Jumatatu, 7 Januari 2019

MATUKIO KATIKA PICHA MATEMBEZI YA UVCCM KUTOKA KANGANI KUELEKEA WAWI PEMBA.

VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) waliobeba Bendera za Taifa pamoja na picha za waasisi na viongozi wakuu wa Serikali za Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiendelea na matembezi ya kuenzi miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakitoka Wadi ya Kangani Wilaya ya Mkoani kuelekea Wawi Wilaya ya Chake Cheke Mkoa wa Kusini Pemba.

  NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akishiriki ujenzi wa Shule ya Msingi Chanjaani Kisiwani Pemba katika matembezi ya UVCCM ya kuenzi miaka 55 ya mapinduzi yaliyoambatana na utekelezaji wa shughuli mbali mbali za kijamii.

MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Mhe. Rashid Hadid (kushoto), Mwakilishi wa Viti Maalum Vijana Zulfa Mmaka (kulia) wakishiriki shughuli za ujenzi wa skuli ya msingi Chanjaani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
 VIJANA wa UVCCM wakiwa katika Matembezi ya kuenzi miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakitokea Wadi ya Kangani Wilaya ya Mkoani wakielekea Wadi ya Wawi Wilaya ya Chake Chake Pemba.



 IJANA wa UVCCM wakiwa katika Matembezi ya kuenzi miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar kisiwani Pemba wakiwa katika shughuli za ujenzi wa skuli ya Chanjaani Pemba.

 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanziubar  Mussa Haji Mussa akizungumza na CHAMA BORA TV mara baada ya ujenzi wa Skuli ya Chanjaani.

 MWAKILISHI wa Jimbo la Chake Chake Mhe. Suleiman Sarahani  Said akizungumza na CHAMA BORA TV juu ya mafanikio bali mbali yaliyofikiwa ndani ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni