UTANGULIZI:
ASSALAM
ALEYKUM,
Ndugu
Wandishi wa Vyombo mbali mbali vya Habari.
Awali ya yote, napenda
nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu, ardhi na vyote
viliomo ndani yake, kwa kutujaalia uzima na afya njema. Aidha, nachukua nafasi
hii kwa mara nyengine tena kuwashukuru nyinyi waandishi wa vyombo mbali mbali
kwa kukubali wito wetu na kuhudhuria kikao hiki.
Ndugu
wandishi wa Habari.
Mnafahamu fika kwamba
kila ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari ya kila mwaka, Chama Cha Mapinduzi huwa
kimo katika vuguvgu la kuadhimisha kuzaliwa kwake tangu vyama vya TANU na ASP
vilipoungana na kuunda Chama kimoja (CCM) tarehe 5, Februari 1977 tukio ambalo
lilifanyika katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Ndugu wandishi wa Habari.
Sasa Maadhimisho hayo
yatafanyika katika ngazi za Mikoa, na tayari kila Mkoa umeshaandaa ratiba za
shughuli mbali mbali ambazo watazifanya katika Mikoa yao.
Shughuli hizo ni kama
zifuatazo:-
Kutakuwa
na zoezi la Usafi wa Mazingira katika maeneo ya Mikoani, Wilayani, Majimboni,
Matawini na Maskani za CCM.
1. Shughuli
za kukagua Wagonjwa na kuwafariji Wazee wasiojiweza.
2. Kutakuwa
na Mikutano Mikuu ya Ngazi mbali mbali.
3. Mikutano
ya Kamati za Siasa.
4. Mikutano
ya Halmashauri Kuu za Jimbo.
5. Zoezi
la kupanda miti katika maeneo mbali
mbali ya kijamii na vyanzo vya Maji.
6. Kutakuwa
na michezo ya aina mbali mbali kama vile mashindano ya resi za baiskeli, michezo ya
nage, michezo ya Bao, Mpira wa Basketboli pamoja na Mpira
wa Miguu.
7. Makongamano
yatakayoelezea historia ya CCM, mafanikio ya miaka 40 ya CCM pamoja na Utekelezaji
wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2015 –
2020.
Ndugu
Wandishi wa Habari.
Pamoja na mambo yote
hayo tuliyoeleza lakini pia yanaweza kujitokeza mengine ambayo hayakutajwa katika
taarifa hii, lakini Mikoa watayafanya katika kuadhimisha kuzaliwa kwa CCM kwani
mwaka wote huu wa 2017 ni mwaka wa kuadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa kwa Chama
hicho.
Ndugu
Wandishi wa Habari.
Mwisho naomba kutoa
wito kwa Wana CCM wote kushiriki kwa wingi katika Mikoa yao kuadhimisha siku hiyo
muhimu ya kuzaliwa kwa Chama chetu cha CCM. Aidha, Chama Cha Mapinduzi
kinawashukuru kwa dhati kabisa Wana CCM na Wananchi wote wa Jimbo la Dimani pamoja
na Kata za Mikoa ya Tanzania Bara
iliofanya Uchaguzi kwa kupiga kura kwa
amani na utulivu mkubwa hatimae kukichagua kwa kishindo kikubwa Chama Cha CCM, kwa kujua kwamba CCM ndio
kimbilio la wanyonge na ni Chama kinachotekeleza Ilani yake ya Uchaguzi kwa
makini na kwa wakati.
Baada ya maelezo hayo, nikushukuruni tena kwa kunisikiliza na nikutakieni kila la kheri katika majukumu ya kazi zenu.
Ahsanteni
sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni