NAIBU
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Ndugu Othman Ally Maulid akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa Ofisi rasmi katika hafla iliyofanyika leo katika
Afisi Kuu ya Wazazi Kikwajuni Unguja. |
NAIBU
Katibu Mkuu mtaafu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Mhe.Najma Giga akitoa nasaha kwa viongozi na
watendaji wa Jumuiya hiyo. |
BAADHI
ya Viongozi na Watendaji wa Jumuiya ya Wazazi wakifuatilia kwa makini nasaha
mbali mbali zinazotolewa katika hafla hiyo ya makabidhiano. |
NA
IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Ndugu
Othman Ally Maulid amesema atasimamia kwa vitendo ibara ya Tano ya Katiba ya
CCM ya mwaka 1977 toleo jipya la mwaka 2017 inayoelekeza kuwa Ushindi wa CCM ni
lazima kwa kila Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Chaguzi ndogo ndogo na Uchaguzi
Mkuu.
Kauli
hiyo ameitoa leo katika hafla ya makabidhiano ya Ofisi baina yake na aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhe. Najma Giga huko katika Afisi ya Wazazi
iliyopo Mpirani Kikwajuni Zanzibar.
Ndugu
Othman amesema kwamba pamoja na majukumu mbali mbali ya kiutendaji
yanayoikabili Jumuiya hiyo bado ana jukumu la msingi la kuhakikisha Chama Cha
Mapinduzi kinashinda katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Ameeleza
kuwa kila Taasisi nchini ina malengo yake hivyo kwa upande wa CCM ambayo ni
taasisi ya Kisiasa ni lazima iwekeze mipango yake katika kuhakikisha inashinda
na kuendelea kuongoza wananchi kwa misingi ya uadilifu.
Katika
hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo ameahidi kushirikiana na Watendaji, Viongozi
na Wanachama wote wa Jumuiya na Chama kwa ujumla ili kuleta ufanisi wa
kiutendaji ndani ya Jumuiya hiyo.
Aidha
amewasisitiza viongozi na watendaji wa Jumuiya hiyo kuvitumia vyombo vya Habari
nchini kutangaza miradi mbali mbali inayotekelezwa na Serikali chini ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Dkt.John Pombe Magufuli.
Katika
maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo amesema atatumia miongozo mbali mbali ya
CCM na Jumuiya ya Wazazi kubuni mipango mbali mbali ya maendeleo itakayosaidia
kuleta ufanisi.
Naye
Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Wazazi Najma Giga, amewashukru viongozi na
watendaji wote wa jumuiya ya wazazi kwa ushirikiano waliompa wakati wote
alipokuwa kiongozi wa Taasisi hiyo.
Aliwasisitiza
Watendaji wa Taasisi hiyo kushirikiana vizuri na Naibu Katibu mpya ili
kuendeleza mafanikio yaliyopo ndani ya Jumuiya hiyo.
Aidha
ameeleza kuwa licha ya kumaliza muda wake wa kiuongozi ndani ya Jumuiya hiyo
bado ataendelea kuwa karibu katika kushiriki masuala mbali mbali ya kimaendeleo
ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya hiyo.
Akitoa
shukrani Mkuu wa Utawala msaidizi Ndugu Mustafa Rashid, amesema kwa niaba ya
watendaji wenzake watafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Naibu Katibu Mkuu
huyo ili kufikia malengo endelevu yaliyowekwa na jumuiya hiyo katika kuimarika
kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni