Alhamisi, 5 Januari 2017

KATIBU MKUU NA UJUMBE WAKE WAWASILI AFISI KUU CCM, ZANZIBAR


Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia na Mjumbe wa NEC Idara ya Itikadi na Uenezi CCM - Zanzibar Ndugu Waride Bakari Jabu alipowasili Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui - Zanzibar.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Ndugu Alhaj Borafia.


Katibu wa NEC  Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akisalimia na Watumishi wa CCM Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui - Zanzibar.


Ujumbe wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana wakitia saini katika kitabu cha wageni Afisi Kuu ya CCM - Zanzibar.



Ujumbe wa CCM kutoka Tanzania Bara ukiongozwa na Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana wakielekea katika eneo la historia ambapo aliuwawa Muasisi wa ASP, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Mheshimiwea Sheikh Abeid Amani Karume


Ujumbe wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana wakipewa maelezo mafupi  sehemu ya historia ambayo aliuwawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mheshimiwa Abeid Amani Karume  hapa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.


Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar  Ndugu Vuai Ali Vuai akitoa maelezo mafupi  sehemu aliyouwawa Muasisi wa ASP, Mheshimiwa Sheikh  Abeid Amani Karume.
Katibu Mkuu na Ujumbe wake kutoka Tanzania  Bara wakitoka sehemu ya historia ambayo aliuwawa Muasisi wa ASP na Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Sheikh Abeid Amani Karume


Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake wakitoka katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui  Zanzibar.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake wakiagana na Viongozi mbali mbali wa Chama Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui kwa ajili ya kwenda kupumzika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni