VIONGOZI na Wanachama wa UWT wa Mkoa wa
Magharibi wakiwa katika hafla ya kukabidhi komputa nne ya Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk, iliyofanyika katika Ofisi za CCM Kiembe
Samaki Unguja.
MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk,amewasihi Viongozi na
Wanachama wa CCM kufanya Kazi za Chama Cha Mapinduzi kwa bidii ili kuandaa Mazingira
rafiki ya Ushindi wa Mwaka 2020.
Rai hiyo aliitoa wakati akikabidhi Komputa
Nne zenye Thamani ya Shilingi Milioni Nane kwa Ofisi za UWT Zanzibar ambazo ni
Afisi Kuu ya UWT Zanzibar, UWT Mkoa wa Magharib,UWT Wilaya ya Dimani na UWT
Wilaya ya Mfenesini ambapo kila Ofisi imekabidhiwa komputa Moja,Hafla hiyo imefanyika
katika Ofisi za CCM huko Kiembembe Samaki Unguja.
Mhe.Amina amesema ili Chama kishinde katika
Uchaguzi Mkuu ujao kila mwanachama anatakiwa kuweka mbele maslahi ya CCM badala
ya maslahi binafsi.
Katika maelezo yake Mhe.Amina, ameeleza kuwa Vifaa
hivyo ni mwendelezo wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020,ikiwa ni
sehemu ya kutekeleza kwa vitendo ahadi alizozitoa kwa Wananchi.
Pamoja na hayo amewaahidi Akina Mama wa Mkoa
wa Magharibi kuwa ataanzisha Vikundi vya Ujasiriamali ili kuwakwamua kiuchumi na waweze kujiajiri wenyewe na kuondokana katika wimbi la umaskini.
Amewasihi Viongozi na Wanachama wa UWT
kuthamini juhudi za kimaendeleo zinazofanywa na Viongozi hao ili wazidi kupata
nguvu na Uthubutu wa kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi.
Akizungumza katika Hafla hiyo Mgeni rasmi
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo,amempongeza Mbunge huyo Mhe. Amina na Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo ambao wamekuwa karibu na Wananchi kwa
kutekeleza kwa Vitendo Ilani ya CCM.
Ndugu
Tunu, amewataka Viongozi na Watendaji waliokabidhiwa Komputa hizo kuzitunza
vizuri ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuhakikisha shughuli za
kiutendaji za UWT zinatekelezwa kwa ufanisi zaidi.
Amesema Viongozi wa Chama na Serikali wanatakiwa
kufuata nyayo za Viongozi Wakuu ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa katika kuwatumikia Wananchi kwa
uadilifu.
Awali Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi
Ndugu Zainab Ali Maulid,amesema Umoja na Mshikamano ndio siri ya mafanikio ya
kuimarika kwa Umoja huo.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni