Alhamisi, 31 Januari 2019

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU WA U.W.T Z'BAR NDG.TUNU JUMA KONDO ALIPOKUTANA NA MABARAZA YA WILAYA YA AMANI NA MJINI YA UMOJA HUO.


NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi UWT Zanibar Ndugu Tunu Juma Kondo akiwahutubia Wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya za Amani na Mjini za Umoja huo, ikiwa ni ziara yake ya mwanzo toka ateuliwe kushika nafasi hiyo na kujitambulisha pamoja na kupanga mikakati ya kuimarisha UWT.

 MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Mjini Ndugu Ghanima Sheha akizungumza namna Mkoa wake ulivyojipanga katika kusimamia maslahi na fursa za wanawake katika nyanja za kiuchumi,kisiasa na kijamii.

 KATIBU wa CCM Mkoa wa Mjini Ndugu Mohamed Nyawenga akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini Amani Unguja.

 KATIBU wa UWT Mkoa wa Mjini Ndugu Stahamili Omar akisoma risala ya Umoja huo mbele ya Naibu katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo katika hafla ya kujitambulisha.



NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi UWT Zanibar Ndugu Tunu Juma Kondo akikabidhi kadi za UWT kwa wanachama wapya wa Umoja huo.




 WANACHA wapya wa UWT wakila kiapo cha utii kwa kusoma ahadi za mwanachama wa CCM mara baada ya kukabidhiwa kadi hizo.



 KATIBU wa UWT Wilaya ya Mjini Ndugu Khadija Juma Khamis akisoma ratiba ya Hafla hiyo.

 BAADHI ya Wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya a Mjini na Amani za Umoja huo wakiimba kwa shangwe nyimbo mbali mbali za Chama na UWT.


 BAADHI ya Waasisi na Waanzilishi wa UWT wakiwa katika hafla hiyo.








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni