MAKADA wengine wanne leo
wameendelea wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa
Zanzibar,ambao ni Waziri wa Maji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa,Kada wa CCM Mwatum
Mussa Sultan,Kada wa CCM Mwl.Haji Rashid Pandu na Kada wa CCM Dk.Abdul-halim
Mohamed Ali ambao wamefikisha idadi ya makada 13 waliochukua fumu hizo toka zoezi
hilo lianze Juni 15,mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa
Habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo, majira ya saa 4:00 asubuhi
Waziri wa Maji Prof.Makame Mnyaa
Mbarawa,hafla hiyo imefanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Amesema anamshukru Mwenyezi Mungu
kwa kumjaalia uwezo na nguvu za kushiriki katika mchakato huo ambao ni muhimu
katika hisoria mpya ya maisha yake.
Amesisitiza kwamba jambo muhimu
kwa sasa ni kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kufungua milango ya neema katika
zoezi hilo liendelee kufanyika kwa ufasini na afikie malengo yake ya kuwa Rais wa
Zanzibar.
Aidha amesema atazungumza kwa
upana mambo mbali mbali juu ya mbio zake za kuwania Urais wa Zanzibar pindi
atakapokamilisha zoezi la kujaza fomu hizo.
Naye Mwatum akizungumza na
Waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo, alikipongeza Chama Cha
Mapinduzi kwa ukomavu wake wa demokrasia ya kuwaruhusu makada wake wa jinsia
zote kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi kupitia Chama hicho.
Amewataka Wanawake nchini
kuendelea kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ili kufikia
asilimia 50 kwa 50 katika vyombo vya kufanya maamuzi.
Amesema amechukua fomu hiyo ili
kuwahamasisha wanawake wengine wajitokeze katika kuwania nafasi mbali mbali za
uongozi kama walivyo wanaume.
"Nachukua nafasi hii
kumuomba Mwenyezi Mungu anisimamie katika safari yangu hii ya kuomba ridhaa ya
kuwa Rais wa Zanzibar", amesema Mwatum.
Pamoja na hayo amesema hatoweza
kutoa maelezo mengi kwa waandishi wa habari mpaka atakapokamilisha zoezi la kujaza fomu hiyo.
Kwa upande wake kada wa CCM
Mwl.Haji Rashid Pandu,akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo amesema
lengo lake ni kutetea maslahi ya wakulima ambao mchango wao ni mkubwa katika
maendeleo ya nchi.
Kada huyo ambaye kitaaluma ni
mwalimu,amesema lengo lake ni kusimamia kwa vitendo falsafa ya mapinduzi ya
kilimo nchini.
Akizungumza kada wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM) Dk.Abdul-halim Mohamed Ali aliyechukukua fomu ya kuomba ridhaa
ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM,amesema lengo ni kuhakikisha Zanzibar
inakuwa na maendeleo endelevu.
Dkt.Abdulhalim, amesema endapo
Chama Cha Mapinduzi kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kuwania kiti
cha Urais, atakuwa mstari wa mbele kutatua changamoto za wananchi bila ubaguzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni