Jumamosi, 12 Januari 2019

MATUKIO KATIKA PICHA MAADHIMISHO YA MIAKA 55 YA MAPINDUZI-PEMBA.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, alipowasili katika viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba, kuhudhguria Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapungua Mkono Wananchi akiwa katika gari Maalum ya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, wakati akiingia katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwa Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea shatu ya Gwaride rasmin la maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliofadhimishwa kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Ali Mohamed Shein, akikagua Gwaride rasmin la Sherehe za Mapinduzi kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba. 


 ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, wakionesha jinsi ya uchezaji wa Gwarige la kimya, wakati wa Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Gombani.



 MKE wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehe Mzee Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume, Mke wa Rais Mstaaf wa Tanzania Mama Anna Mkapa na Mke wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Mama Shadya Karume, wakifuatilia Hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

 VIONGOZI mbali mbali wa Kitaifa wakiwa katika uwanja wa Gombani Pemba.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni