NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala Mabodi amesema
kuwa hakuna Chama wala taasisi yoyote ya kisiasa inayoweza kuzuia Chama
hicho kisisimamie utekelezaji wa Ilani Uchaguzi ya mwaka 2015/2020 kwa
wananchi wa Visiwa vya Zanzibar.
Msimamo huo ameutoa katika mwendelezo wa ziara zake za kuimarisha uhai wa
Chama huko katika Kisiwa Cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini “A” kichama,
wakati akizungumza na wanachama, viongozi na watendaji wa CCM Wadi ya
Tumbatu Gomani.
Alisema kila jambo linalofanywa ama kutekelezwa na CCM lipo katika nyaraka
za kimiongozo na kisheria ambazo ni Katiba ya Chama, Ilani na miongozo ya
maadili na Uchaguzi tofauti na vyama vingine vya kisiasa vinavyoongozwa na
matakwa binafsi ya watu wachache.
Pia alisema misingi hiyo ndio chimbuko la Ukomavu wa kisisa na Demokrasia
iliyotukuka ndani ya CCM, na inawajengea ujasiri viongozi wa chama hicho
kusimama popote kujenga hoja imara za kuinada ilani ya chama kwani wanajua
kuwa hakuna wa kuzuia utekelezaji wake.
Mwanasiasa huyo ambaye amefanya ziara katika kisiwa hicho kidogo cha
Tumbatu kilichopo Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa
mara ya kwanza toka alipoteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni,
aliwasihi Wana CCM hasa wazee kuendelea kuwa karibu na taasisi hiyo ili
waweze kutoa ushauri na maoni yao juu ya masuala mbali mbali ya uongozi na
utendaji.
Alieleza kwamba Chama hicho bado kinaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi
zote zilizoahidiwa katika uchaguzi Mkuu uliopita bila ya kujali itikadi za
kisiasa, kidini na kikabila ili wananchi wote waweze kunufaika na matunda
ya serikali inayotokana na Chama Tawala.
Dkt. Mabodi aliwambia wananchi hao kwamba wanatakiwa kuthamini na kulinda
miradi mbali mbali inayotekelezwa na serikali kwani imetokana na nguvu zao
ambao waliichagua kwa kura nyingi CCM isimamishe serikali yenye maono na
utu wa kuwatumikia wananchi kwa vitendo.
Hata hivyo alifafanua kwamba CCM haina muda wa kurumbana na kushughulikia
hoja dhaifu za wapinzani na badala yake inaenda mbio kusimamia kuwakumbusha
viongozi na taasisi za umma zenye wajibu wa kushughulikia mipango ya
maendeleo na ustawi wa jamii, kuona inakamilika kwa wakati.
“ CCM ni chama kinachotokana na ASP na TANU vilivyokuwa vyama vya wakulima
na wakwezi na vikaikomboa nchi na kutuachia matunda haya, hivyo ni lazima
tuyalinde na kuyatetea kwa vitendo.
Pia puuzeni kwa nguvu zote uzushi na sera zizisokuwa na maana juu ya
maisha na maendeleo ya nchi, kwani hazina lengo la kutufikisha pale
tunapopataka zaidi ya kutugawa na ndio maana CCM inapinga kwa nguvu zote
dhana za migogoro na utengano.”alieleza Dkt. Mabodi na kuwataka wana CCM
kuendelea kulinda Amani na Utulivu wa nchi huku wakiendelea kufanya kazi
kwa bidii za kujiongezea kipato.
Akitoa ufafanuzi juu ya Uchaguzi wa Chama hicho unaoendelea kwa ngazi ya
Matawi kuchukua fomu aliwaagiza Makatibu na Manaibu Katibu wa Chama na
jumuiya zingine kuahakikisha wanafuata taratibu zilizowekwa ili kila mtu
mwenye nia ya kugombea apate nafasi hiyo.
“ Kama nikibaini kwamba kuna mizengwe ama makundi ya kutuharibia uchaguzi
ngazi yeyote kwanza watu tuliowapa majukumu watawajibu pia uchaguzi huo
nitawashauri wenzangu ikibidi ufutwe na kufanyika tena kwani tunahitaji
watu wenye uwezo na uchungu na chama”. Alisema Naibu katibu huyo.
Aliwataka wanachama kuhakikisha wanachagua viongozi wenye sifa na
wanaokubalika katika jamii ambao watajenga timu ya kukiletea ushindi na
heshima chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Haji Juma Haji
akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kwamba CCM imepitia katika
vipindi tofauti vya kiutawala
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni