Jumapili, 10 Machi 2019

DK.MABODI ASEMA SMZ IMETEKELEZA ILANI KWA ASILIMIA 97.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akihutubia Wana CCM na Wananchi katika Kongamano la UWT Pemba.


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zabnzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi amesema mafaniko yaliyofikiwa katika Nyanja za kiuchumi,kijamii na kisiasa visiwani Zanzibar yametokana utekelezaji na usimamizi bora wa Sera za CCM.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Tanzania lililofanyika katika uwanja wa kufurahishia Watoto  Tibirinzi Wilaya ya Chake – chake  Kusini  Pemba.

Alisema Serikali ya awamu ya saba chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amefanikiwa kusimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa kuwaletea wananchi maendeleo mijini na vijijini.

Dk.Mabodi alieleza kuwa Serikali imeweza kuimarisha sekta mbali mbali za Afya,Elimu,Kilimo,Uvuvi,Barabara,Maji Safi na Salama, Makaazi,miundombinu ya nishati ya umeme,miundombi ya usafiri wa anga na nchi kavu,michenzo na utamaduni kwa asilimia 97.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi alieleza kuwa mafanikio hayo yamechochewa na kuimarika kwa hali ya amani na utulivu nchini na amesema CCM itahakikisha inaendelea kulinda na kuimarisha amani hiyo kwa maslahi ya Taifa.

Aidha Dk: Mabodi alisema Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuisimamia Serikali itekeleze mambo muhimu yanayogusa maisha ya kila siku ya wananchi wa makundi mbali mbali.

Ameeleza kuwa siri ya mafanikio hayo inatokana na Baraka za waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 pamoja na Muungano ambazo ndio dira ya viongozi wa sasa katika kutekeleza maendeleo endelevu.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka amesema kongamano hilo la kumpongeza Dk.Shein litakuwa ni chachu ya kuwaongeza hamasa na mshikamano kwa wanawake wa Zanzibar.

Akisoma risala ya UWT Katibu Mkuu wa Umoja huo Mwl.Queen Mlozi alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni kupongeza na kueleza masuala mbali mbali yaliyotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

Amesema Kupitia kongamano hilo wanawake wamejitathimini juu ya masuala mbali mbali waliyofanikiwa katika Nyanja za uongozi,utendaji pamoja na fursa mbali mbali za kielimu na kijamii.

Alizungumza Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Bi.Tunu Juma Kondo amasema wanawake visiwani humo kupitia Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Saba chini ya Dk.Ali Mohamed Shein wamefanikiwa kupata fursa za uongozi, elimu na kujiajiri wenyewe kupitia fursa za ujasiriamali.

Wakizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ), wameeleza kuwa chini ya uongozi wa Dk.Shein Sekta ya Elimu imeimarika sambamba na ujenzi wa skuli 10 za ghorofa zilizotajwa katika Ilani ya CCM.

Waziri wa Mawasiliano,Miundombinu na Usafirishaji Dk.Sila Ubwa Mamboya, amesema Serikali imejenga barabara mbali mbali za kiwango cha lami mijini na vijijini ili kuwarahisishia wananchi huduma za usafiri.

Naye Naibu Waziri wa Afya Mhe.Harusi Suleiman alisema  Serikali imejenga Vituo vya Kisasa vya Afya na kuziongezea hadhi hospitali mbali mbali kutoka ngazi za vijiji hadi kuwa hospitali za Wilaya, sambamba na utoaji wa huduma bure za afya.

Kwa upande wake Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe.Moudline Castico  masuala ya uwezeshaji Serikali imetoa mikopo kwa wajasiriamali 500 yenye thamani ya zaidi ya shilingi biloni moja wengi wengi wao wakiwa wanawake.

Mhe.Moudline Serikali imeendelea kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto ili waishi kwa amani bila kuvunjiwa haki zao za msingi.

Naye Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe.Salama Aboud alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Dk.Shein Serikali imeimarisha miundombinu ya maji safi na salama sambamba na kuanzisha mradi mkubwa wa kuinua uchumi wa Zanzibar wa utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia.

Naye Waziri wa Viwanda na Masoko Mhe.Amina Salum, alieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Dk.Shein Serikali imeanzisha viwanda vikubwa na vidogo vidogo ili wananchi wajiajiri wenyewe.

Aidha Balozi Amina aliongeza kuwa wananchi wamenufaika na kilimo cha zao la karafuu baada ya Serikali kuongeza bei ya zao hili kwa kiwango cha soko la Dunia hali ambayo wananchi wameweza kuondokana na uchumi tegemezi.

Naye Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Chumu Kombo Khamis, alisema Sekta ya Utalii imeimarika kwa kasi na kufikia zaidi ya watalii 5000 ambapo imepita malengo la Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 iliyotaja kufikia idadi hiyo kabla ya mwaka 2020.

Alieleza kuwa Serikali imeimarisha taasisi zake za masuala ya Habari ziliwemo Shirika la Magazeti Zanzibar pamoja na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kwa kuweka miundombinu ya kisasa ili wananchi wapate habari za uhakika kwa wakati.

Akizungumza Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma amesema Serikali ya awamu ya saba imewawekea mazingira rafiki wanawake nchini kuwania nafasi za uongozi katika vyombo vya kutunga sharia ili wazisaidie jamii.

Akitoa shukrani kwa Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Thuwaiba Kisasi amewapongeza wananchi mbali mbali hasa wanawake walioudhuria katika kongamano hilo.

Aliwataka wanawake wote nchini kuunga mkono na kuthamini juhudi mbali mbali zinazotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk.Ali Mohamed Shein.

Kongamano hilo limeudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake, Serikali pamoja na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni