Jumapili, 6 Januari 2019

UVCCM YASEMA VYAMA VYA UPINZANI VITAKUFA KIFO CHA MENDE KABLA YA 2020.

 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndugu Mussa Haji Mussa akisoma taarifa ya Matembezi ya kuenzi miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar  kupitia hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Wilaya ya Mkoani Pemba.

 BAADHI ya Vijana wa UVCCM walioshiriki katika matembezi hayo ya kutoka Chokocho hadi Mkanyageni Pemba wakifuatilia kwa makini hotuba zinazotolewa na mgeni rasmi katika matembezi hayo.


 NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR. 

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Mussa Haji Mussa ametuma salamu nzito kwa wanasiasa waliofilisika Kisera na Kisiasa kuwa wajiandae kisaikolojia kwani vyama vyao vitakufa kifo cha Mende kabla ya mwaka 2020.

Alisema wanasiasa waliozoea kufanya kazi za kisiasa kwa kutegemea umaarufu wa maneno matupu na porojo zilizokuwa na chembe ya utekelezaji wa kivitendo wajipange kufanya kazi zingine na kujitoa katika uringo wa siasa za sasa kwani hawaendani nao. 

Alisema CCM kupitia jumuiya zake hasa UVCCM wamekusudia kuandika historia ya mageuzi makubwa ya kisiasa kwa kuanza na kazi ya kung'oa baadhi ya watu wanaojiita wapinzani visiwani Zanzibar  hasa Pemba. 

Aliongeza kwamba tayari wananchi wa visiwa hivyo wameendelea kuthamini na kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwa asilimia kubwa,kwani maendeleo yametekelezwa katika maeneo yote Mijini na vijijini. 

Naibu Katibu Mkuu huyo,anasema kwa sasa CUF haina tena sifa ya kuwa Chama cha kisiasa bali ni  kikundi cha wahuni wanaowalaghai wananchi kwa kauli za upotoshaji. 

"UVCCM tuna malengo mapana kwanza ya kuijenga kimuundo,kisiasa na Kiitikadi taasisi yetu ili vijana wanaotokana na Umoja wetu wawe wanachama,  viongozi na watendaji wenye  uzalendo uliotukuka kwa maslahi ya umma. "alisema Naibu Katibu Mkuu huyo. 

Matembezi hayo yalifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi ambapo zaidi ya vijana 400 wameshiriki matembezi hayo kutoka Chokocho hadi Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni