Jumapili, 21 Juni 2020

DK.KHALID ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS ZANZIBAR

 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallos  Nyimbo (kushoto) akisalimiana na Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed(kulia), aliyefika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

 Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar.
 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallos  Nyimbo (kushoto) akimkabidhi mkoba wenye fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed(kulia), hafla iliyofanyika Afisi Kuu CCM Kisiwandui Zanzibar. 




 Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed(kulia),akisalimiana na kada mkongwe wa CCM Baraka Shamte(kushoto), mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari.





           Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohamed,leo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Cassian Gallos Nyimbo, huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. 

Amesema endapo Chama kitamuona anafaa na kumpatia ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, atashirikiana na wananchi wote kuendeleza maendeleo yaliyofikiwa na Dk.Shein.

Amesema ameamua kuingia katika mchakato wa kuomba nafasi hiyo ya Urais baada ya kujitathimini na kuona anao uwezo na nguvu za kuwatumikia wananchi kwa uadilifu mkubwa.

Amefafanua kuwa akipewa nafasi hiyo ataongoza kwa kufuata kanuni,sera,miongozo na taratibu zilizopo nchini kisheria.

Katika maelezo yake Dkt.Khalid, ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Donge ameongeza kuwa atafuata Katiba zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Dkt.Khalid, ameeleza kuwa katika kuimarisha maendeleo ya nchi atahakikisha anafuata dira ya maendeleo ya nchini ili kwenda sambamba na mikakati ya kiuchumi katika nyanja za Kimataifa.

"Namshukru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema na kunipa uwezo wa kuja kuchukua fomu hii ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar, naendelea kuwaomba wananchi wenzangu mniombee duwa niweze kutimiza dhamira yangu hii ya kuwatumikia wananchi", amesema Dkt.Khalid.

Amesema maendeleo yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 10 ya Uongozi wa Dk.Ali Mohamed Shein, yamefikiwa kutokana na juhudi za kila mwananchi na yeye akiwa ni miongoni mwao.

Amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020, iliyoleta maendeleo mijini na vijijini.

Dkt.Khalid amekuwa ni Kada wa CCM wa 15 anayeomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar toka kuanza kwa zoezi la utoaji wa fomu hiyo katika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwanduzi Zanzibar Juni 15,mwaka 2020.   






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni