NA
IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
UMOJA
wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Tanzania kwa upande wa Zanzibar, leo
umezindua rasmi kamati ndogo ndogo nne zitakazokuwa na majukumu mbali mbali ya
kufanisha kwa ufanisi kazi za umoja huo kwa mwaka 2019/2020.
Akizungumza
mara baada ya uzinduzi huo Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi
amezitaja kamati zilizozinduliwa kuwa ni pamoja na Kamati ya Uchumi, Mipango na
Fedha, Kamati ya Mawasiliano kwa Umma, Kamati ya Elimu,Malezi na Mafunzo pamoja
na Kamati ya Mahusiano na Taasisi za Wanawake ndani na nje ya Nchi.
Amesema kuzinduliwa kwa kamati hizo ni matarajio makubwa zaidi ni kuwafikia
Wanawake na Vijana pamoja na makundi
mbali mbali yaliyopo katika jamii na watoto ili kushinda Uchaguzi ujao mwaka
2020.
Katika
maelezo yake Makamu Mwenyekiti huyo amewasisitiza Wajumbe wote wa Kamati hizo
kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika
utekelezaji wa majukumu ya msingi ya UWT pamoja na CCM kwa ujumla.
“Wanawake
ni Jeshi kubwa tena la ukombozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, nasaha zangu
kwenu ni kwamba tutumie nafasi hii kuhakikisha tunawafikia wanawake wote hasa
waliopo Vijijini na Pembezoni kwa nia ya kuwaweka karibu na kufanya nao
shughuli zetu za kisiasa.
Pia
Wanawake wa UWT lazima tupate Sauti zetu kila mmoja kwa nafasi yake ndani ya
Umoja Wetu kuyasema mambo mema yanayotekelezwa na CCM chini ya Viongozi wetu
Wakuu ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli wanaoendelea kusimamia kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2015/2020.”, amesema Makamu Mwenyekiti Thuwayba Kisasi.
Amewataka Wanawake nchini kushirikiana katika malezi ya Watoto ili waweze kukuwa wakiwa
katika malezi na maadili bora yatakayowasaidia kupambana na changamoto za
mmomonyoko wa maadili.
Awali
akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo , ameeleza kuwa UWT imejipanga kufanya kazi zake Kisayansi zaidi kwa lengo la kufanikisha
kwa wakati malengo waliyojiwekea ndani ya Umoja huo.
Aidha amesema Kamati hizo
zilizozinduliwa zitakuwa ni chachu ya kubuni miradi mipya ya kiuchumi
itakayoongeza kipato ndani ya UWT pamoja na kupatikana fursa ya mahusiano
mazuri na Taasisi mbali mbali za Wanawake Duniani.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Kamati tekelezaji WUT Taifa Ndugu Lucy Mwakembe amesema Umoja huo utaendelea kupanga
mikakati mbali mbali ya kimaendeleo ili kujiinua kiuchumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni