Kada mwingine aliyejitosa katika kinyanga'nyiro hicho ni Meja Jenerali Mstaafu Issa Suleiman
Nassor alisema anakishukuru chama kwa utaratibu walioweka wa demokrasia ya kila mwanachama kujitokeza kugombea nafasi hiyo.
Alisema amefurahia utaratibu uliowekwa na CCM na kwamba endapo akipatiwa ridhaa na chama kupeperesha bendera ya kinyanga'nyiro atatekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya chama.
"Ikiwemo kusimamia hali ya amani tulionayo na sisitiza hicho kitu umoja na uzalendo nataka kila
mtu hajue ana nafasi ya kuhakikisha ataifanyia nini Zanzibar,"alisema
Alisema yeye ni muhumini wa muungano na nitaendeleza muungano uliopo kwa mujibu wa katiba inavyoeleza ataimarisha uchumi kadri itakavyokwenda na kadri ilani ya CCM inavyozungumza.
"Na nitaendeleza yale yote yaliyofanywa na viongozi waliotangulia kama nitapata ridhaa ya wananchi basi tutahakikisha uchumi wa Zanzibar una kuwa kwa maslahi ya wananchi kwa jumla na si kwa maslahi ya watu wachache au mtu binafsi,"alisema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni