Jumamosi, 22 Desemba 2018

NAIBU KATIBU MKUU WA UVCCM ZANZIBAR NDG.MUSSA HAJI MUSSA AWAUHUTUBIA VIJANA WA UVCCM .

NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Mussa Haji Mussa akiwahutubia vijana wa UVCCM Zanzibar katika hafla ya mapokezi yake.


NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) anayefanyia kazi zake Zanzibar  Ndugu Mussa Ali Mussa leo amewasili nchini kwa mara ya kwanza toka ateuliwe kushika nafasi hiyo ya uongozi ndani ya Taasisi hiyo.

Mara baada ya kuwasili Zanzibar Naibu huyo amepokelewa na viongozi wandamizi wa Jumuiya hiyo pamoja na Familia yake kwa shangwe na furaha kubwa, huku wakimpa maneno ya kumtia ari na hamasa ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Hafla ya mapokezi hayo imefanyika katika Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar katika Uwanja wa Gymkhana Kikwajuni ambapo kiongozi huyo amezungumza na viongozi,watendaji na wanachama wa ngazi mbali mbali za Taasisi hiyo ya Vijana.

Ndugu Mussa akiwahutubia wanachama hao amesema ataendeleza mambo mema ya kuleta maendeleo endelevu ndani ya Jumuiya na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla, huku akisisitiza kuwa atashirikiana na viongozi wenzake wa jumuia kwa ngazi zote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni