|
MWENYEKITI wa Kikundi cha Hamasa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Ndugu Shaaban Ali Othman (kushoto) akimkabidhi Daktari dhamana Tamim Hamad Said(kulia) Friji mbili za kuhifadhi dawa za hospitali zilizotolewa na kikundi cha hamasa cha vijana wa Afisi Kuu CCM Zanzibar. |
|
MWENYEKITI
wa Kikundi cha Hamasa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Ndugu Shaaban Ali Othman (wa
pili kushoto) akizungumza mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Wilaya ya
Kaskazini ‘A’ Unguja, Daktari dhamana Tamim Hamad Said (wa kwanza kushoto)
pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Haji Machano Juma(wa kwanza
kulia) wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa na kikundi
cha hamasa.
|
|
KATIBU wa Kikundi cha Hamasa cha Afisi Kuu ya CCM Zanzibar ndugu Suleiman Mohamed Rashid (wa kwanza kushoto aliyesimama) akizungumza katika kikao cha hafla ya makabidhiano ya mafriji mawili yaliyotolewa na kikundi cha hamasa. |
|
KATIBU wa CCM Wilaya ya Kaskazini 'A' ndugu Haji Machano Juma akizungumza katika hafla hiyo. |
|
Daktari Dhamana wa Hospitali hiyo Tamim Hamad Said, akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya mafriji ya kuhifadhi dawa. |
|
Katibu Msaidizi wa Taasisi hiyo Ndugu Khamis Salum Abdi , akizungumzia mafanikio yaliyofikiwa na CCM. |
|
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ndugu Pandu Salum Sungura . |
|
BAADHI ya vijana wa kikundi cha hamasa cha Afisi Kuu ya CCM Zanzibar wakisikiliza kwa makini nasaha za viongozi mbali mbali wa CCM, UVCCM na Hospitali ya Wilaya Kivunge katika hafla ya makabidhiano ya Vifaa Tiba iliyofanyika leo Tarehe 30/01/2019 |
|
Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Kikundi cha Hamasa cha Afisi Kuu ya CCM Zanzibar pamoja na Uongozi wa Hospitali ya Wilaya Kivunge , Mkoa wa Kaskazini Unguja, mara baada ya hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba. |
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
VIJANA
mbali mbali nchini wameshauriwa kuendeleza utamaduni wa kujitolea katika
kuisaidia jamii katika masuala mbali mbali ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na
kimaendeleo.
Rai
hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Hamasa cha Afisi Kuu ya CCM
Zanzibar Ndugu Shaaban Ali Othman wakati akikabidhi Friji(Jokofu) mbili zilizotolewa
na kikundi hicho na kukabidhi Uongozi wa Hospitali ya Kivunge ya Wilaya
Kaskazini 'A' Unguja.
Amesema
vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kusaidia uhifadhi wa vifaa tiba vya
hospitali hiyo hasa dawa za matumizi ya binadamu zinazohitaji hali ya baridi
muda wote.
Ameutaka
uongozi wa Hospitali hiyo kuvitunza na kuvitumia katika matumizi yaliyokusudiwa
ili vitoe huduma endelevu kwa wananchi mbali mbali wanaofika hopitalini hapo
kwa ajili ya matibabu.
Pamoja
na hayo amebainisha kuwa vifaa hivyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na viongozi wa CCM ambao ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.John Pombe
Magufuli pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
wanaotekeleza kwa kasi mipango ya
maendeleo kwa maslahi ya wananchi wote.
Ameeleza
kwamba vijana nchini wana wajibu wa kutekeleza kwa vitendo masuala mbali mbali
ya kijamii kwa lengo la kuwasaidia wananchi wanaokabiliwa na changamoto katika
mazingira wanayoishi.
Katika
maelezo yake Mwenyekiti huyo Shaaban,amesema endapo vijana wa Zanzibar wataweka
mbele dhana ya uzalendo,umoja, mshikamano na kuelekezana mambo mema ya
kuisaidia jamii, itasaidia Zanzibar kuwa nchi bora zaidi duniani iliyopiga
hatua kubwa za kimaendeleo.
Awali
Katibu wa Kikundi hicho cha Hamasa, Suleiman Mohamed Rashid amefafanua kuwa
kikundi hicho kitaendelea kusaidia masuala mbali mbali ya kijamii katika maeneo
mbali mbali yaliyopo katika Wilaya zote za Unguja na Pemba.
Amesema
Chama Cha Mapinduzi kipo mstari wa mbele kushughulikia changamoto zinazoikabili jamii katika maeneo ya mijini na
vijijini.
Akizungumza
mara baada ya kupokea vifaa hivyo Daktari Dhamana wa Hospitali hiyo Tamim Hamad
Said, amesema uongoizi wa hospitali hiyo umefurahi kupokea vifaa hivyo kwani
vilikuwa ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya taasisi hiyo.
Dr.Tamim
ameahidi kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa hasa kuhifadhi dawa na vifaa
mbalimbali vinavyotumika katika matibabu ili wananchi wapate huduma bora za
Afya.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ndugu Pandu Salum
Sungura amesema vijana wa mkoa huo wapo imara katika kuunga mkono juhudi za
vijana wenzao wa kikundi cha hamasa kutoka Afisi Kuu ya CCM Zanzibar,
kilichoonyesha mfano bora wa kutoa vifaa hivyo kwa hospitali ili viwasaidie
wananchi wa Mkoa huo.
Akizungumza
katika hafla hiyo kwa niaba ya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, Katibu Msaidizi wa
Taasisi hiyo Ndugu Khamis Salum Abdi amesema Chama Cha Mapinduzi kinaendelea
kusimamia na kutekeleza Ilani yake ya Mwaka 2015/2020 kwa ufanisi mkubwa kwa
lengo la kumaliza kero zinazoikabili jamii.
Amesema
suala la kuwapelekea wananchi maendeleo halina itikadi za kisiasa hivyo kila
mwananchi, kikundi pamoja na taasisi yoyote wana wajibu wa kutatua changamoto
za wananchi.