MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), MH.SAMIA SULUHU HASSAN AMESEMA KUWA CCM NDIO CHAMA CHENYE MIZIZI YA ASILI YA KITANZANIA KWANI KIMETOKANA NA VYAMA VYA UKOMBOZI AMBAVYO NI TANU NA ASP.
KAULI HIYO AMEITOA WAKATI AKIZUNGUMZA NA KAMATI ZA SIASA ZA NGAZI ZA MATAWI HADI SIASA ZA MKOA WA KUSINI UNGUJA KICHAMA HUKO DUNGA, AMEELEZA KWAMBA HESHIMA HIYO ILIYOJENGWA NA WAASISI WA VYAMA HIVYO INATAKIWA KUENDELEZWA NA WANACHAMA WA SASA KWA KUHAKIKISHA CHAMA KINAENDELEA KUONGOZA DOLA KWA NJIA ZA KIDEMOKRASIA.
AIDHA MH.SAMIA AMBAYE PIA NI MAKAMO WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMESISITIZA UMOJA NA MSHIKAMANO BAINA YA WANACHAMA NA VIONGOZI WA NGAZI MBALI MBALI NDANI YA CHAMA NA JUMUIYA KWA UJUMLA, ILI KUENDELEZA DHANA YA SERIKALI KUJITEGEMEA YENYEWE BILA YA KUSUBIRI UFADHILI WA WAHISANI KUTOKA NJE.
MAPEMA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR, DKT.ABDALLA JUMA SAADALLA MABODI AMEAHIDI KUSIMAMIA IPASAVYO MCHAKATO WA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA HICHO ILI KILA MWANACHAMA AWEZE KUPATA HAKI YAKE KWA MUJIBU WA KATIBA NA MIONGOZO YA CCM.
SAMBAMBA NA HAYO AMEELEZA KUWA KATIKA MCHAKATO HUO HATORUHUSU KUFANYIKA VITENDO VYA KUPANGWA SAFU ZA MAKUNDI YA UONGOZI NA RUSHWA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni