Jumanne, 11 Desemba 2018

DK.SHEIN :USHINDI WA CCM JANG'OMBE NI MAANDALIZI YA KUANDIKA HISTORIA MPYA YA USHINDI WA CCM 2020



WAJUMBE wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa ambao pia ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saada Mabodi(wa kwanza kulia) , Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Idd (wa kwanza kushoto), Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto), wakiimba mara baada ya kuingia katika Ukumbi wa Mikutano wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Kisiwandui Zanzibar.

WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakiwa katika Kikao cha kawaida kinachofanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, huko Kisiwandui Afisi Kuu Zanzibar.






WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakiwa katika Kikao cha kawaida kinachofanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, huko Kisiwandui Afisi Kuu Zanzibar.



WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakiwa katika Kikao cha kawaida kinachofanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, huko Kisiwandui Afisi Kuu Zanzibar.


 MJUMBE wa Kamati Kuu CCM Taifa Balozi Seif Ali Idd (kushoto), akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi  Taifa, Ndugu Abdalla Haji Haidar (kulia), mara baada ya kuwasili Kisiwandui kwa ajili ya Kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar.

  MJUMBE wa Kamati Kuu CCM Taifa Balozi Seif Ali Idd (kushoto),akisalimiana na  Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa ambaye pia ni Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Mwl.Kombo Hassan Juma,katika Kikao cha Kamati Maalum kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi (kulia) mara baada ya kuwasili Kisiwandui kwa ajili ya Kikao cha Kamati Maalum

 BAADHI ya Viongozi mbali mbali wa CCM wakisubiri Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kwa ajili ya mapokezi ya Kikao cha Kamati Maalum.

 MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa  Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar  Mhe. Nagma Giga mara baada ya kuwasili Kisiwandui leo.


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

Kikao hicho cha Siku Moja kimeanza majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.

Kupitia Kikao hicho Makamu Mwenyekiti Dk. Ali Mohamed Shein, amewapongeza Wanachama, Watendaji na Viongozi wote wa CCM kwa kufanikisha Ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe ambapo aliyekuwa Mgombea wa CCM Mhe.Ramadhan Hamza Chande alishinda kwa  kura 7,274 sawa na asilimia 90.5.

Dk.Shein amesema ushindi huo haukuwa wa bahati mbaya bali ulitokana na ridhaa ya Wananchi wa Jimbo hilo kwa kuridhishwa na kasi ya Utekelezaji kwa vitendo Sera na mipango endelevu ya maendeleo inayotekelezwa kupitia Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Katika maelezo yake Dk.Shein amewasisitiza Wajumbe wa Kikao hicho na Wana CCM kwa ujumla kuwa Ushindi wa CCM Jang’ombe ni sehemu ya maandalizi ya Ushindi wa Kihistoria katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Pamoja na hayo amewakumbusha  Wajumbe wa Kikao hicho kwamba wanatakiwa kuwa mfano bora wa kulinda maadili, miongozo na kanuni za Chama Cha Mapinduzi.

Baada ya kutoa nasaha hizo Mwenyekiti wa Kikao hicho Dk.Shein amefungua Kikao na kupokea na kujadili kwa kina taarifa mbali mbali kutoka katika Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi.

Kikao hicho ni cha kawaida kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977 Toleo jipya la 2017,Ibara ya 108 (2), inayofafanua kwamba Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itafanya mikutano yake ya kawaida mara moja kila miezi mitatu.   

Viongozi wakuu na Wajumbe wa Kikao hicho walioudhuria ni pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni