyingi zilizosababisha uchaguzi huo kukosa sifa ya kuwa uchaguzi huru na wa haki na hatimaye kufutwa.

Kupitia taarifa hiyo Waride wamewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa mikoa minne kichama ya Unguja katika uzinduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM itakayofanyika katika  Afisi kuu ya CCM Kisiwandui, January 31 mwaka huu.

Alisema Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.

CCM Imeridhika na maamuzi ya Tume ya Uchaguzi, Zanzibar

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  kimeelezea kuridhishwa kwake na maamamuzi ya Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani.

                                          MWISHO.

Jumanne, 5 Januari 2016

WANACCM WAJITOKEZE KWA WINGI KATIKA UCHAGUZI WA MARUDIO PINDI TU TAREHE ITAKAPO TANGAZWA

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai kwa mara nyengine tena amewataka wanachama wa Chama hicho kujiandaa na hatimaye kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi  wa marudio, ili kukiletea ushindi wa kishindo chama hicho.
Aidha, amesisitiza haja kwa wanachama wote popote walipo kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha maadhimisho ya sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika Januari 12, mwaka huu, Mjini Unguja.

Ndugu Vuai ameyasema hayo leo hapo Afisi Kuu ya CCM alipokuwa akizungumza katika kikao maalum na Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC Zanzibar kilichojumuisha pia na Makatibu wa CCM wa Mikoa ya Unguja.

Amesema Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kinawataka viongozi, wanachama wa CCM na Jumuiya zake kujipanga kikamilifu na kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio na kuwachagua kuanzia Rais, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani wakati utakapowadia.

Aidha, ametumia nafasi hiyo kusisitiza haja kwa wana CCM na wanancho wapenda amani wote Unguja na Pemba kujitokeza kwa wingi kusherehekea maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo na siku ya kilele cha maadhimisho hayo.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar amewasihi  wananchi hasa wana CCM kuachana na propaganda potofu zinazofanywa na kuenezwa mitaani na wapinzani kwa  lengo la kuwagombanisha viongozi na wafuasi wa CCM na badala yake hawana budi kujishughulisha na mambo ya msingi kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa ujumla.

Ameyataja mambo hayo ya msingi kuwa kwanza ni kujiandaa na hatimaye kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa marudio mara baada ya kupangwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na pili kushiriki katika maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964.
Chama Cha Mapinduzi ni Chama imara, chenye heshima na kinachotambulika na kuheshimika ndani na nje ya Tanzania, hivyo wanachama wake katu hawatakubali kupokea propaganda potofu zinazopandikizwa na wapinzania kwa ajili ya kutaka kudhoofisha nguvu ya Chama hicho.

Akizungumzia kuhusu suala la CUF kutoshiriki katika sherehe za mwaka Mapinduzi  za mwaka huu kama ilivyodaiwa na Chama hicho hivi karibuni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar alisema kitendo hicho si jambo la ajabu miongoni mwa Jamii  ya Wazanzibari, kwani kwa vipindi tofauti  kadhaa huko nyuma  wamekuwa wakisusia sherehe hizo.

“Miaka  mingi huko nyuma kabla ya kuundwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa (SUK) Viongozi na wafuasi wa Chama hicho (CUF) walikuwa na kawaida sio tu ya kutoshiriki katika sherehe hizo, bali pia waliweza kususia hata vikao halali vya Baraza la Wawakilishi”. Alidai Naibu Katibu Mkuu huyo.

Amesema CUF kwa muda wote tangu kuasisiwa kwake, kimekuwa na kigugumizi kikubwa katika kuyatambua na kuyathamini Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoleta ukombozi wa kweli kwa wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba hali inayowafanya kuishi wakiwa watu huru ndani ya Taifa lao huru na kufaidika na matunda yatokanayo na Mapinduzi hayo.

Mara kadhaa wana CUF hasa viongozi waliomo ndani ya Serikali walidiriki kuwasilisha mawazo yao ya kutaka neno SMZ liondoshwe na lisitumike kabisa katika Serikali ya Zanzibar  mawazo ambayo yaligonga mwamba, hali inayodhihirisha kuwa CUF haitambui sembese kuthamini sherehe hizo na kinachofanyika sasa ni visingizio tu.

Jambo la msingi kwa jamii ya Wazanzibari  ni vyema wakaelewa kwamba ndani ya mioyo ya Wana CUF hawayatambui kabisa Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964 na mara kadhaa Viongozi wake wamekuwa wakisisika hadharani kupitia majukwaa ya kisiasa wakitaka Zanzibar iwe na Kumbukumbu za Uhuru bandia wa mwaka 1963.
 
Kwa mantiki hiyo basi, CCM kinawaomba wana CCM na wale wote ambao ni waumini wa kweli wa Mapinduzi ya Januari 12, 1964 popote walipo nchini, wajitokeze kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika sherehe za maadhimisho ya kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar huku wakiwaambia  wana CUF kwamba “wasitafute visingizio kwani hawana chembe ya Imani na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya 1964 na kwamba kushiriki ama kutoshiriki kwao hakutaathiri chochote sherehe hizo”.